Huu ndiyo Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Articles of Union)

Mimi Mushi nimebadilishana na Shirima shamba langu la heka saba kwa mbuzi wa kisasa

Mushi .........
Shirima ............
 
Duh napita ngoja nizipitie vifungu kny katiba vilivyoorodhoshwa vyote then nije na comment ya uhakika
 
hiyo document ingekuwa scanned na kuwekwa hapa ningeamini.......kwa sasa bado nina mashaka
 
Najua mtachukia koment yangu, lakini ukweli ni kwamba mtoa mada hajaweka mkataba kama taito ya thread yake inavyosema. Alichoweka ni quote ya kitabu ambacho kila mtu anaweza kukisoma pale library.. Tunachotaki ni kopi ya mkataba uliosainiwa na wahusika. Either uskaniwe na kuwekwa hapa au usambazwe by other means ili watu waujue. Na hcho ndicho Slaa aliwahi kuomba. Nadhani hik ktabu kinajulikana sana na wanazuoni wamekisoma sana.

Tunataka mkataba as a document sio page ya kitabu.

Siku itakapopatikana nakala halisi ya mkataba wa muungano litakuwa jambo la mbolea sana.

Hatahivyo kwa kuanzia si mbaya sana kwa hiki kilichopatikana.
 
Aliyeleta hio ametoa kwenye kitabu cha aboud jumbe mwinyi 'the partnership - thirty turbulent years of the union'

kisheria hio sio document yenyewe kwa kuwa:-

1. Hau jatiwa saini na spika wala katibu wa bunge.

2. Haujatiwa saini na yeyote mwenye mamlaka anayewakilisha jamhuri ya tanganyika na jamhuri ya zanzibar

wanasheria wataongezea

Hatuhitaji saini ya yeyote hapa , kinachotakiwa ni kuufahamu mkataba wa muungano hata kama ni draft. Vinginevyo ungesema haya maandishi sio yenyewe.
 
Hivi ansard za Bunge la Tanganyika na zile za Baraza la Mapinduzi la Zanziba la tarehe 25/4/1964 zinaonyesha kupitisha hoja hiyo?
 
Mbona Mkataba wangu ninotumia kuwapangashia fremu za duka wapangaji wangu una vipengere vingi na una kurasa kadhaa bkuliko huu wa kuunganisha nchi mbili!?

Bado nasita kuamini kama kweli Jamhuri mbili zinaweza kufunga mkataba kwa style ya Affidavit.
 
Naona kati ya watu muhimu waliohusika na nyaraka za muungano na ambao bado wako hai ni Pius Msekwa. Huyu "akiwahiwa" anaweza kutueleza mengi sana kuhusiana na muungano wa Nyerere na Karume. Wajameni waandishi makini na watafiti tusaidieni hilo ili kuweka mambo sawa.
 
Huu muungano ni kama wa kijana muhuni aliyeamua kuishi (sio kuoa) na changudoa aliyemzoea. Wanachojaribu kufanya wanaoutetea huu muungano ni kulazimisha tuiite ndoa halali. Upuuzi mtupu!!!!

Ha ha ha ha ha ha! Mkuu hebu fafanua kidogo. Kwa muktadha huu kijana ni nani na changudoa ni yupi?
 
mimi si mwanasheria
MAPUNGUFU NILIYOYAONA KWAHARAKA HARAKA ndani ya mkataba wenyewe

1.haukuainisha tarehe ya kuaza kufanya kazi
2.hauna masharti ya kuvunjika kwake, nini kikitokea mkataba utakua umevunjika
3.nani alileutia sahihi kwa pande zote mbili(tanganyika na zanzibar) ziko wapi hizo sahihi zao
4. nani alikua shahidi/mashahidi wa mkataba
5.''Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri'':-
litawezekana vipi jambo hili wakati kutakuwa na katiba ya zanzibar na ya muungano tu bila ya katiba ya tanganyika?
6.makamo wa pili haikuainishwa atatoka wap na kuchaguliwa na nani
7.a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni jambo la muungano na serikali ya tanganyika ikatiwa humo humo yote(ilifanywa kwa bahati mbaya au makusudi?)


KASORO KATIKA UTEKELEZAJI
1. HAKUNA kumbukumbu kuwa kuna kikao cha baraza la mapinduzi zanzibar kilichoamu au kuridhia muungano(SIKWAMBII WANANCHI ambao leo wanaambiwa wasijadili kuvuunja muungano)
2. makamo wa pili wa raisi hakuwepo hata siku moja
3.mamlaka ya tanganyika ilifutwa kinyume na mkataba
4.mwanasheria wa zanzibar hakuhusika

na mengine mengi yaliyozuka baadaee kama kuongezwa onyo mambo ya muungano . bunge halina mamlaka kwa mambo yasiyo ya muungano ya zanzibar lakini linaweza kulichukuwa jambo lisilo la muungano la zanzibar na kulifanya la muungano(maana yake nini?)

aliye wasilisha mada nampa hongera kwa jitihada yake lakini kazi bado ipo .....TUNATAKA MKATABA WA MUUNGANO sio mswaada wa sheria uliopitishwa na bunge la tanganyika huu.

wazanzibar kwa upande wetu tumeshasema hatutaki muungano wa kitapeli kila nchi ichukuwe chake tusitafute uhasama bure kwa upuuzi huu

 
mkuu nashukuru,,,,,lakini sijaona sahii ya jk nyerere na abed karume,,hivo inaishia kuwa chapisho
 
huwa najiuliza sana but nakosa majibu....najua kati ya watu walioutetea huu Muungano kwan nguvu zote basi ni Baba wa Taifa Mwl Nyerere licha ya kuwa na mapungufu kibao....ilifika wakati alikuwa hata akitoa vitisho

Hivi kwa nini mzee wetu alifikia hatua hiyo au kuna something that is hidden?...naogopa laana mwenzenu
 
mkuu nashukuru,,,,,lakini sijaona sahii ya jk nyerere na abed karume,,hivo inaishia kuwa chapisho

plz usi-quote post ndefu kama hii...ni usumbufu kwa wasomaji wengine...MOD kama vp ziedit replay zenye quote ya style hii kupunguza usumbufu
 
Hivi ansard za Bunge la Tanganyika na zile za Baraza la Mapinduzi la Zanziba la tarehe 25/4/1964 zinaonyesha kupitisha hoja hiyo?

Wakuu!

Nadhani hakukuwa na baraza la wawakilishi kipindi cha muungano, kama sikosei, aboud jumbe ndo alierudisha baraza la wawakilishi
 
mkuu nashukuru,,,,,lakini sijaona sahii ya jk nyerere na abed karume,,hivo inaishia kuwa chapisho
Huu ndio utoto tusioutaka hapa JF, ni kwa nini uquote uzi mzima wakati reply yako ni mstari mmoja tu. acha ushamba kumbuka kuna watu wanatumia simu unawapa tabu isiyokuwa na sababu yoyote.
 
Huu muungano inaonekana ulikuwa wa chap chap, ila haukufuata kanuni za chap. Hivi nani aliyeamua Tanganyika isiwe na serikali? Nasiki mwanasheria wa Zanzibari alipewa likizo wakati wa kuandaa haya mambo, ni kweli?
 
Tatizo sio mkataba wenyewe, tatizo ni kwamba mkataba haukufwatwa tangu mwanzo wake. ulichokiweka hapa ni mkataba ambao ulijadiliwa na bunge la Tanganyika. mkataba ulitaka pia bunge la Zanziba liujadili na kuupitisha ndipo usainiwe kuwa sheria rasmi ya kuanzisha Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar. kwa upande wa Zanzibar hawakupata fursa hiyo kwani hata bunge halikuwepo. na pia hakuna ushahidi wowote kwamba bunge la Zanzibar liliwahi kukaa na kupitisha mkataba huo, hivyo hata kama mkataba ni mzuri kiasi gani - unakosa uhalali wa kisheria.

Duh! Kumbe wazenji hawakuwahi kujadili? Basi hakuna muungano ila kuna uchumba wa muungano. Ukiishi na binti/mwanamke kwa muda zaidi ya miezi mitatu hata kama hujaenda kujitambulisha kwa wazazi wake na wakakaa kujadili kama wakupe mwana wao au la automatically ni mkeo kwa sheria za Tz. Nadhani waliitumia hii na mpaka leo tunaimba muungano wakati taratibu hazikufuatwa na kukamilishwa. Samahani kwa kutumia mfano wa mahusiano ya mapenzi.
 
Huu muungano ni kama wa kijana muhuni aliyeamua kuishi (sio kuoa) na changudoa aliyemzoea. Wanachojaribu kufanya wanaoutetea huu muungano ni kulazimisha tuiite ndoa halali. Upuuzi mtupu!!!!

Nakupa mia mkuu!
 
Tatizo sio mkataba wenyewe, tatizo ni kwamba mkataba haukufwatwa tangu mwanzo wake. ulichokiweka hapa ni mkataba ambao ulijadiliwa na bunge la Tanganyika. mkataba ulitaka pia bunge la Zanziba liujadili na kuupitisha ndipo usainiwe kuwa sheria rasmi ya kuanzisha Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar. kwa upande wa Zanzibar hawakupata fursa hiyo kwani hata bunge halikuwepo. na pia hakuna ushahidi wowote kwamba bunge la Zanzibar liliwahi kukaa na kupitisha mkataba huo, hivyo hata kama mkataba ni mzuri kiasi gani - unakosa uhalali wa kisheria.
Zanzibar hawakuwa na bunge bali baraza la mapinduzi kwa kuwa bunge lilivunjwa na mapinduzi ya Januari 12,1964.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom