Hussein Bashe aongea na vyombo vya habari

Tumuache Bashe afanye kazi yake aliyotumwa. Tusianze kumjadili, tutampoteza na hivyo ashindwe kufanya kazi yake vizuri.
 
KWA MTINDO HUU HIVI KWELI TIMU YA KIKOSI KAZI ANAYOIONGOZA HUSSEIN BASHE KUSAIDIA KULETA MUAFAKA NA MWELEKEO MPYA NDANI YA UVCCM ITAKUWA NA MATUNDA YA USAWA KWA MATAWI YOOOTE YA UVCCM NCHINI BILA KUENDELEZA UBABE WA MAKUNDI KIBAO NDANI YA CHAMA TAWALA?????????????

Duuh, kumbe Hussein Bashe huwa ni kijana mwanasiasa mpika majungu hivi??? Kwa nini abuni story kisha aishie bila kutaja mdaiwa wake wala kutoa uthibitisho wowote usiozua maswali zaidi???

Je, matawi ya UVCCM katika hiyo mikoa alioitaja kwenye kashfa nzito, ya 'kutumiwa watu kusaidia matawi hayo kuchafuana', wenzake hao wazungumzia vipi haya Majungu yenye shutuma zito bila uthibitisho wowote.

Kwa mtaji huu wa Bashe, je kamati hiyo ya UVCCM Reform itaweza kweli kusaidia kuibua njia na mikakati unganishi kama mwenyekiti mwenyewe wa hicho kikosi kazi ndio tayari anauza sura kwenye kioo kwa kuwashutumu wenzake kula njama hivyo???

.... Suala ya yeye, Shigella na Ridhiwani kudaiwa ni mafisadi kasema ni maoni ya watu. Ila akasisitiza ndani ya CCM pamevamiwa pia na yeyote sasa anaweza kuongea na vyombo vya habari na kutoa taarifa tu!

  • Anasisitiza mkakati wa kuchafuana ndani ya UVCCM unajulikana unasukwa na nani na anaye-finance anajulikana kwani dhamira yake ni urais 2015. Ametuma vijana Iringa, Mbeya, Ruvuma na anaendelea kuwatumia wengi. Itafika wakati watalazimika kumtaja hadharani.

  • Kaulizwa kama wataitumia JF kakiri kuwa wataitumia pia kukusanya maoni ya wananchi kuelekea kuifanya UVCCM irejeshe heshima yake na ku-appeal kwenye public.
 
waangalie ni jinsi gani wanaweza kunishawishi mie ambae sina kazi, ninapata mlo mmoja kwa siku maisha yangu ni magumu sijui kesho ntaishije ili niweze kua na imani na chama ambacho viongozi wake ni mafisadi wanatembelea magari ya gharam ya milion 300. wakiweza kunishawishi basi hapo watapata vijana wengi
 
Huyu kijana jana 03-05-2011 akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya UVCCM taifa alidai uhuru wa kutoa maoni umezidi na hivyo kuwa Fujo.

Binafsi nilimfagilia aliposhinda kura za maoni nzega japo baadae shoka la zengwe la uraia likamshukia na baadae kusafishwa kiaina na hata pia mabadiliko aliyofanya Habari Corp yalikuwa na mwelekeo mzuri.

Ila kwa mtazamo wangu naona kijana amelikoroga kwa kutetea hoja ya kunyamazisha watu kutoa maoni yao juu ya hatma ya serikali yao.

Najiuliza pia hii series ya kauli ya viongozi wa UVCCM akina Shigela, Riz1, Malisa na wengineo zinalenga nini? wametumwa hawa!
 
watuhumiwa wa ufisadi hao.
Kunyima watu kutoa maoni kutazalisha Somalia hapa Tz

Eti vipi tuhuma za Bashe ,Rz 1, Shigile kuwa mafisadi waliziongelea?
 
Huyu anasumbuliwa na masilahi yake kwa mafisadi ambao ndio hasa walengwa wa uhuru wa kutoa maoni anaoupinga, wengine tulitarajia hayo wali hatushangai.

Lakin akumbuke pia kama kusingekuwa na uhuru wa kutoa maoni hayo maoni yake ya jana angeyatolea wapi??
 
Huyu kijana jana 03-05-2011 akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya UVCCM taifa alidai uhuru wa kutoa maoni umezidi na hivyo kuwa Fujo,binafsi nilimfagilia aliposhinda kura za maoni nzega japo baadae shoka la zengwe la uraia likamshukia na baadae kusafishwa kiaina na hata pia mabadiliko aliyofanya Habari Corp yalikuwa na mwelekeo mzuri
Ila kwa mtazamo wangu naona kijana amelikoroga kwa kutetea hoja ya kunyamazisha watu kutoa maoni yao juu ya hatma ya serikali yao
Najiuliza pia hii series ya kauli ya viongozi wa UVCCM akina Shigela,Riz1,Malisa na wengineo zinalenga nini? wametumwa hawa!
...haachi asili yake ndio maana hataki uhuru wa kutoa maoni yalivyo hapa. Anataka iwe kama kwa babu zake!
 
Siku hizi ukiwa na swala lolota tu unaita press conference. Hivi hii ina maana gani?? Bashe naye ni nani hadi kuongea na waandishi wa habari?/ Maadili kwisha kabisa siku hizi.

Riz 1 naye juzi kaitisha, sasa mambo yamekuwa kama ukoo wa kambare.
 
Sikuizi kila mtu ana press conference, hata mtotowamgu wa darasa la sita anacheka, kwa mtu kama bashe kuwa na hii. Duhh:phone:
Benno Malisa utajuta kumpa huyo mkimbizi hii kazi, ina maana ulishindwa kupata kijana mtanzania mzawa si siri hili nitatizo kubwa sana kutegemea wageni waje kututatulia matatizo yetu hii ni fedheha
 
Bashe ni mfa maji, tusubiri wenye akili, nadhani JF tunao wengi sana! Suala la Uraia lilijibiwa kwamba halina utata, yaani BASHE si RAIA HAKUNA UTATA
 
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, Hussein Bashe, amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimevamiwa na watu ambao wameanza kutumika kwa maslahi binafsi ya watu wachache.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kamati ndogo anayoiongoza ya kukusanya maoni na kuandaa mapendekezo ya mageuzi ndani ya umoja huo.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa kuhusu shutuma zilizoelekezwa kwake na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa umoja huo Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Matefu, kuwa yeye (Bashe) ni fisadi.

Alisema tuhuma hizo hazina msingi na ni za jumla jumla kwani Matefu hakusema ufisadi huo ni wa aina gani na umefanyika wapi.

Alisema hakuna sababu kwa viongozi wa UVCCM akiwemo Katibu Mkuu, Martin Shigela, Makamu Mwenyekiti, Beno Malisa kujiuzulu kwenye nafasi zao kama ilivyoshauriwa na Matefu.

Alisema kuna vijana ndani ya umoja huo ambao wamenunuliwa na watu fulani ambao huwatumia kwa ajili ya kampeni zao za urais wa mwaka 2015.

Bashe alisema vijana hao wamekuwa wakiandaliwa maneno ya kuzungumza na hata sehemu za kuzungumzia na waandishi wa habari, gharama ambazo kwa uwezo wao binafsi wasingemudu.

Kuhusu kuenguliwa kwake kuwania ubunge wa jimbo la Nzega kutokana na tuhuma za utata wa uraia wake, Bashe alisema uraia wake hauna utata na hapendi kuzungumzia suala hilo kwa undani.
 
Wew bashe ni mmoja wa wanunuliwa!.Hauna lolote!.usitufanye sisi machizi,Lowasa na Rostam ndo wanakutuma tuma wewe.
 
Kwani si umeona hata gazeti la Mtanzania limebadilisha upepo wa uandishi baada ya Katibu Mkuu wa CCM kuuthibitishia UMMA kwamba swala la kupambana na ufisadi sio la CCM
 
Back
Top Bottom