Huu nao ni ufisadi, japo ni ufisadi dagaa nao unapaswa kukomeshwa

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Yupo mtu, raia wa Kenya aliwahi kuniambia kuwa, watanzania wote ni wezi. Nikamkatilia kata kata. Tukabishana sana, mwisho tukaachana bila kufikia muafaka. Lakini baadaye nikagundua kuwa, madai ya yule Mkenya yalikuwa na ukweli kwa asilimia kubwa. Ufisadi huu wa vidagaa unafanyika sana kwa wafanyakazi wa Serikali hasa hii ipo zaidi katika wizara ya elimu.

Wakati wa kuajiriwa. Unakuta mtu Kwao ni Kigoma, kapangiwa kufanya kazi Kigoma. Lakini ukiingia katika faili lake utashangaa kukuta maelezo yanayoonyesha kuwa kwao ni Mtwara. Mtu wa Dodoma, anafanya kazi Dodoma. Lakini utashangaa mgogo naye kageuka kuwa Mhaya wa Bukoba.

Mnyaru naye anadai kwao ni Tanga huku Mbondei anageuka na kuwa Mnyakyusa. Ilimradi kila mtu anafukuzia nyongeza ya vijisenti vya nauli wakati wa likizo. Sijui kwa yale makabila ambayo ndimi zao haziachi rafudhi ya asili kuongea kama wachaga, wakurya na wasukuma. Sijui inakuaje pale mchaga anapodai kwao ni Iringa! Hakika huu nao ni ufisadi pia.
 
Acha tu wafanye hivyo coz hawafanyi manunuzi yoyote ya kupata 10% japo wanafunzi wao wakishafika maofisini hawataki tena 10% ila wanakula 90%
 
Tatizo ni system.. Ndiyo maana watu wanaona chama mbadala ni bora kuliko hiki kilichopo. Kila awamu kinapoendesha serikali,ni uozo unaoanzia juu.. Huko chini unakoongelea ni kwa waganga njaa tu! Nikupe mfano mmoja utashangaa. Kwamba,kuna fedha zinazotumwa kwenye H'shauri za nchi hii kwa ajili ya Ukimwi[chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii]. Mnapoandika mchanganuo, ndipo mnapopewa fedha. Cha ajabu,yule mhusika wa mfuko huo wizarani,hatumi fedha kabisa ama atatuma kidogo kwa zile H'shauri ambazo hazikuandaa mazingira ya kumpa % huyo bwana! Matatizo yanaanzia juu kwa kifupi.
 
Back
Top Bottom