Huu ni mtazamo wangu - Nchi hii tujaribu kuwapa wachaga

Rejea heading yangu hapo juu ni kua kwa mtazamo wangu na tembea yangu Tanzania mikoa mingi palipo na kabila la mchaga lazima kuna kamaendeleo fulani na pia kama ukiwachunguza hili kabila utaona ni watu wanaopenda sana maendeleo na si kwao binafsi tu la hasha hata kwa jamii inayowazunguka! Tafadhali sana mniwie radhi sijaleta mada hii kwamba naingiza ukabila na wala mimi sio mchaga bali ni mtazamo wangu tu. Ili tuondokane na umasikini uliokidhiri hapa nchini kwetu na ndoto ya maisha bora kwakila mtanzania ni sawa na ile ndoto yakutaka kujenga gorofa angani! basi ni mchango wangu tu na mawazo yangu tu hembu tujaribu kuwatesti hawa jamaa na kama kuna mtu anapendekeza kabila jingine anakaribishwa kuchangia mada hii.

Jamani hivi hamuoni kama inji hii inaliwa? Kele Uwiii!
Tupeni nafasi tuongose japo kidogo tuwaletee utajiri inji hii jamani.
 
Eee bana una mawazo mazuri sana ila ndo hivyo si rahisi watu wakakuelewa manake watu wengi hasa kutoka yale makabila yaliyo nyuma zaidi kimaendeleo wanawaogopa wachagga sana na wamepandikizwa kitu kibaya kufikiri kwamba wachagga ni wezi. Hii ilitokana hasa na historia ya nchi yetu wakati wa UJAMAA. Wakati ule kuwa na fedha au kuwa tajiri ilionekana kama dhambi na serikali ilikuwa inawafuatilia sana watu wenye hela na walikuwa wanatiwa matatani. Kumbuka wakati ule hata kuwa na nyumba ya kupanga ulikuwa unaonekana fisadi na kama una nyumba 2 ndio usiseme utaeleza umepata wapi pesa za kujenga.Sasa hawa ndugu zetu wachagga wengi walishaingia kwenye biashara tangu zamani na walikuwa na pesa na walijenga majumba makubwa kwao na mijini pia. Kilichotokea watu hawakuweza kutambua walipata fedha wapi kwani watu wengi walikuwa hawajishughullishi na biashara waliona kama uhuni au wizi.Ni kweli ukienda uchaggani kuna maendeleo sana. Kulingana na takwimu hasa za miaka ya sitini na sabini ulikuwa huwezi kufananisha Moshi na sehemu nyingine Tz na hadi sasa Kilimanjaro vijijini hakuwezi kufananishwa na sehemu nyingine yeyote vijijini kiujumla kuna maendeleo sana.Nakumbuka wakati fulani waliandika katika kitabu kwamba MOSHI IS A DEVELOPED AREA IN A DEVELOPING COUNTRY. kwamba Moshi ni kama nchi iliyoendelea ndani ya nchi maskini.Serikali tangu enzi za Nyerere ilifanya makusudi makubwa sana kuwazuia wachagga wasiendelee kwa kasi waliyokuwa nayo, lakini voingozi wengi walishangazwa na waha akina Mangi kwani ndio walifanya juhudi zaidi. Nyerere aliwaogopa sana Wachagga kwani ndio waliokuwa mstari wa mbele kupinga sera za kimaskini za Ujamaa. wapo wengi tu waliopingana na Nyerere na ili kujilinda Nyerere alichofanya ni kuwafukuza serekalini. Mfano ni Edwini Mtei ambaye alitaka mabadiliko kutoka Ujamaa miaka ya 70 lakini mwisho wake Nyerere alimwona hatari kwa Ujamaa na aliishia kumtupa chini. Akina Maliti huyu naye alikuwa hata balozi wa Tz UN na ameandika vitabu vizuri sana kwasababu mawazo yake yalikuwa mbele sana walikosana na Nyerere na aliishia kuondolewa ili ujamaa upone.serekali ya awamu ya 1 ilifanya jambo 1 baya sana kwa akina Mangi kuanzia miaka ya 70 mpaka 90 mwanzoni. Mimi nikiishi na wazazi wangu waliokuwa wakifanya kazi Moshi kama walimu, walinieleza baadaye kwamba nisingeweza kufaulu darasa la 7 kama wasingenihamisha kutoka shule ambayo walikuwa wakifundisha ambayo ipo Moshi vijijini. Sababu ilikuwa mpango wa serekali kwamba watu wa Kilimanjaro vijijini waliwekewa wastani wao wa kufaulu darasa la 7 ambao ulikuwa mkubwa mno zaidi ya 96% pass mark! Lengo lilikuwa kwamba wasiende mashule ya serekali kwani walionekana tayari ni wengi kule na pia serikali ilisema wao akina Mangi wanafedha nyingi za kahawa na hivyo wanaweza kuwapeleka watoto wao shule binafsi kwa hiyo hakuna kufaulu. La ajabu ni kwamba hawa jamaa walijenga mashule mengi binafsi na Moshi imekuwa ikiongoza kwa mashule mengi tangu wakati wa uhuru na hadi leo bado shule za sekondari ni nyingi kuliko mkoa wwowote. Kuna sekondari zaidi ya 300 Kilimanjaro pekee wakati mkoa unaofuatia nadhani una shule 118.Niseme tu kwa kuishi kwangu Moshi nimejifunza kwamba wachagga ni watu tofauti kidogo na makabila mengine ya Tz. Hawa jamaa wanapenda kazi sana. Akina Mangi wanaongoza kwa wingi vyuoni na si rahisi hata kuwagundua kwani wengi wao hawajioneshi. Binafsi nafahamu wachagga wengi waliomatajiri wakubwa lakini utashangaa walivyo wa kawaida.Nilikuwa na Mkenya 1 na alishangaa kusikia Wachagga ni Watz kwani kule Kenya ni wengi na wanawachalenji wakenya sana. Hawa ndugu wana uvumilivu mkubwa na ujasiri wa kufanya mambo mengi.Tatizo kubwa la tz ni kwamba tumekuwa tukiwapa uongozi watu ambao hawana vision na matokeo yake sote tumeyaona. Pengine sasa tufanye uamuzi mgumu wa kuwapa watu ambao ni aggressive kwenye maendeleo kama akina Mangi. Hawa jamaa ni wapiganaji sana angalia akina Mbowe, Mvungi, Mbatia, Lema naye nadhani ni wa huko na wenyeviti wa makampuni mbalimbali hasa binafsi. Lakini kwa ujumla serekali ya mafisadi hawapendi kuwapa uongozi wa nchi hii kwa sababu wanazojua wao.
Crackpot+Mbege
 
Ni wakati sasa tupime kila mtu anauwezo gani, ili kuwe na specialisation kwenye kila sector. Bila hivyo nchi haitaendelea hata centimetre....
 
huwezi kumpa mtu uongozi kwa sababu ya kabila,kwani Makufuli mchaga?Mwandosya mchaga?selelii Mchaga?Mwakyembe mchaga?Olesendeka Mchaga,Dr slaa Mchaga?, Sitta mchaga? Mnyika mchaga? baadhi ya wachaga mafisadi ni.Mlamba na mkurugenzi Tra,kimei, na wengine wengi! nawakubali tu wachache

nafikiri hoja yake ina kila sababu ya kuheshimiwa,wachaga wanapenda maendeleo,hilo hakuna ubishi,tujaribishe tunaweza toka hapa tulipo
 
Jaribuni kuwapa mnakumbuka enzi za mrema alionjeshwa cheo mambo yalivyoenda freeshaa
 
Hivi mnaongelea maendeleo gani ambao Mchagga anayo! Kukukopa bank, Akiba, Boa, CRDB, NMB, Na kufungua bar za uchochoroni? Tunapoongelea Maendeleo tunaongelea nguvu za kiuchumi, naomba Mchagga yoyote anitajie Wachagga wangapi wanamiliki benki apa Tanzania, Mchagga wanamiiliki makampuni Meli ya usafirishaji, Wachagga wangapi Wanamiliki viwanda vinavyojulikana Kimataifa, Wachagga wangapi wanamiliki Real estate apartements, Wachagga wangapi wanamiliki makampuni ya bima, Wachagga wangapi wanamiliki vyuo vikuu, Wachaga wangapi wanamiliki Hospitali zenye viwango.Kwa uchache hayo nimeyataja ndio msingi wa maendeleo
 
Je wamjua Mengi au wewe mgeni nchi hii nitajie mfanyabiashara mwingine mbongo anayemfikia. Au yeye siyo McCabe kwa ufahamu wako.

Taja Mengi utajiri wake, usinilete habari ya Mwenyekiti wa makampuni, unajua maana yake? Huyu Mengi wako kashindwa kununua Kilimanjaro Hotel, kashindwa Bei, kanunua muarabu, wewe ukiona mchagga kajenga hotel kaiandika Rombo Hotel au Mwika Hotel wewe unaona huwo ndio utajiri, Maendeleo udhani mchezo wewe
 
Michaeli Shirima anamiliki aslimia zaidi ya 50 ya Presicion Air, wapo wengi tu wenye viwanda, mashirika madogo ya ndege, majumba makubwa, ndio mahoteli, kwa real estate hawa jamaa ndio usiseme nenda Arusha, Dar, angalia Kariakoo, machache tu hayo. Acha wale wengine wengi sana wenye mitaji ya bilioni 2 hadi 10.
 
Tanzania lazima ijenge system yenye kuweka set of values.tukiwa na system(sio kamati ya ccm) ambayo itateuwa mtu fulani anafaa kuwa rais na baada ya kuwa rais atafanya mambo yote bila kuingilia misingi(principles or values) ya utanzania.tukifikia hapa tanzania inaweza kuongozwa na mtu yeyote hata mwenye ugonjwa wa akili.
 
Taja Mengi utajiri wake, usinilete habari ya Mwenyekiti wa makampuni, unajua maana yake? Huyu Mengi wako kashindwa kununua Kilimanjaro Hotel, kashindwa Bei, kanunua muarabu, wewe ukiona mchagga kajenga hotel kaiandika Rombo Hotel au Mwika Hotel wewe unaona huwo ndio utajiri, Maendeleo udhani mchezo wewe

Acha roho ya kwanini
 
Michaeli Shirima anamiliki aslimia zaidi ya 50 ya Presicion Air, wapo wengi tu wenye viwanda, mashirika madogo ya ndege, majumba makubwa, ndio mahoteli, kwa real estate hawa jamaa ndio usiseme nenda Arusha, Dar, angalia Kariakoo, machache tu hayo. Acha wale wengine wengi sana wenye mitaji ya bilioni 2 hadi 10.
Angalia vizuri bandiko langu, nitajie Wachagga wamiliki, unanilete Mambo ya asilimia, unaongelea Karikaoo gani Wenye Maghorofa mengi Kariakoo, Wahindi, Waarabu, Wapemba, Wakinga, then ndio Wachagga, na hotel za Wachagga zipo Manzese na Sinza, na Kimara, ungeniambia Wahindi ningekuelewa
 
na bado utakufa na roho ya kwanini hujamalizana na CDM unaanza vita na wachaga kwa kifupi tu wachaga wako tofauti na makabila mengine na wanauwezo wa kufanya kitu kikaonekana ndio maana biashara za kati nyingi zinafanywa na hawa ndugu na hata uchumi wa mchaga mmojammoja uko juu tofauti na makabila mengine ni sawa na brazil leo washindwe kuwa na wachezaji wengi wenye vipaji na wamesambaa duniaani .ni karama yao ndo Mungu alivyowabariki! Mchaga kufanikiwa kibiashara ni talanta huwezi kuitoa ndivyo tulivyobarikiwa hata ubisheje tuko juu
 
Taja Mengi utajiri wake, usinilete habari ya Mwenyekiti wa makampuni, unajua maana yake? Huyu Mengi wako kashindwa kununua Kilimanjaro Hotel, kashindwa Bei, kanunua muarabu, wewe ukiona mchagga kajenga hotel kaiandika Rombo Hotel au Mwika Hotel wewe unaona huwo ndio utajiri, Maendeleo udhani mchezo wewe
We wachaga wengi tu wanamahoteli Riki hotel ni ya nan?Kibo hotel ni ya nani?Embassy hoteli ni ya nani?Moshi hoteli ni ya nani?Keys hotel ni za nani?
 
Sikujua kama Tanzania uongozi ni wa kupeana!

Mie nilijuwa anachaguliwa mtu kwa sifa zake na si kabila lake wala dini yake.

Maendeleo ya nchi hayaletwi na kiongozi, maendeleo huletwa na watendaji, ambao ni raia. Sasa ukiwa kiongozi kwa mfano kama alivyokuwa nyerere unategemea maendeleo hapo? Si alikuwa na Mtei (Mchaga). Mbona hakumsikiliza?

Tatizo la wachaga ni wabinafsi sana, akiwa madarakani na akiamua kung'atuka yatakuwa kama ya cdm, lazima ahakikishe anamrithisha wa karibu nae, mfano hai; Mtei to Mbowe.
 
Back
Top Bottom