Huu ndiyo Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Articles of Union)

Mimi naona ubabaishaji zaidi kuliko hicho kinachoitwa muungano, sasa ikiwa Bunge lilikuwa la Tanganyika sasa hao Wazenji walikuwepo wapi au ndio waliridhia wakawachia kila kitu Watanganyika ? Duhhhh! hii kazi ipo wacha Wazenji waukatae huu muungano.
 
Mi sijaelewa kitu hapo.Mkataba gani huu? huyu mleta uzi amequote kwenye kitabu au ndiyo mkataba wenyewe maana hakuna hata sahihi za walioingia mkataba halafu anatuambia ndiyo mkataba wenyewe.Je ni kweli uliandikwa kwa kiswahili?maana wabongo tuna kasumba ingawa vitu ni vyetu wenyewe lakini tunaandika kwa lugha za kigeni.Huu siyo mkataba bali amechukua maneno kutoka katika kitabu na kuita ndiyo mkataba.
 
Wajemeni mbona hayo mambo11 mi siyaoni,,,kah!!! mweee!



Hayo hapo yameorodheshwa kuanzia a.....k mkuu wangu, mkataba wenyewe umekondeana sana ndiyo maana wakuu hawataki tuuone.
Makubaliano yamefikiwa tarehe 22, bunge la Tanganyika likapitisha tarehe 25 na tarehe 26 ndiyo muungano wenyewe !! Yote hayo chini ya wiki moja!!

Ni kama mkataba wa kundesha shamba la bangi kwa ubia, sorry nina hasira.
 
Mi sijaelewa kitu hapo.Mkataba gani huu? huyu mleta uzi amequote kwenye kitabu au ndiyo mkataba wenyewe maana hakuna hata sahihi za walioingia mkataba halafu anatuambia ndiyo mkataba wenyewe.Je ni kweli uliandikwa kwa kiswahili?maana wabongo tuna kasumba ingawa vitu ni vyetu wenyewe lakini tunaandika kwa lugha za kigeni.Huu siyo mkataba bali amechukua maneno kutoka katika kitabu na kuita ndiyo mkataba.

Hapo kwenye bold ulitaka itumike lugha gani ikiwa Karume Sir. hakuwa na shule akaishia kuwa kuli bandalini?
 
Viongozi wetu walianza zamani sana kututenda, na hii ni kwa kuwa tuna uvumilivu wa kijinga! Yana mwisho.
 
Najua mtachukia koment yangu, lakini ukweli ni kwamba mtoa mada hajaweka mkataba kama taito ya thread yake inavyosema. Alichoweka ni quote ya kitabu ambacho kila mtu anaweza kukisoma pale library.. Tunachotaki ni kopi ya mkataba uliosainiwa na wahusika. Either uskaniwe na kuwekwa hapa au usambazwe by other means ili watu waujue. Na hcho ndicho Slaa aliwahi kuomba. Nadhani hik ktabu kinajulikana sana na wanazuoni wamekisoma sana.

Tunataka mkataba as a document sio page ya kitabu.
 
Bunge lililopitisha mkataba tar 25/4, lilikuwa la Tanganyika peke yao au lilihusisha wazanzibari? Sijaona sehemu spika wa Zenji akitajwa.

Moja kati ya mapungufu ya huu muungano
 
Tatizo sio mkataba wenyewe, tatizo ni kwamba mkataba haukufwatwa tangu mwanzo wake. ulichokiweka hapa ni mkataba ambao ulijadiliwa na bunge la Tanganyika. mkataba ulitaka pia bunge la Zanziba liujadili na kuupitisha ndipo usainiwe kuwa sheria rasmi ya kuanzisha Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar. kwa upande wa Zanzibar hawakupata fursa hiyo kwani hata bunge halikuwepo. na pia hakuna ushahidi wowote kwamba bunge la Zanzibar liliwahi kukaa na kupitisha mkataba huo, hivyo hata kama mkataba ni mzuri kiasi gani - unakosa uhalali wa kisheria.

mh! Kazi ipo na mapungufu yanaonekana ni mengi sana!
 
Kwa tuliobahatika kusoma "LAW OF CONTRACT" huu si mkataba, labda tuite "MEMORANDUM OF UNDERSTANDING". Halafu katika kipengele cha ( iv) mbona mambo ya muungano yameongezeka? na kipengele cha iii(b) makamu wawili wa raisi hiyo haipo sikuhizi.

Je tunataka kuaminishwa kwamba huu mkataba ulifanyiwa marekebisho? pande zote mbili zilikaa kufanya marekebisho?. Narudia tena kusema, huu si mkataba.
 
Ni ukurasa wa kitabu lakini ukweli ni kuwa utaongeza mjadala na pia utawaamsha waliokuwa hawajui kuwepo kwa kitabu hiki. haya yote yatachagiza kupata the real doc signed-tusimbeze mtoa mada kwa mchango wake mzuri- big up subirijibu
 
Duh, kama kweli huu ndo mkataba wa muungano, basi mapungufu ni mengi sana. only 2 page limit? kitu muhimu kama hiki ndio maana unaonekana kuwa na matege sana. mimi naona nasi tuanze kudai Tanganyika yetu,tuwe na serikali tatu.
 
Aisee too simple to be true. Tanganyika was sacrificed cheaply like what chief Mangungo did to his land.

Tuanze upya. Ndo maana hawataki muungano ujadiliwe, sio wa kurekebisha huu ni wa kuunda upya kabisa.
 
Huu muungano ni kama wa kijana muhuni aliyeamua kuishi (sio kuoa) na changudoa aliyemzoea. Wanachojaribu kufanya wanaoutetea huu muungano ni kulazimisha tuiite ndoa halali. Upuuzi mtupu!!!!
 
Hata siamini, yaani hutu tumaneno tuchache ndio tunawapa Wapemba nguvu kuubwa ya kutumia umeme wetu kwa mkopo muda woote na baada ya fununu za kupatikana mafuta huko kwao leo wanatukana tumaneno tule tule?!!
 
Back
Top Bottom