maulaga
JF-Expert Member
- Feb 22, 2009
- 472
- 120
Mkuu,
Jamaa wanaonekana wanaamini wana ushawishi mkubwa, kama hujashawishiwa wewe basi huenda kuna mamilioni ya watanzania wamefanikiwa kuwashawishi kama wanavyoainisha hapo juu.
Najaribu kushawishika pia lol
Tatizo la nchi hii ni kwamba kila kitu kinapangwa kwa mtazamo wa Dar es Salaam. Hata shule za sekondari za kutwa zilianza kwa mtazamo wa Dar ambako kuna mabasi. Umeme ukikosekana Dar inakuwa kama ni tatizo la wote hata watu wa Lindi ambao hawapo kwenye grid. Dar inakuwa kila kitu.
Mimi naishi na kutembelea vijiji mbalimbali naongea na vijana wakada mbalimbali, nashangaa sana kuambiwa eti jamaa wanakubalika. Kuna mahali ukienda wanashangaa kusikia eti kuna UVCCM. Wengi wanajua kuna CCM kwa sababu wakati wakampeni huwagawia kanga na fulana za kijani baada ya hapo mambo huishia na kupewa pombe za kienyeji au pilau.
Labda urudi mpango wa enzi ya TANU YOUTH LEAGUE ambapo vijana wa shule walishurutisha kujiunga na baadaye ndani ya CCM wanafunzi wa vidato vya tano na sita walilazimishwa kujiunga na CCM kama tiketi ya kwenda chuo kikuu. La si hivyo UVCCM itabakia kuwa ni ya vijana walio barikiwa na vipato au watoto wawenye madaraka na biashara kubwakubwa waishio mijini.
Na ndio maana matamko yote yanatolewa mijini na vijana wa mijini na sio vijijini kama Nanguruwe au Igawisenga. Na watoaji utawasikia ni akina Hussen Bashe, Nape na Ridhiwan. Hao ndio wenye chama, wengine wote ni wadandiaji.