Hurricane Watch: Watanzania Texas!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kuna mamia ya Watanzania Dallas na Houston na baadhi yao ni wanachama wa JF. Kama mmesalimika tupeane taarifa!!!
 
Kwa binafsi yangu pamoja na familia yangu tunawaombea salama na Hurricane IKE.......take courage guys......We Love You
 
Ni kweli kwamba huko Texas kuna Watanzania karibu 300 (idadi hiyo haijathibitishwa) na walio wengi wanaishi katika Jiji la Houston na vitongoji vyake.Kuanzia Jana usiku (Jumamosi). Jiji hilo lenye wakazi wanaokadiriwa kufikia millioni 5 limekumbwa na kimbunga "IKe" ambacho kimesababisha Uharibifu wa majengo na miundo mbinu mingine.Kwa mujibu wa habari za CNN inakadiriwa wakazi karibu 3 millioni wa Jiji hilo hawana huduma ya Umeme.Kimbunga Ike siku ya Jumatano kimeua watu 100 huko Carribean haswa katika Visiwa vya Haiti.

Serikali ya Jimbo la Texas ilitoa Tahadhari toka Jumatano jioni,na Wakazi wa Jiji hilo na Miji ya Galveston,Baytown na Kemah waliondoka na kwenda kwenye maeneo ya mbali na yaliyo uwanda wa Juu kama Austin na Dallas ili kukwepa janga hilo.Mji wa Pwani wa Galveston umejaa maji (4feet).Mpaka sasa kuna Taarifa ya Vifo vya watu 4.Hata hivyo kimbunga Ike kimetua na nguvu ndogo kuliko ilivyotabiriwa,kimetua Houston kama storm 2.Hivi sasa Kimbunga kimepungua nguvu na kinaelekea Magharibi ya Jimbo la Arkansas.Kutokana na Kimbunga Ike kunatabiriwa mvua nyingi katika Majimbo ya Louisiana,Arkansas,Missouri,Indiana,Ohio na Michigan kwa siku za Jumamosi usiku na Jumapili.

Bado hakuna habari za Mtanzania yeyote kukumbwa na Janga hilo,Ni wazi kwamba tutapata taarifa kama kuna mwenzetu yeyote amekumbwa na Janga hili.Serikali ya Jimbo na ile ya Shirikisho wanatathmini hasara iliyosababishwa na Kimbunga Ike.
 
Bado hakuna habari za Mtanzania yeyote kukumbwa na Janga hilo,Ni wazi kwamba tutapata taarifa kama kuna mwenzetu yeyote amekumbwa na Janga hili.Serikali ya Jimbo na ile ya Shirikisho wanatathmini hasara iliyosababishwa na Kimbunga Ike.

Hilo Ni Muhimu!
Lakini hata kama waTZ watakuwa hawajapoteza maisha ninaaamini mumepata usumbufu mkubwa sana kutoka na hili kwa hiyo nachukua nafasi hii kuwapa pole wale wate walioathirika kwa namna moja au nyingine, pole hizi ziwaendee wakazi wote wa Texas hata wasio wamarekani WaTz namaanisha wasio kuwa wabongo!
 
Back
Top Bottom