Huu ndio Usupa staa wenyewe.

Nadhani siku hizi ndio fashen kuonyesha hizo za ndani, sisi tupandao daladala ndio huona mengi zaidi-unaweza kuona lundo la shanga utadhani mtu anaenda kuuza!

Mmoja hiyo mishanga ilimkatikia katika daladala karibu na kufika kituo cha Mwenge ilikuwa aibu! Hayaokoteki kwa kuwa yalisambaa kwenye floor ya bus zima!

Kwa mtazamo wangu ni ULIMBUKENI; mbona kuna ma star wanavaa kistaarabu tuu! Au kuonesha VITUZ ni moja ya kuukamilisha huo u star?
 
Back
Top Bottom