Huu ni baadhi tu ya ufisadi mkubwa ndani ya CHADEMA; ni kuhusu mamilioni ya Sabodo

hii hoja tunaweza kuipuuza lakini tukumbuke ccm wako makini sana kwenye kumaki mambo kama haya na kuyatumia vizuri wakati wa kampeni....ni vyema chadema ikawa makini sana hasa wakati huu ambapo wananchi wanaamini ndio kimbilio lao.!!
 
mtoa hoja bado haulekei kudhibitisha tuhuma zako ndio maana wanajamvi tunaziona kama jungu , kwani unaposema ajitokeze kiongozi yeyote wa chadema akinzane na hizo tuhuma zako ili upate kuweka data kamili kwa maana hiyo hizo data zote za matumizi ya fedha ya CHADEMA sio za kweli ila unataka kupata taarifa kamili ya matumizi ya hizo fedha kutoka kwa uongozi wa chadema.

pili unapodai kuwa hizo fedha za mzee Sabodo shs milioni 300 zimetumika kununua nyumba dubai na kuifanyia ukarabati, vile vile hizo hizo fedha zina tumika kukarabati billicanas hivi unajua bei ya soko kwa nyumba hapa dar es salaam mfano magomeni hiyo milioni 300 haitoshi kununua nyumba kwenye eneo hilo sembuse undhaibuni tena dubai , sasa hiyo nyumba itakuwa imenunuliwa miliono 100 au? kweli dubai? mi naona mleta tuhuma bado hujajipanga ,kama kweli ni mgeni kwenye hili jamvi tena kwa jina la mwanahalisi mi napata shida kuchambua uhalisi wa tuhuma zako. TAFADHALI JIPANGE!
 
Hivi mil 300 unaweza kufanya mambo yote aliyoyataja huyu jamaa? Kununua nyumba dubai ni sh ngapi? Kujenga nyumba kunduchi sh ngapi? Kufanya ukarabati wa billz sh ngapi? Mtoa mada akajipange upyaaaa!!

MUWE WEPESI WA KUELEWA MNATAKA MCHAMBULIWE KILA KITU HALAFU MFANYE NINI 300M NI MFANA WA PESA TOKA MAFUNGU MBALIMBALI ZINAZOINGIA KWENYE ACC. Mbalimbali za cdm sasasa hapa kama kweli wewe ni mkereketwa wa CDM fuatilia kama mipango iliyotangazwa kufanyika kwa ujenzi na maendeleo ya Chama imefikia wapi! Je, VISIMA VYA SABODO NI MBUNGE GANI (jimbo) ama Diwani yupi (KATA) anayechimba kisima!? Jitahidi kuendelea kuwa mpumbavu na sio MJINGA.
 
Mimi ni kiongozi wa Chadema na wewe uliepost hii thread bora ukae chini utafakari b4 hujaandika ujinga wako humu, do you think Mbowe na Slaa ndio CHADEMA???? Wao ni viongozi na hawana hiyo njaa unayotaka kupotosha nayo watu, they stand for right and always they'll be there 4 TANZANIAN's people..... Bills mbona imekarabatiwa hata hiyo hela ya Sabodo haijatoka. Nadhani unjejiweka wazi what do you want from those 2 leaders....... na uache propaganda.....

eeeeh??haya nayo maneno ya kiongozi?umenichekesha...kazi kweli kweliu
 
Mimi ni kiongozi wa Chadema na wewe uliepost hii thread bora ukae chini utafakari b4 hujaandika ujinga wako humu, do you think Mbowe na Slaa ndio CHADEMA???? Wao ni viongozi na hawana hiyo njaa unayotaka kupotosha nayo watu, they stand for right and always they'll be there 4 TANZANIAN's people..... Bills mbona imekarabatiwa hata hiyo hela ya Sabodo haijatoka. Nadhani unjejiweka wazi what do you want from those 2 leaders....... na uache propaganda.....
Mkuu labda lile jengo la RITA yeye anadhani la bills. Si unaona kwenye sredi yake anasema Ukarabati unaendelea twende tukaone na kupruvu?
 
Na hii ya kuchukua gari shangingi wakati mbowe alikataa?

Swala la slaa kukaa abla apartments? Ingawa bei iliyotajwa ni kubwa kidogo I think its less than 250,000 kwa siku. Kuna picha ililetwa ya Slaa na mmiliki wa abla apartments wanakunywa kahawa mnakumbuka?

Hivyo visima mtajenga lini?

Jibuni hoja kwa hoja
Suala la kukaa alba apartments ni la binafsi labda wewe uje na invoice ya alba apartment inayokwenda cdm kudai malipo ya kodi ndo tutajibu.
 
mbona kwenye misaada ya sabodo hapo hamdai soure? Na kama hiyo mnaikubali mbona hamjibii nukta hiyo hiyo tulioko nje tupate faida?
Usiwe kama mwehu. Kwa akili yako sh 700Milioni unaweza kununua nyumba Dubai na kujenga nyumba kunduchi na kukarabati Billicanas na hela ikatosha?
Kuhusu visima, ni lini na wapi ambapo Sabodo alisema pesa anazotoa lazima zianze kuchimba visima on the spot? Na kama hakukuwa na time frame ya kuchimba na kuanza kutumika kwa hivyo visima, unawashwa nini kuuliza sasa? Mbona flyovers ulizoahidiwa Dar es salaam huziulizii?
Kwa hiyo, kama unavyovumilia kusubiri flyovers na kwa visima pia hivyo hivyo unapaswa kusubiri na kuwa mvumilivu
 
Mtoa hana jipya mill 300 sio pesa za kufanya mambo yote hayo, na zaidi ya hapo Billcanasi inafanyiwa ukarabati mara kwa mara kama una kumbukumbu(mtoa maada). Pili kwa exchange rate ya leo, assuming that pesa yote inatumika kununua nyumba Dubai haitoshi kwani ni USD 187520.
Kiffupi ni kwamba jaribu ku-breakdown hiyo mill 300 kivingine hapa umechemka.
 
Tunathibitishaje kama ni kweli au la? Eti twende billicanas tukaangalie ujenzi, kweli? Billicanas yenyewe inauwezo wa kugenerate zaidi ya millioni 100 kwa mwezi. Please come up with something vivid sio unatunga stori kama za Shigongo. Kila mtu anaweza kuamka na kuandika kama ulichoandika!

Mi nimeshangaa kuifanya bills mufilisi mpaka ikarabatiwe na pesa kiduchu hivyo. Mhe. Mbowe katumia pesa binafsi kibao kuifanya Chadema iwe imara. Hata ndugu zake hawakuwa wanapenda Mbowe awe anajihusisha na siasa zinazoweza kumfilisi.
 
MUWE WEPESI WA KUELEWA MNATAKA MCHAMBULIWE KILA KITU HALAFU MFANYE NINI 300M NI MFANA WA PESA TOKA MAFUNGU MBALIMBALI ZINAZOINGIA KWENYE ACC. Mbalimbali za cdm sasasa hapa kama kweli wewe ni mkereketwa wa CDM fuatilia kama mipango iliyotangazwa kufanyika kwa ujenzi na maendeleo ya Chama imefikia wapi! Je, VISIMA VYA SABODO NI MBUNGE GANI (jimbo) ama Diwani yupi (KATA) anayechimba kisima!? Jitahidi kuendelea kuwa mpumbavu na sio MJINGA.
Una makengeza au unajipa ujinga na upumbavu mwenyewe? Huwezi kuipitia tena sredi kuelewa ni kiasi gani kinalalamikiwa? Mleta sredi anakuja na figure tofauti tofauti ambazo jumla yake ni sh Mil 700. Kwa akili yako unaweza kununua nyumba Dubai kwa Mil 700? Jibu kwanza hilo.....
 
wanacdm bwana!hata kujenga hoja tatizo,yaan nyie mnapewa kusifiwa tu,kazi ipo,watu kama MOLEMO wanaomba mod afute thread,loh cdm mnatia aibu sana,hapa mumeshikwa kwenye nyonga,msiwe wepes wa kukurupuka though nina hakka dr slaa atatoa ufafanuzi maana bila huyo no cdm,nyie mumekaa mkao wa kulembua kama mpaka wanja,
 
Hivi mil 300 unaweza kufanya mambo yote aliyoyataja huyu jamaa? Kununua nyumba dubai ni sh ngapi? Kujenga nyumba kunduchi sh ngapi? Kufanya ukarabati wa billz sh ngapi? Mtoa mada akajipange upyaaaa!!

Yaani!
Nimesoma nikacheka kwa masikitiko.Umasikini wa Watanzania umekithiri hadi vichwani.
Huyu aliyeandika inaonekana hajawahi kushika hata milioni moja ya kitanzania.Angekuwa amewahi kuona wachilia mbali kushika kamilioni, angejitahidi kusuka uongo wake vingine.
1. Milioni 300 kufanya hayo yote ni ndoto
2. Hizo milioni 300, ina maana wakigawana - Freeman, Slaa na Josephine, shughuli za chama hazijapata hata senti moja?
3. Anazungumzia kununua nyumba Dubai na kuikarabati - anaijua Dubai au anaiskia redioni?
 
Jamaa umetoa hoja,sema tatizo kuna wa2 hawaoni,.haiwezekani m2 anayepambana na ufisadi kukifanya chama kumlipia senior mchumba ulinzi
 
Umejiunga leo na umeaanza na pumba, Hebu weka ushahidi wako hapa sio unatoa povu kama yule Fisadi Mkapa anayesubiria ukombozi wa kweli na kupelekwa jela.

Mwanahalis;

Join Date : 7th March 2012
Posts : 3
Rep Power : 0Likes Received: 0
Likes Given: 30

Kazi ipo!!!!
 
wacha kujichanganya nikuwekee ushahidi wa visima au gari kivipi..!!!! mmetumwa kututoa kwenye topic ya mkapa..hatulali tunaye leo..mpaka atarudia tena ile doz yake ya presha..

Mkuu nitumwe na nani mimi? Wenyewe mnamalizana huko tukiuliza mnakimbilia kwamba tumetumwa. Angalia unavyotoka mapovu. Nakuuliza mimi niweke ushahidi wa visima au gari wewe unasema uniwekee ushahidi! Wapi na wapi tuliza mpira takaseni nyumba yenu. Mimi sizijui akaunti za CDM na wala sijihusishi na CDM niliacha kujihususha na vyama katikati ya miaka ya 90.
 
Kwa akili za kawaida tu sh millioni 200 haziwezi kufanya kazi zote hizo kununua nyumba dubai, kuikarabati, kukarabati Bilicanas, Kumjengea Nyumba Slaa Kunduchi... Nyumba Nzuri Sinza tu hata million 200 hupati.

Siku nyingine ukitaka kuwadanganya watu wazima angalau ongelea kitu kinachokaribiana na ukweli.
 
Jamaa umetoa hoja,sema tatizo kuna wa2 hawaoni,.haiwezekani m2 anayepambana na ufisadi kukifanya chama kumlipia senior mchumba ulinzi
Hoja au majungu? Binafsi namfahamu Dr Slaa vizuri sana kwa taarifa yako huyu mzee angetaka afanye ufisadi angekuwa na pepo yake! Huyu amekuwa keki toka akiwa Mbunge na CCM wanamjua vizuri kuwa si mchafu labda tukubaliane kama mtu makini anaweza kuanza kuvuta sigara akiwa na zaidi ya miaka 55! Chadema ni taasisi inayoendeshwa kwa budget kama taasisi zingine.budget inaandaliwa toka ngazi za chini hivyo mtoa mada atuambie chama kinaendeshwaje kama pesa zote 3bilion zimefanya hayo aliyotaja? Unazungumzia akaunti ya wadhamini kuchotwa fedha za uchaguzi wa Arumeru sasa hapo issue ni nini? Budget ya uchaguzi imepangwa na Mbowe,Slaa tu? Kama budget inapangwa na watu wawili chama kizima hata huyo Mwanahalis(Tuntemeke) anafanya nini kwenye chama chenye up.uuzi wa level hii?
 
Kumbe CHADEMA inalipa mishahara ya walinzi wa kanisa!
Josephine
njoo ujibu hizi tuhuma kabla hatuja-conclude!
 
Back
Top Bottom