Huu ndio unafiki wa Ndesamburo na pesa zake

kwani hawa magamba wanaalili ya kutambua hilo?

angel unajua machalii wengine ndio firt time wanafika mo town na wanabaki wanabung'a bung'aa tu ka mtumba wa KB...wacha niingie zangu walindi nikapate mchemsho.
 
kama unakuwa na unamiliki kampuni then hujui unawafanyakazi wangapi, hujui wanalipwaje? then wewe utakuwa punguani

Punguani??? Wewe utakuwa hujui management. CEO ahangaike na trivial issues za kampuni wakati kuna mameneja na wakuu wa idara? Wewe utakuwa magamba maana magamba ndio zao za kutojua science of managing.
 
pesa ndogo sana, eti kwa kisingizio wanapata "TIP" toka kwa watalii, tunawasiliana na kiongozi wa kilimanjaro porters association tuweze kupata figure za ukweli
Pesa ndogo ni kiasi gani na weqwe ulitaka walipwe kiasi gani?...
 
Hamjanielewa,mimi binafsi nakubali sana mchango anaoutoa pale moshi, ila kilchonishtua ni mamilion ya pesa aliyochangia chama chake ilhali wale wapanda mlima wanalia njaa mitaani kwa ujira mdogo

ujira mdogo ni upi?
 
hawa ni wale wanaopanda mlima wakishashuka wakilipwa wanahamia bar wanakunywa anzia asubuh wanatoka nje kuangalia mlima Kilimanjaro wakiuona wanarudi bar kwa mbwembwe wakisema mlima haujaama kesho tutapanda wanaagiza bia+nyama+ changudoa, HUYU WAMEMMALIZA HANA NGUVU ZA KUPANDA MLIMA TENA AMEONA ALIE NA NDESA

nimecheka sana hawa jamaa wanavituko sana nimeishuudia hapa malindi night club.

Kwanza kwenye miaka ya 2008 walikuwa wanalipwa 12,000/= kwa siku sasa itakuwa juu kidogo.
 
Mimi binafsi siwezi kumlaumu Kashaga kwa malalamishi yake. Inaonyesha hajui au nimbumbu wa mambo ya utawala katika biashara labda ni mwanafunzi au ni mfanyakazi wa Serikali.
Utawala wa biashara una anzia chini huku tuliko, nitoe mfano mmoja kwa faida yake. Kashaga ameamua kujenga nyumba ya kawaida ya kuishi, anapatana na fundi ujenzi kuanza msingi, fundi anamtandika 1.5m gharama ya ufundi pamoja mambo mengine ikiwamo kuchimba msingi. Hapo kawaida huyo fundi atachukua vibarua kwa kazi ya kuchimba na kumsogezea udongo na matofali. Mwisho wa kazi ya msingi vibarua wanalalamika kuwa Kashaga kuwa kawapunja hela ya kazi. Hapo kama hana jazba atawashauri hao vibarua warudi kwa fundi aliewapa kazi ili wapate haki waliokubaliana.
Kashaga mwache mzee ndesa apumzike, kafanya mengi na bado anafanya mengi
 
Back
Top Bottom