Huu ndio uongo wa Padri Mapunda kwa CCM na mapenzi yake Chadema

Huyo padre ndo wale wale wanaohubiria waumini viwango wa sadaka wanasotakiwa kutoa. Huyo itabidi CAG amfanyie auditing ili kujua utajiri wake manake analala anaota utajiri.
typical vapour! pity you!
 
Hivi kwa nini kila anaeikosoa CCM ni Chadema?

Wengine hata ofisi za kata za chadema hatuzijui lakini hatuwezi kuacha kukosoa madudu yanayofanywa na CCM, CCM imeoza full stop.


HAta Sumaye in CDM loH!
 
Padri yuko sahihi we unadhani ridhiwani ng mama yake wamepitwa bila kupingwa kwa sababu hakuna watu ccm wa kugnmbea nao? Huwezi kulinganisha siasa za ccm na chadema juu ya uteuzi wa viti maalum bungeni. Katika nchi nyingi za kiafrika wasomi wengi ni waoga kujihusisha na sias za upinzani wengi wanakimbilia kugombea vyeo ili watajirike haraka. hili linaonekana kirahisi tu kwenye vyama hivi, wanawake wasomi ni wachache upinzani na hao wacache wanatokana na ushawishi wao hao ndugu zao sasa utategemea nini kwenye uteuzi. hapa una darasa la saba sio na hapa una mwenye digrii lakini ni ndugu yako na huko bungeni ni hoja nzito zinajadiliwa na chama ni lazima kipambane kujibu hoja ili wananchi wasije wakakidharau kwa kukosa hoja unafanyaje? ccm leo hii wakisema wamekosa watu wa kugombea vyeo ndo maana wameruhusu wengine wapite bila kupingwa ni uongo wa juani, ni undugunisation tu hapo hakuna kitu.
 
Kinachosikitisha ni kwamba hali ya hewa ikichafuka kutokana na tabaka fulani kupendelea wateule wao wachache,viongozi hao hao walio sababisha hali hiyo tete huwa wa kwanza kutaka msaada toka kwqa viongozi wa kiroho kuwaweka sawa waumini.

Ni hatari kwa taifa dhaifu lililo kosa uadilifu kuthubutu kumkemea kiongozi wa kidini kwa kitendo cha kukosoa na kusimamia maadili ya jamii husika.Watasema sana lakini hawatashinda,siku ya kufa nyani miti yote huteleza.Rudi kajipange upya,jamii inapokosea lazima ielezwe bayana



AKIONGOZA misa katika Kanisa Katoliki la Manzese jijini Dar es Salaam, Jumapili iliyopita, Padri Baptiste Mapunda “alikemea tabia ya kupeana uongozi ndani ya familia moja” akidai itakwamisha utendaji wenye tija na maendeleo.

Mapunda ambaye ameondokea kuwa ni “padri mwanasiasa wa kambi ya upinzani nchini”, alisema hali hiyo inaongeza pengo kati ya matajiri na masikini, kisha akawashutumu viongozi wa kisiasa akidai wameua Azimio la Arusha alilodai lilianzishwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na kuligeuza kuwa “azimio la wala rushwa na ufisadi”.

Alimfananisha Rais huyo wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mtume Musa akisema alitumia hekima na busara, kuwaondoa Watanzania katika ukoloni bila ya kutumia silaha, na kwamba wakati wote wa utawala wake hapakuwepo migomo ya walimu, madaktari au kuuawa kwa mwandishi wa habari.

“Jambo la msingi tuhakikishe rais anapunguziwa madaraka na matumizi ya vyombo vya dola yasiwepo katika siasa, viongozi wengi hawakuchaguliwa kwa haki na ndiyo maana taifa limekuwa na majanga makubwa”, alisema kama alivyonukuliwa na gazeti moja la kila siku nchini, Jumatatu wiki hii.

Nimewahi kukorofishana hadharani na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Meja Jenerali Saidi Kalembo nikimtetea Padri Mapunda alipopigwa marufuku asiongoze ibada yoyote mkoani humo mwaka 2003, zuio alilopewa kwa sababu alikuwa akihubiri siasa za uchochezi.

Nilifanya hivyo kwa imani kwamba ilikuwa bahati mbaya na angejirekebisha kama kiongozi wa kiroho, jambo ambalo ameshindwa kulifanya kwa miaka tisa sasa tokea wakati huo.

Kila Mtanzania mwenye akili timamu anafahamu kuwa Padri Mapunda “alikemea tabia ya kupeana uongozi ndani ya familia moja” baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kupitisha majina ya wanafamilia yake kugombea nafasi za kisiasa katika chama hicho.

Walioteuliwa kugombea ujumbe wa NEC kwa wilaya za Lindi Mjini na Bagamoyo, mkoa wa Pwani na kumwibua padri huyo kusema hayo ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na mtoto wao, Ridhiwani Kikwete.

Wote pia hawakupata wapinzani katika kinyang’anyiro hicho na kisha wakashinda siku za uchaguzi huo, lakini mwanafamilia mwingine ambaye ni mdogo wa Rais huyo, Mohammed Kikwete aliyeteuliwa kugombea uenyekiti wa chama hicho wilayani Bagamoyo alianguka.

Huo ndio wivu mbaya kabisa alionao kiongozi huyo wa kiroho unaokwenda sambamba na chuki, fitina za malengo ya kisiasa, majungu na uchonganishi unaolenga kuwapandikizia hasira za uasi wananchi ili kukidhi matakwa yake mwenyewe na wapambe wake.

Anafanya kila anachoweza ili wafuasi wake wa kiroho wamfuate pia katika itikadi zake za kisiasa na chuki zake kwa Rais Jakaya Kikwete, familia yake, CCM na Serikali ya Awamu ya Nne.

Sitaki niaminishwe kwa namna yoyote kuwa mahubiri yake hayo ni agizo la Kanisa Katoliki kutoka popote, hivyo nitabaki naamini katika moyo wangu wote kwamba hayo ni matakwa yake mwenyewe ya kisiasa na siyo ya kiroho na hata vinginevyo.

Ni ajabu kwa padri kusimama katika altare kanisani na kusema uongo huku akiwa ameshika Biblia Takatifu, lakini pia ni dhambi zaidi kuhubiri uzushi unaolenga kuwachonganisha watu ili wafarakane kwa namna yoyote.

Harakati za Mama Salma Kikwete, Ridhiwani Kikwete na Mohammed Kikwete kugombea nafasi hizo za kisiasa katika CCM hazikuanzia mikononi mwa Rais Kikwete wala ndani ya NEC isipokuwa wilayani wanakotoka.

Zilianzia Lindi Mjini na Bagamoyo walikoomba kugombea nafasi hizo baada ya kujipima wenyewe, kisha wakajiridhisha kuwa wanakidhi masharti ya Ibara ya 14(1) – (3) ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 1977 Toleo la 2010 inayosema ifuatavyo:

“Mwanachama yeyote (wa CCM) atakuwa na haki ya kushiriki katika shughuli zote za CCM kwa kufuata utaratibu uliowekwa, haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya CCM pale ambapo anahusika, (na pia) haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa kiongozi wa CCM na ya kuchagua viongozi wake kwa mujibu wa katiba na taratibu…”.

Walifanya hivyo kwa kuchukua, kujaza na kurejesha fomu na kuambatanisha vielelezo vyote walivyotakiwa kuviwasilisha katika ngazi zote za mchakato huo mrefu ulioanzia wilayani, mkoani hadi kwenye vikao vya kitaifa ambako uteuzi wao ulifanywa kwa kuzingatia Katiba ya CCM na siyo kwa matakwa ya Kikwete au ya familia yao.

Wote wanakubaliana na masharti yote ya Ibara ya 5(1) – (19), na pia wanakidhi matakwa ya Ibara ya 7, 8(1) – (7), 12(1) – (2) na 15(1) – (9) za katiba ya chama chao hicho na masharti yote yaliyotajwa na Ibara ya 2(1) – (2), 3(1) – (2) na 5(1) – (2)(a) – (d) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa.

Kabla ya kuteuliwa na NEC kugombea nafasi hizo, hatua ambayo pia haikuwa ya mwisho ya kuzipata nyadhifa hizo ila hadi wawili kati yao waliposhinda katika uchaguzi mkuu wa ngazi zinazohusika, kila mmoja alipaswa kujitetea mwenyewe kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wilayani kwake ili kuomba wamchague, hivyo ni uzushi na uongo mkubwa kudai eti kuwa kuna tabia ya “kupeana uongozi ndani ya familia moja” katika CCM.

Hata Rais Kikwete naye akitaka kugombea nafasi yoyote katika chama hicho hapewi tu wadhifa huo na familia yake iwe na mkewe, watoto wake, wadogo zake, wajomba zake, shangazi zake, binamu zake, mama zake, baba zake wala vinginevyo.

Itabidi atimize masharti yote ya Ibara ya 5(1) – (19), 7, 8(1) – (7), 12(1) – (2) na 15(1) – (9) za Katiba ya CCM na matakwa yote yanayotajwa na Ibara ya 2(1) – (2), 3(1) – (2) na 5(1) – (2)(a) – (d) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtu anapokurupuka na kudanganya utadhani ni mganga wa kienyeji kama alivyofanya Padri Mapunda anakuwa moja kwa moja ni mzandiki kinywani na amesheheni wivu mwili mzima, chuki binafsi, uchonganishi na uchochezi kwa misingi ya kisiasa.

Ndiyo maana anadanganya pia kwamba eti viongozi wa serikali ya CCM waliua Azimio la Arusha na kuligeuza kuwa “azimio la wala rushwa na ufisadi” huku akijua anaongea uongo.

Kama ambavyo lilianzishwa mwaka 1967 na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya vyama vya Afro – Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar na Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanzania Bara, wakati huo vikiwa ni vyama pekee vya siasa kila upande kabla ya kuungana na kuwa CCM ilipofika mwaka 1977, azimio hilo pia lilifanyiwa marekiebisho mapya ya msingi mwaka 1992 kwa njia zote halali.

Sababu kubwa zaidi iliyosababisha kufanywa kwa marekebisho hayo ni Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, jambo ambalo linaelezwa katika Ibara ya 3(1) – (2) ya Katiba ya nchi hii.

Padri Mapunda mwenyewe anajua kwamba Azimio la Arusha ni imani ya kisiasa ya TANU na ASP na baadaye CCM, hivyo isingewezekana liendelee kuwepo hata baada ya nchi kuwa ya vyama vingi kwani kila chama kinakuja na imani, itikadi na sera zake.

Ndiyo maana mwaka 1992, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokutana Zanzibar iliona haliwezi tena kuendelea, badala yake likabaki kuwa ni dhana inayotajwa katika Ibara ya 3(1) ya Katiba ya nchi inayosema kwamba “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”.

Kana kwamba haitoshi, padri huyohuyo na Watanzania wengine wanafahamu namna gani vyama mbalimbali vya siasa vinavyopingana, vile ambavyo kuna vingine havitaki Tanzania iendelee kuitwa “nchi ya kijamaa” kwa sababu hiyo ni itikadi ya kisiasa ya CCM.

Vipo vinavyotaka neno hilo liondolewe kwenye Katiba, hivyo endapo lingekuwepo hadi sasa ingekuwa fujo, vurugu na kutumika kuwa kichaka cha baadhi ya watu kuitukana CCM, serikali na viongozi wake, hivyo ni uongo mkubwa kudai limegeuzwa kuwa “azimio la wala rushwa na ufisadi” ila ni chuki zake mwenyewe za kisiasa.

Aidha, siyo kweli kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alifanya kazi peke yake ya kuwaondoa wakoloni hapa nchini, badala yake ilifanywa na Watanzania wote waliokuwepo wakati huo. Tunachoweza kusema ni kwamba yeye alikuwa ni kiongozi wao kupitia chama cha TANU kwa Tanzania Bara, halafu Sheikh Abeid Amaan Karume aliyekuwa Rais wa ASP akiongoza mapambano hayo huko visiwani Zanzibar.

Kama ni hekima au busara kamwe haziwezi kumwendea yeye peke yake ila Watanzania wote waliokuwepo, lakini wendawazimu wachache wamekuwa wakimtumia kuonyesha chuki zao za kisiasa dhidi ya viongozi wa serikali iliyopo madarakani hivi sasa.

Kuhusu madai kuwa wakati wote wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza haukuwepo mgomo wowote, Padri Mapunda pia aliamua kuzungumza uongo huo kwa sababu ya chuki hizohizo, hasira za mgombea urais aliyekuwa akimuunga mkono mwaka 2010 kushindwa vibaya, hali iliyoepusha kuundwa kwa serikali ya ubaguzi wa kidini na hasa ukatoliki nchini.

Mwaka 1967, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwemo aliyekuja kuwa Spika wa Bunge mwaka 2005, Samwel Sitta waligoma kwa madai ya kisiasa dhidi ya Serikali ya Awamu ya Kwanza, kisha wakatimuliwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe hadi walipokuja kumwangukia na kuomba radhi.

Aidha, hakuna ubishi kwamba wakati wote wa Operesheni Vijiji vya Ujamaa mwaka 1974, maelfu ya Watanzania walishurutishwa kuhama kwenye makazi yao ya asili huku nyumba zao zikichomwa moto kwa mtutu wa bunduki, na pia kuna wengine walipigwa risasi na kujeruhiwa kwa namna moja ama nyingine hasa waliokuwa wakigomea zoezi hilo.

Ilipofika mwaka 1982, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha Jeshi la Polisi waliopelekwa wilayani Tarime, mkoa wa Mara, walitumia nguvu za ziada kuzima uasi na kumwaga damu dhidi ya raia waliokuwa wakivunja sheria na kutotii mamlaka ya serikali iliyokuwepo madarakani kwa kuwapiga risasi.

Akihutubia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mwaka 1986, wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Mwalimu Nyerere pia aliunga mkono mauaji yaliyofanywa na askari hao wa FFU kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero mkoani Morogoro waliokuwa wamegoma, kufanya vurugu na kuandamana kinyume cha sheria.

“Kazi ya bunduki ni kuua, kumbe zipo kwa ajili ipi? Kama watu hawataki kutii sheria za nchi hata kama ni mbovu, wanapambana na polisi hapo unadhani askari watafanya nini wakati wana silaha hizo mikononi?” Alisema Mwalimu Nyerere alipokuwa akiitetea Serikali ya Awamu ya Pili kwa kupambana kikamilifu na uvunjifu wa sheria kwa makusudi.

Katika hali hiyo, ni uongo mkubwa kudai kwamba mauaji dhidi ya watu wanaofanya hivyo yameanza wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne, na pia ni uzushi kuwa Baba wa Taifa aliwaunga mkono wendawazimu wachache wanaovunja sheria kwa kutotii mamlaka zilizopo madarakani.

Kama Padri Mapunda angekuwa halitumii Kanisa Katoliki kuhutubii siasa za uchonganishi, uchochezi na ubaguzi asingefanya ubaguzi wa kidini na chuki, badala yake angefuata nyayo za bosi wake hata kama kwa kuvunga, Mhashamu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam anakofanya kazi katika Parokia ya Manzese.

Lakini kwa sababu ana ubaguzi wa kidini na itikadi za kisiasa, Padri Mapunda amekuwa hasemi chochote wakati viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanapotoa kauli za uchochezi na hatari.

Hakusema chochote wakati Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa alipotangaza kwa kinywa chake mwenyewe, tena hadharani kuwa Tanzania isingetawalika aliposhindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Alisema nchi ingemwaga damu, na kwamba Rais Kikwete kamwe asingefika hadi mwaka 2015 akiwa bado madarakani ila angeng’olewa kwa mabavu kinyume cha sheria na katiba ya nchi hii.

Hakusema chochote pale Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Joshua Nassari aliposema mkutanoni kwamba Chadema ina mpango wa kufanya uhaini wa kuitenga mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro na kuanzisha Jamhuri ya Watu wa Kaskazini.

Naamini hakuwakemea kwa sababu ya itikadi za kisiasa, upendeleo na ubaguzi wa kidini kwa sababu ni wakristo wenzake huku Dk. Slaa akiwa padri wa zamani wa Kanisa Katoliki, halafu Nassari ni mtoto wa Mchungaji Samwel Nassari wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mlima Meru.

Hakukemea mauaji yaliyofanywa na polisi kwenye Msikiti wa Mwembechai jijini Dar es Salaam mwaka 1997, na pia hakusema chochote baada ya mauaji ya Pemba mwaka 2001 kwa vile Rais aliyekuwepo madarakani wakati huo, Benjamin Mkapa ni muumini wa Kanisa Katoliki.

Hafanyi kama Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambaye amekuwa mstari wa mbele kutetea watu wote wanaovunja sheria, kuhatarisha amani au kutoa kauli za uchochezi bila ya kujali imani zao kiroho na kukemea matendo yote maovu.

Amekuwa akiwa akifanya hivyo huku akiwataka watu wote kuheshimu sheria za nchi, kutii mamlaka au serikali inayokuwepo madarakani kwa vile zote “zinawekwa na Mungu” kama inavyosema Biblia Takatifu.

Kabla sijafikia mwisho, sasa ninaomba nionyeshe kuwa kauli ya Padri Mapunda ya kukemea kile alichodai ni “tabia ya kupeana uongozi ndani ya familia moja” siyo lolote wala chochote ila ni uzandiki, fitina, uchochezi na harakati zake za kisiasa dhidi ya CCM.

Kama angekuwa anakerwa na hali hiyo, tena kwa vitendo angekuwa amewakemea viongozi wa Chadema kwa kuwajaza wake zao, dada zao, watoto wao na ndugu zao wengine bungeni kwa kivuli cha Viti Maalum.

Wakati wa kutafuta wabunge hao mwaka 2010, Kamati Kuu ya Chadema iliyafuta matokeo halali ya washindi waliopigiwa kura na akina mama wenzao katika Baraza la Wanawake la Chama hicho (BAWACHA), uchaguzi ambao ulifanyika kikatiba katika Ukumbi wa PTA uliopo kwenye Uwanja wa Sabasaba, Mtoni jijini Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Mshauri wa Kisiasa wa Chadema na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Mkumbo Kitilya, washindi wengi waling’olewa kwa sababu tu walitoka kwenye kambi inayomuunga mkono Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Waling’olewa kwa sababu hawakutoka kambi ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Wilborad Slaa na viongozi wengine wa kitaifa. Hapo ndipo uchaguzi huo ulipofutiliwa mbali na badala yake, wabunge hao wakateuliwa ofisini kwa kuangalia familia zao au mahusiano mengine kati yao na viongozi waandamizi wa chama hicho.

Baadhi ya wabunge hao ni Rose Kamili ambaye ni mke wa Dk. Slaa, Christina Lissu (dada yake na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu) na Raya Ibrahim Khamis, mtoto wa dada yake na Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar), Saidi Issa Mzee.

Wengine ni Mhonga Saidi (binamu yake Zitto), Anna Komu (shemeji yake Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Anthony Komu), Lucy Owenya (binti wa Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mjumbe wa Kamati Kuu, Philemon Ndesamuro) na Grace Kiwelu ambaye ni mke wa mtoto wa Ndesamburo na kadhalika.

Huu ndio uongo, uzushi, umbeya na uzandiki unaofanywa na Padri Baptiste Mapunda dhidi ya CCM na serikali yake, ule ambao unakwenda sambamba na mapenzi yake makubwa ya kisiasa kwa Chadema katika upande wa pili!
 
Kinachosikitisha ni kwamba hali ya hewa ikichafuka kutokana na tabaka fulani kupendelea wateule wao wachache,viongozi hao hao walio sababisha hali hiyo tete huwa wa kwanza kutaka msaada toka kwqa viongozi wa kiroho kuwaweka sawa waumini.

Ni hatari kwa taifa dhaifu lililo kosa uadilifu kuthubutu kumkemea kiongozi wa kidini kwa kitendo cha kukosoa na kusimamia maadili ya jamii husika.Watasema sana lakini hawatashinda,siku ya kufa nyani miti yote huteleza.Rudi kajipange upya,jamii inapokosea lazima ielezwe bayana

wanapoongea viongozi wa uamsho huwa hatuwaoni au ndio Padri ???
 
Muulize ana watoto wangapi mtaani manake siku hizi imekuwa ajira sio utumishi wa bwana tena.Kesho kutwa tusishangae akawa katibu msaidizi wa christian democratic movement (cdm)
 
Mleta uzi umeharibu kwa kuandika kwa jaziba na chuki na mwisho wa yote kile unachomtuhumu Fr.Mapunda umekienzi wewe. Umeonysha chuki dhidi ya watu wengine na CDM bila sababu. Ungemtuhumu padre huyu bila kuonyesha kuwa wewe kwako tuhuma ziwe tuhuma lazima ziwe ni kwa chama kingine lakini sio CCM. Kosa ni kosa na haliwi kosa kwa sababu na wengine wamelifanya. Kwa CCM sioni unachokitetea. Mauaji na migomo haiwezi kuwa jambo jema pale ambapo uwezo wa kuvizuia vitu hivyo upo. Watu wanadai haki zao zilizoporwa wewe unasema huna fedha lakini unafanya sherehe za mabilioni, safari zisizoisha na ambazo zimedhihirisha pasi na shaka hazina tija. Hapo kweli utawalaumu wanaogoma. Utawatetea wanaosababisha wagome? Migomo ya wakati wa Mwalimu na ya sasa are two different things and causes are different. Hii ya sasa hivi ingeweza kuzuilika lakini inasababishwa na seriakli na chama ambao wamekosa vipaumbele na uzalendo. Huu ni ukweli unaosemwa kila uchao na wengine wanasemea chinichini lakini akitokeas shojaa kama padre huyu kwako inakuwa nongwa. Kwanini usimlaumu Frederick Sumaye kwa yale aliyosema juzijuzi. Kwanini usimlaumu Ulimwengu na Mbwambo na makala zao zinazokosoa serikali na CCM. Hivikwa sababu padre kasema. Alichokisema padre ndicho wenye mapenzi na wazalendo wa nchi hii wanakisema. Usifukie uchafu chini ya busati
 
jitafakari watu watakavyo kujibu. unaona majibu ya watu, hao wote hawaichukii ccm nadhani wana hoja za msingi
 
Mleta mada kaandika kirefu na kwa namna ya kuchosha sana.

Padre yoyote ana wajibu wa kukemea maovu katika jamii. Na CCM ya leo ni uovu uliokithiri. Kusema kuna wengine waovu pia haifanyi CCM isafishike. Two wrongs don't make a right.
 
Mbona Museveni analaumiwa kwa mambo haya haya ya JK? Nduganization of politics is a bad omen for Tanzania
 
Hivi kwa akili yako unategemea Padri Mapunda atakuwa chama gani.

hana chama mapadr hatoruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa azimio hilo lilipitishwa na baraza la maaskofu katoliki Tanzania mwaka 1992.. Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza ila hapo nyuma engi waliokuwa interested na siasa walikuwa TANU na baadaye CCM
 
si alichoongea padri mapunda ndiyo kilicho fanya watu wachukie ccm. hata kama asiongea. kama wewe ni mchafu ni mchafu tu siyo mtu akikwambia ndiyo watu waone, ni sawa sawa na CCm ata kikisimama chenyewe bila kusemwa ni chama kichafu mno. ukitakka kupima kama akili yako iko sawa check kama una kipenda ccm? kisha utajijua kama wew si mgonjwa wa akili. kuona uchafu wa CCm si lazima uwe mwana chama wa CDM ili mradi tu usiwe na aki finyu na unafki.
 
sidhani kama kuwa tu na uhusiano na mtu maarufu ni ticket ya kuwa condemned katika shughuli za public au kazi za kuteuliwa.

si haki kuwanyima watanzania wenzetu hawa kuwania hivi viti,
hawa wamekuwa exposed kwenye hizi shughuli tangu wanakua, wanapata ushauri wa mbinu na mitazamo toka kwa watu waliobobea,
maisha yao yote wako informed na hizi issue, sio rahisi kuwafuta humu, baadhi yao hii ndio career pekee wanaoijua.
ni kama mimi uniweke pamoja na mtoto wa mkulima au mfugaji utegemee tuvune sawa!! haiwezekani.
malezi ya watoto yaathiri sana akili zao na mitazamo yao watakapokuwa watu wazima. (effects nzuri au mbaya)
Mi nadhani tuwapongeze hawa wazazi kwa kuweza kuonyesha kwa vitendo na kuinfluence kizazi chao kupenda kizi kazi za jamii.

LAKINI: TAHADHARI, natumaini KILICHOWAVUTIA NI KUWA wameona kazi nzuri za wazazi wao, sio opportunity ya kuonea, kukanyaga, wananchi wasiojua humo ndani kuna nini.
 
Hivi kwa akili yako unategemea Padri Mapunda atakuwa chama gani.

Ukiona mtumishi wa Mungu - awe Shehe au mchungaji yuko CCM kuna mawili.
Aidha ni muuza madawa ya kulevya na hivyo anahitaji ulinzi wa serikali ya CCM, au Yuko CCM kuikemea na kuwarudisha mafisadi kwa Mungu. kama yupo CCM basi anabelong kwenye kundi la pili, maana waliokundi la kwanza wanajulikana kwa matendo yao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom