Hussein Bashe: Wabunge wa CCM acheni kupinga kila jambo!

Unajua hizo Bilioni 900 pamoja na hizo bei za kuruka za barabara yah lami 1bn kwa kilometre unachapa kile kipande cha Mpanda mpaka Kigoma mpaka Nyakanazi, the rest huku kwenye Mbeya -Tabora mpaka Nzega. Automatically biashara ya njaa Tanzania unakuwa umeiua kabisa.
 
Ndio kawaida yao hawa magamba wakiwa nje, wakikumbukwa wanageuka kama alivyogeuka Nape.
 
Gamba likijeruhiwa lina akili sana. Likipewa sehemu ya kula posho halifikiri kabisa. Mnamkumbuka Mwakyembe?
Ila kwa kauli hii Bashe nakupa Tano. Ila nakusubiria 2015 watakupa ubunge sijui hizi kauli bado utakuwa nazo?

Kama kweli tukiwa na moyo wa dhati wa kujenga uchumi bila kujali itikadi zetu za vyama tutafika haraka.
 
Hussein wote wamekuunga mkono lakini mimi sikubaliani na wewe kwenye jambo hili "wabunge wa ccm hacheni kupinga kila jambo"...sikubaliani na wewe kuwa wabunge wa CCM wanapinga kila jambo kama ambavyo unataka kuonyesha hapa....
1.Mtu wa kwanza kusema kuwa posho ziangaliwe upya siyo Zitto kama ambavyo unataka kuonyesha hapa bali ni mpango wa miaka mitano wa maendeleo ambao JK aliuelaza kwenye hutuba yake dodoma siku chache kabla ya bunge.
2.Sikweli kuwa wabunge wote wa ccm wanapinga ila wapo walooongea na wengi bado hatujui maoni yao kwa hio kwa kiwango cha uelewa wako kusema wabunge wa ccm kwa ujumla wao ni kutowatendea haki watu kama january makamba ambao nao wanaona kuwa poisho ziondolewe
3.jambo la kudai posho ziondolewe litakuwa ni la kisiasa au kutafuta umaarufu kwa sasa kwani wakati Sitta akipitisha kila mtu alipinga na wao wakaendelea ,leo kuona kama ni karata ya kisiasa ndio wanatoka nalo mbio.
4.Ninaamini ni jambo ambalo lilipitishwa kwa utaratibu na liondolewe kwa utaratibu na lisigeuzwe kuwa ni ngazi ya kujipatia umaarufu kwa wanasiasa wa upinzani hata siku moja
Wenye masikio na wasikie.
 
Hivi huyo mbunge wa bashe kwa nini asijitoe.. Hizo posho zake ampelekee yule kijana anaye tumia jina lake ...
 
Alishabau huyu naye katokea wapi tena.......................kujipendekeza tu,,,,si aende sudan kaskazini akasaidie kujenga taifa jipya?.....watu wengine ni kutafuta umaarufu tu...kwanza aliambiwa sio raia na akaenguliwa kwa kigezo hichohicho ktk nafasi ya kugombea ubunge yeye akasema ni raia na hajachukua hatua yoyote...............hivi watz ni mapoyoyo kiasi hiki mpaka maalshababu wanatusemea?......au niulize huyo alishababu alifika hapa nchini kwa lengo gani na au vibalui vyake vinamruhusu kufanya shughuli gani?....au huyu alishabau yeye kabila gani hapa tz au alizaliwa wapi vile?........watu km hao wana mambo mengine zaidi ya kufanya kuliko kuingilia mambo ya ndani ya nchi....maalishababu km hao tuwakaribishe na tuwaachwe wafanye biashara zao na si vinginevyo..................*&&^^*&^%^%&*^%$%&%%,,,,,mi nawachukia sana kwani hawana uzalendo wowote na wanafiki tu...tazama akina rostam mtu ambaye ni msukuma piwa anavyoliibia taifa kwa mbwembwe................
 
kwa kweli mimi nimependa post yako, kuna mambo ambayo ni ya maslahi kwa taifa hivyo hakuna haja ya kuangalia upo chama gani. hivi baba yako akiwa chama kingine halafu akakwambia soma kwa bidii mwanangu ili ufaulu we utabisha na kuamua kulala usingizi kwa sababu tu baba ni mpinzani wako kiitikadi? jamani wabunge wa CCM na makada wao wote kwanini hamna uzalendo? hivi kwa Mungu mtajibu nini? hizo posho za kukalia viti mkiziacha je mtakufa kwani? mbona hammwogopi hata Mungu? Kumbuka; yeyote asiyejali wa kwao ni sawa na mchawi.
 
Nimechefuka na the so called mtoto wa mkulima...eti anatoa hoja ya kwamba fedha hizo ni kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali wanaokuja wakati wa bunge. Hizi ni hoja mfu kabisa tena mufilis. Matatizo ya wananchi wa majimbo wanakotoka wabunge yatamalizwa na vijisenti hivyo vya posho? Mbona tunakosa uwezo wa kufikiri na kujenga hoja wananchi tuwaelewe? Huu ni upuuzi usiomithirika hata kidogo. Bado sijaona uteteze wa maana hapa. Tuanapaswa kufika mahali ambapo Ubunge uwe na maana ya uwakilishi na si ajira ya kuwenda kuepna fedha, na matokeo yake tunayaona watu na taaluma zao wamekimbilia siasa badala ya kujikita katika kutoa huduma zinazoendana na taaluma zao.
 
Bashe Umenigusa Mtima wa Roho Yangu
Nakuombea Mungu akupe Umri, akulinde akutane na haja za Moyo wako katika Jina la Yesu Kristo Amen!
 
Jamani naona kila mbunge wa ccm anaye simama lazima aunge mkono hoja? Je asipo unga mkono hoja atafanywa je na wakina NEPI? Make c jaona mbunge wa ccm akikataa kuiunga mkono hii bajeti na mijadala mingine. Nisaidieni kwa hilo.
 
Kwa jinsi mbunge huyu Stephen Julius Masele alivyo anza kuchangia nilidhani ana jambo la muhimu kwa kauli yake yakuanza kuponda kwamba Bunge lina jadili swala muhimu sana na kile siyo kikao cha harusi.......
Mara kaanza kusifia wasukuma kwa kula sana.......... Hivi hili ndilo alilotumwa na wapiga kura wake kweli?
 
Hao unadhani wanafikiri kwa vichwa vyao, mwenzangu wanasemina elekezi na theme ni naunga mkono hoja hawana jipya unaona kabisa katika maelezo yake yote anapingana na bajeti lakini mwisho wa siku inakuwa naunga mkono hoja
 
Kwa jinsi mbunge huyu Stephen Julius Masele alivyo anza kuchangia nilidhani ana jambo la muhimu kwa kauli yake yakuanza kuponda kwamba Bunge lina jadili swala muhimu sana na kile siyo kikao cha harusi.......Mara kaanza kusifia wasukuma kwa kula sana.......... Hivi hili ndilo alilotumwa na wapiga kura wake kweli?
Kwa kula nini?
 
ungeendelea kumsikiliza ungepata logic ya huo usemi. Sawa Great thinker.
 
Back
Top Bottom