OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 428
bashe tunamjua ni mfuasi wa lowasa! huna jipya bashe na mbinu zenu na hao baba zako RA na EL tunazijua!
Namuunga mkono Bashe Nchi hii ipo katika wakati mgumu kiuchumi ,kisiasa na hata kijamii kuliko vipindi vyote tulivyowahi kupita, na la pili Sioni tatizo kwa Bashe kuwa mfuasi wa lowasa sina tatizo na hili hata kidogo so far lowasa ni kiongozi mwerevu, na mchapa kazi we have to acept that Edo ni miongoni mwa watanzania wachache waliojaliwa kuwa na karima ya uongozi,
Ni nani anayebisha kuwa lowasa akiwa waziri mkuu alifanya mambo mengi mazuri ambayo yanafaa kuenziwa , Ni nani anayebisha kuwa ni Lowasa ndie aliepambana na kuhudhibiti ugonjwa wa Rift Valley 2006 , Tumesahau kuwa ni lowasa aliyesimama imara dhidi ya ajenda za nchi za kaskazini mwa Africa za kuzuhia tanzania kutumia maji ya ziwa victoria,Ni nani anayebisha kuwa ni lowasa ndie aliyewaondoa wahindi waliopora Viwanja katikati ya jiji la Dar es Salaam ,Tumesahau lowasa alivyokuwa anahangaika usiku na mchana kipindi cha njaa mwaka 2006/2007 kuhakikisha hakuna mwananchi anaekufa na njaa ,Ni nani anayebisha kuwa shule za kata ni juhudi binafsi za edo ,Ni nani anayebisha kuwa sera ya serikali kuwa na dispensary kila kata ni jitihada za lowasa ,Ni nani anayebisha kuwa kipindi cha lowasa serikali ilikusanya kodi na kufikia malengo .Tatizo lililopo watanzania tumekuwa wasahulifu
Lowasa ameondoka madarakani miaka 3 iliyopita Nchi inayumba inakabiliwa na matatizo makubwa ya ajira ,mfumuko wa bei ,tatizo la umeme, upungufu wa walimu,upungufu wa uduma za jamii,kufeli kwa wanafunzi kidato cha nne ,Msongamano wa magari jijini mwanza , Arusha ,Dar (Angalau dar edo alituletea barabara tatu na akaomba FFu isaidie trafiki kupunguza tatizo la msongamano wa magari .Tatizo letu sisi watanzania hatupendi kukubali mazuri yanayofanywa na wezetu both in private sector na serikalini ,tumezohea kudanganywa na waandishi wa habari ambao uwezo wao wa kufikiri una mashaka
juhu ya yote We have to agree and apreciate that lowa is a visionary leader