Huu msafara wa rais ni hasara kwa taifa....!

Ochutz

JF-Expert Member
May 21, 2011
465
105
Rais yuko kusini anaelekea nachingwea,msafara wake ni atleast gari 40 ivi. Mi natatizwa na suala hili. Kwani kuna ulazima wa kila mtu kuwa kwenye uo msafara! Kwa nini wengine msimsubiri kwenye maeneo yenu. Jamani kuna masuala muhimu yanahitaji kushughulikiwa na serikali kwa nini tunatumia gharama kubwa kwenye mambo yasiyo ya msingi. Aaaaaaagh mnaboa sana sisiemu.
 
Wewe unataka hao wengine wakale wapi? wana familia pia - mbona mnataka kuharibu ajira za watu?
 
Msafara unakuwa mrefu kwa sababu ya idara mbalimbali zinazohusika na msafara huo. Kama atatembelea secta 10, basi tegemea wakuu wa idara hizo watakuwepo kutoa maelezo au hoja. Tusitangulize suala la mlo tu katika masuala ya kitaifa.
 
mimi sina tatizo akiwa kiofisi ila nina tatizo pale anapokuwa yupo nchini kila weekend anaenda kwake msoga,anasababisha foleni sana halafu ni safari zake binafsi lakini huo msafara ni mkubwa sana,inatumika hela ya kodi ili akatambikie kwao b'moyo...
 
ngoja atembee nao... sasa hivi ni mjanja sana anatembelea sehemu ambazo anazijua yeye....mwambieni aje kushukuru wapiga kura wa mwanza huku au arusha
 
mimi sina tatizo akiwa kiofisi ila nina tatizo pale anapokuwa yupo nchini kila weekend anaenda kwake msoga,anasababisha foleni sana halafu ni safari zake binafsi lakini huo msafara ni mkubwa sana,inatumika hela ya kodi ili akatambikie kwao b'moyo...
Mwalimu Nyerere alipokuwa anaenda Butiama kibinafsi alipewa escort na wapambe kibao kama RAIS,

Mwinyi nae alipokuwa anaenda Yombo kusalimia jamaa zake alipewa ulinzi kama RAIS,

Che Mkapa alipokuwa anaenda Lupaso kunywa NIPA na wamakua wenzie alipata ULINZI kwa gharama za walipa kodi.

JE leo JK kwenda kucheza bao kila week end Msoga kwa gharama za walipa kodi imekuwa KOSA????
 
JE leo JK kwenda kucheza bao kila week end Msoga kwa gharama za walipa kodi imekuwa KOSA????

Ahaaa lazima kuna uongo hapa! Bao analijuwa kweli huyu Jamaa, maana bao linahitaji akili alikuwa analicheza sana Nyeerere huyu labda kucheza Mdundiko na Mnanda
 
Ahaaa lazima kuna uongo hapa! Bao analijuwa kweli huyu Jamaa, maana bao linahitaji akili alikuwa analicheza sana Nyeerere huyu labda kucheza Mdundiko na Mnanda
Watu wanali underestimate bao, lakini mtu mwenye akili ndogo hawezi kucheza bao maana linahitji mahesabu ya hali ya juu, siamini kama Mkwerre anaweza kuwa na hesabu hizo.
 
Back
Top Bottom