taffu69
JF-Expert Member
- Feb 26, 2007
- 2,094
- 538
Kwa mtizamo wa haraka, mauaji ya vijana hawa yangetokea leo isingeundwa tumeya rais wala kusikia tamko lolote kutoka kinywani mwake na akina Zombe na wenzake wangepewa pongezi nyingi mno kutoka kwa watawala wetu. Kuundwa kwa Tume ya Mhe Kipenka na kukamatwa kwa akina Zombe ilitokana na upya/ugeni wa madaraka/ofisi kwa watawala waliokuwepo wakati huo kuanzia Rais na wale wa chini yake. Kwa siku za karibuni mauaji mengi ya kiholela yamefanywa na askari ama raia lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Mauaji ya albino, polisi walioua Tunduma, Arusha Dar (Kimara) Kyela na kwingineko ni mifano michache ya matukio ya kutisha ambayo yanatokea ndani ya utawala wa sasa pasipo hatua zozote kuchukuliwa.
Mungu zirehemu roho za wale wote waliofikwa na mauti kwa njia hii ya kishetani na mkono wa Mungu uwaelemee wahusika wote popote pale walipo.
Mungu zirehemu roho za wale wote waliofikwa na mauti kwa njia hii ya kishetani na mkono wa Mungu uwaelemee wahusika wote popote pale walipo.