Hussein Bashe Aja Na Yake Ktk Face Book

mchonga

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,233
247
Taarifa ya Bashe Ktk Ukuta wake ktk Facebook

OMBI KWA KATIBU MKUU UVCCM
by Hussein Bashe Bashe on Monday, 28 February 2011 at 07:58
OMBI KWA KATIBU MKUU UVCCM

Ndg yangu Shigela Umewadia wakati wa ww kuita Baraza kuu la Uvccm Taifa tuna wajibu wa kukutana na kujadili kama Taifa tunapitia kipindi kigumu ambacho sisi kama Vijana wa Chama kinachoongoza (sipendi kutumia neno chama kinachotawala) tunatakiwa kukutana tena Haraka kuna mambo mengi yakujadili kwa Maslahi ya Taifa letu na Chama chetu.

Ninafahamu utasema Gharama ya Kuita Baraza kwa maana ya POSHO za wajumbe ita Baraza bila POSHO historia ya Nchi yetu wazee wetu walikua wanakutana bila kulipana posho tujitolee wenye uchungu na JUMUIYA,CHAMA ,na Taifa watahudhuria,leo Vijana ajira zinapotea,maisha yanazidi kua magumu,waathirika wakubwa ni Vijana multiplier effect yake ni kubwa,CDM wanatumia haya matatizo kama Mtaji wao wa kisiasa jambo ambalo mm sishangai kwa kuwa sisi wenyewe tumeridhika ama hatuoni haya matatizo ama ni ule utaratibu WA BUSINESS AS USAL,hatuonekani kama we are there to listen help and guide walotupa DHAMANA,kaka yangu MARTIN things are not the way we think they are.

Itisha baraza kuu tukutane we have obligations to this party and this country tumetoka katika uchaguzi october leo ni almost miezi 5 tumeshinda but si ushindi mzuri,tusidhani we are in a safe hands,tusidhani tuko kwenye mfumo wa chama kimoja,wadogo zetu katika sekondari wamefeli,kilimo mpaka sasa kimeshindwa kuwasaidia,ajira sasa viwandani zinapungua UVCCM has to do something.

source:Login | Facebook
 
na bado kumbe wameanza kusoma alama za nyakati. hali ni mbaya hata ajira za kwenye mabenki kwa sasa hazipatikani dah mkap[a uko wapi? Tulikula keki yako wakati tulipomaliza vyuo miaka ile ajira za kumwaga si serikalini na si kwenye sekta binafsi.
Inauma wadogo zetu wanahangaika sana kwa sasa mapinduzi lazima
 
Hayoo ni mawazo ya Bashe au na wajumbe wenzie wa UVCCM??? Hivi Bashe si alifutiwaa ujumbe wake Baraza UVCCM?
 
Hayoo ni mawazo ya Bashe au na wajumbe wenzie wa UVCCM??? Hivi Bashe si alifutiwaa ujumbe wake Baraza UVCCM?
Sisiem haimruhusu huyu jamaa kugombea ubunge Tu, nafasi zingine ndani ya chama yuko huru kutumikia - LOL
 
...Kwa bahati mbaya, kwa sisiemu niijuayo, kilio chake ni sawa na cha samaki, hakiwezi kusikika! Chama chake ni sikio la kufa.
 
Ametoa mawazo mazuri ya kujenga. Kinachotakiwa ni kusimamia anayoyawaza.
 
Hata mngefanya nini kijana timamu hawezi kuwaunga mkono nyie ccm, na wote waliopo humo ni maslahi tu hakuna lolote
 
Haya maneno ya Bashe yananikumbusha mahubiri ya dini yangu juu ya siku ya mwisho (kiama). Kila mtu na lwake!!
 
It will be a waste of time.
Uzoefu unaonyesha kuwa kikao chochote cha UVCCM hii ya sasa hatimaye kitaamua yale anayoyataka Riz1, naye anafanya watakayo washkaji zake na washkaji wa baba'ake.
Au kama vp wafanye tu hicho kikao tuone msuguano kati ya kambi ya Bashe na kambi ya Riz1...
 
Awawezi kufurukuta mbele ya chadema hawa uvsisiem,bashe ni moja kati ya vibaraka wakudumu wa ra na lowassa.
 
Bashe ungekuja CDM huko CCM wamekuchoka..walikunyima ubunge na kukuondolea uraia hivi bado unajipendekeza nini huko?!!maskini!!
 
Back
Top Bottom