Husein Yahaya: Hakuna uchaguzi mwaka huu!

Sheikh Yahya aja na 'uzushi' mpya

na Betty Kangonga

MTABIRI maarufu katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein ameibuka na utabiri mpya kuwa mwaka huu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani hautafanyika kama ilivyopangwa.
Sheikh Yahya alitoa utabiri huo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Hata hivyo, alipotakiwa na waandishi kutoa maelezo zaidi kuhusu utabiri huo alisema kwamba anapotoa utabiri hatakiwi kutolea majibu.
.

Kwa habari zaidi, Soma: Tanzania Daima.
 
Choka mbaya huyo! Hivi nchi yetu inaongozwa na mashetani au nyota na majini?
 
Choka mbaya huyo! Hivi nchi yetu inaongozwa na mashetani au nyota na majini?

"Uzuri" wake huyu kikongwe huwa anajikomba kwa viongozi wa Serikali, la sivyo "angeshanyamazishwa" siku nyingi kwa kutishia watu vifo!
 
Sijui hata hao wanaompa coverage kiasi hicho wana maana gani? Anyway, nadhani wale mashabiki wa mpira juzi walimuonyesha kwamba nyakati zinabadilika!.......
 
"Uzuri" wake huyu kikongwe huwa anajikomba kwa viongozi wa Serikali, la sivyo "angeshanyamazishwa" siku nyingi kwa kutishia watu vifo!

sio kujikomba Buchanan,
huyo Bwana yupo kazini kama Mrema, Marando na wengineo, hayo anayoyaongea sio ya kuyapuuzia hata kidogo, ichukulie hiyo ni kauli rasmi kutoka ikulu, huyo ni mtu wa system miaka nend amiaka rudi
 
aaah, waandishi wanaondaga kumsikiliza na wahariri wao woote hawana kazi y kufanya....wanatuwasilishia ujinga juu ya ujinga wa huyu fisadi wa maneno, tapeli wa viini macho , mpenda viini macho.
 
Choka mbaya huyo! Hivi nchi yetu inaongozwa na mashetani au nyota na majini?

simple...wengine utawatambua kwa PETE walizovaa. Zimezindikwa ati! Mijitu mizima na akili zao zisizo timamu inakubali kulazwa na wafu halafu inakubali pia ku-recharge nguvu za pete kwa maji yaleeeee! inakera kweli. Si unaona ya Shehe Hayahaya. Msimu umewadia!
 
sio kujikomba Buchanan,
huyo Bwana yupo kazini kama Mrema, Marando na wengineo, hayo anayoyaongea sio ya kuyapuuzia hata kidogo, ichukulie hiyo ni kauli rasmi kutoka ikulu, huyo ni mtu wa system miaka nend amiaka rudi
Nchi hii kila kitu kinawezekana!
 
Nimesoma Press Release ya sheikh Yahaya nadhani shida ni ya sisi waandishi, jamaa kasema hakuna uchaguzi mkuu mwaka huu lakini ukisoma utabiri wake hajasema tanzania na utabiri wake amesema unacover nchi zote zilizopata effect ya kupatwa kwa Jua January, kwa hiyo sio neccessarily kuwa tanzania
 
Mimi simlaumu Sheik Yahya maana kama angekosa mashabiki wa mambo yake ya kipuuzi asingeendelea na unajimu katika mambo ya ovyo kama haya. Juzi juzi watu wamezushia vilema na watu wengi waliamini mpaka Polisi ilivyokanusha. Kuna wakati wanavumisha popo bawa na watu wanashabikia. Inaonyesha jinsi jamii yetu ilivyo. Kuamini mambo ya ovyo ovyo wakati wenzetu wanakwenda mwezini!
 
Sheikh Yahya amfagilia Spika Sitta

Boniface Meena

MNAJIMU wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amemwelezea Spika Samuel Sitta kuwa ni kiongozi ambaye kwa sasa yuko juu na kwamba, hakuna atakayeweza kumgusa kwa lolote.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magomeni jijini Dar es Salaam jana, Sheikh Yahya alisema Sitta ataendelea kung'ara na kuibuka kidedea katika kutetea wadhifa wake huo baada ya uchaguzi mkuu kwa kuwa nyota yake ndivyo inavyoeleza.


Alikuwa akitoa utabiri wa mambo mbalimbali ya kijamii na siasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.


"Sitta anaonekana kuwa bado kidedea, atang'ara na hakuna mtu atakayemgusa, nyota yake ndivyo inavyosema bado yuko juu,"alisema Sheikh Yahya.


Hata hivyo alidai kuwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautakuwepo, kwani kutatokea machafuko makubwa nchini na mgawanyiko mkubwa visiwani Zanzibar utakaosababisha Rais Aman Karume aongezewe muda.


Alisema Karume ataongezewa muda kwa kuwa machafuko hayo yatasababisha uchaguzi kutokuwepo lakini, hakuelezea upande wa Tanzania bara itakuwaje.


Sheikh Yahya pia ametabiri kuwa Waziri Mkuu aliyeachia madaraka baada ya kutajwa katika kashfa ya Richmond, Edward Lowassa bado anang'ara pamoja na kwamba mwaka 2015 atajitokeza kugombea nafasi kubwa ya uongozi nchini.


Alisema kuwa utabiri umeonyesha kuwa wakati Lowassa akiendelea kung'ara, viongozi maarufu wataendelea kufa kama alivyowahi kutabiri hapo awali.


Sheikh Yahya alizungumzia pia CCJ kuwa kiliundwa kukiua CCM, lakini hakitafanikiwa kwa kuwa kilikosea nyota. Ili kifanikiwe kilipaswa kuitwa CCN.


"Lakini CCJ wasiogope kuona vigogo wa CCM hawajahamia kwenye chama chao kwani utakapokaribia wakati wa uchaguzi kutotokea mmegeko mkubwa katika CCM na wabunge wengi watakihama," alisema Sheikh Yahya na kuongeza:


"Wamekosea nyota, lakini wasiwe na hofu wakati wa uchaguzi ukifika wataona mmegeko mkubwa utakaotokea," alisema.
 
Hiki Kibabu nacho..Kila siku kinaibuka na jipya..Nadhani uzee unamjia vibaya.Anafuata nyayo za Kingunge..Mwenzie saa hizi katulia tuliii.
 
na Betty Kangonga na Irene Mark

WADAU mbalimbali wamejitokeza na kuuponda utabiri wa mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein alioutoa juzi na kuuelezea kuwa wa kipuuzi hasa katika taifa linaloongozwa kwa sheria na katiba.

Jana vyombo vya habari viliandika na kutangaza kwamba mnajimu huyo alisema zipo baadhi ya dalili zitakazotokea angani ambazo zitafanya kutokuwepo kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

Miongoni mwa waliobeza utabiri wa Sheikh Yahya ni mwanasiasa machachari kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, aliyesema jamii haitakiwi kuupa uzito utabiri huo kwa kuwa nchi inafuata sheria na katiba ambavyo ni muongozo mkuu.

“Najua tunaamini katika sayansi ya siasa na masuala ya sheria, hivyo hatutakiwi kuyapa uzito mambo ya utabiri, hatua hiyo ni kukaribisha ushirikina na inakuwa nchi iliyopoteza dira na mwelekeo wake,” alisema Mnyika.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Masuala ya Haki za Binadamu na Utafiti (AFORD), Julius Miselya, alisema jamii inayomuamini Mungu haipaswi kuogopa utabiri kwa kuwa huo ni ujumbe wa shetani.Askofu Antony Lusekelo kutoka Kanisa la GRC, Ubungo Kibangu, jijini Dar es Salaam alisema mnajimu huyo ametumia umaarufu wake kuita waandishi ili kueleza ndoto zake na kwamba ingekuwa masuala hayo yametolewa na Tume ya Uchaguzi, basi jamii ingeweza kuhoji.

“Sisi hatupaswi kutoa maelezo yoyote katika hilo kwa kuwa yeye ni mtu tu na si tume au serikali na hizo ni ndoto ambazo ameota yeye binafsi na katumia umaarufu wake kuita waandishi ili kuwaeleza, hivyo hatuna la kueleza labda hayo yangesemwa na serikali hapo tungeshauri,” alisema Askofu Lusekelo.

Katibu wa Idara ya Vijana wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Rafael Mgaya, alisema hakuna sababu ya kuamini utabiri wa mtu kutokana na ukweli kwamba bila uchaguzi hakuna serikali katika taifa lolote duniani.

“Hatuamini katika utabiri, huo ni ushenzi. Kwa nini aseme hakuna uchaguzi? Lazima uchaguzi uwepo, bila watu hakuna uchaguzi labda tufe wote ndiyo kusiwe na uchaguzi,” alisema Mgaya na kuongeza kwamba NCCR inaamini kuwa uchaguzi mkuu wa Oktoba upo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, amemtaka mnajimu huyo kwenda likizo na kuachana kabisa na shughuli hizo kwa kuwa anataka kuleta machafuko nchini.

“Huu ni wakati wa sayansi, haya mambo ya kupiga ramli kwa Sheikh Yahya yamepitwa na wakati, anataka kuleta machafuko nchini, tena nashangaa, hivi watu wa usalama wapo wapi? Kwa nini hawamkamati?

“Nasema hivi, Sheikh Yahya anataka kutuharibia nchi kwa umbea wake, anatakiwa awajibike kwa mambo anayoyasema. Mfano huku kwetu watu wamekufa moyo, baada ya kusikia hakuna uchaguzi hawaendi tena kufanya marekebisho kwenye daftari la wapiga kura, je hii ni haki?” alihoji Mrema.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Jamii (CCJ), Richard Kiyabo, alisema anachokifanya Sheikh Yahya ni kujitafutia riziki na kumuonya kwamba Tanzania haiwezi kuongozwa kwa ramli.

“Anajitafutia riziki kwa njia hiyo, asitulazimishe kumwamini. Anaposema hakuna uchaguzi anahatarisha amani yetu. Taifa linatakiwa limkatae kwa utabiri wake, hili sio taifa la shetani, usalama wa taifa uingilie kati suala hili, mtu anafikia hatua ya kusema nchi itamwaga damu,” alisisitiza Kiyabo.

Source: Tanzania Daima.
 
Back
Top Bottom