Hukumu ya Mgombea Binafsi Juni 17, 2010

Rev. Mtikila ameiambia BBC kwamba usiku kucha leo hakulala kwa kutofahamu ni hatua gani atachukua endapo hukumu ya Mahakama ya rufaa itamwangusha. Mimi namshauri tu kwamba wakati wa kuwa na mgombea binafsi hasa kwenye ngazi ya URAIS bado. Aachane kwa sasa na mradi huu ambao nia yake ni nzuri tu kwa hapo baadae. Kwa sasa hatuna chaguzi huru, hatuna tume huru ya uchaguzi, miundombinu ya uchaguzi bado ni duni sana, elimu ya uraia ni ya kiwango cha chini sana kwa wapiga kura wetu, umasikini wa watu wetu unatisha, vyombo vya dola bado ni vya chama kilekile,.....
Tuna mengi ya kushughulikia kwa sasa kabla ya hili la mgombea huru.

Mkuu ninakubaliana na hoja zako kwamba kuna mambo mengi sana ya kutatua, lakini kila kitu kina mwanzo wake. Tukisema tukae tusubiri serikali ya CCM ifanye kazi hiyo, hawawezi maana mazingira yaliyopo yanawapa nafasi ya kushinda kirahisi kwenye chaguzi. Iwapo tutafanikiwa kubadilisha kitu kimoja kimoja, tutafika mahali pazuri. Mtoto huwa haanzi kwa kukimbia, lazima atambae, asimame then anapiga hatua moja na kudondoka na finally anaweza kutembea na kukimbia.

Ninakubaliana na idea yako kuhusu nafasi ya mgombea urais kutogombewa na wagombea binafsi, lakini kwenye Ubunge sioni ubaya wake. Vyama vya siasa vimekuwa vikiminya demokrasia kwenye nominations, na hasa CCM. Ndio maana final list huwa inatolewa two or three days kabla Tume ya Uchaguzi (NEC) haijafunga kupokea fomu za wagombea. CCM wanafanya hivyo ili mtu akinyimwa haki asiweze kukatiza kwenda chama kingine, lakini kama kuna opportunity ya mgombea binafsi ni rahisi kuamua kujaza fomu na kuzipeleka NEC as independent candidate.

Kwa hayo yanayofanywa na CCM ni kuwabana na kuwaondoa diplomatically wale wote ambao wanaweza kuonekana wanakwenda against maslahi ya chama. Subiri nominations za mwaka huu ndio watu wataelewa kwanini serikali imekuwa ikipiga dana dana swala la mgombea binafsi, maana muathirika mkubwa ni CCM na ndio maana wanakwepa sana swala hilo.
 
If this is the case, tuna mengi pia ya kushughulikia kabla hata ya kuanza kujadili demokrasia katika jamii yetu!

Mchakato wa kuchagua na kuchaguliwa kwa maoni yangu kwa sasa katika NCHI yetu kipaumbele sio mgombea huru. Hatuwezi kurukia huko wakati mambo ya msingi kabisa hayajakaa sawa na wala hatuna utaratibu mzuri wa kuwaweka wazi wagombea. Ipo siku mtamkabidhi kichaa nchi hii!
 
Rev. Mtikila ameiambia BBC kwamba usiku kucha leo hakulala kwa kutofahamu ni hatua gani atachukua endapo hukumu ya Mahakama ya rufaa itamwangusha. Mimi namshauri tu kwamba wakati wa kuwa na mgombea binafsi hasa kwenye ngazi ya URAIS bado.


yaani haki ya mwananchi raia ipo kwa wakati fulani tu na wakati fulani isiwepo? Haki ya kugombea nafasi yoyote ni haki ya msingi ya kila Mtanzania, hatuwezi kuifuta haki fulani kwa sababu ati hatuna miundo mbinu fulani au hatuipendi.
 
Mchakato wa kuchagua na kuchaguliwa kwa maoni yangu kwa sasa katika NCHI yetu kipaumbele sio mgombea huru. Hatuwezi kurukia huko wakati mambo ya msingi kabisa hayajakaa sawa na wala hatuna utaratibu mzuri wa kuwaweka wazi wagombea. Ipo siku mtamkabidhi kichaa nchi hii!


ina maana walipo madarakani sasa ni timamu? tulimkataa "kichaa" Mrema tukampata "timamu" Mkapa na matokeo yake?
 
yaani haki ya mwananchi raia ipo kwa wakati fulani tu na wakati fulani isiwepo? Haki ya kugombea nafasi yoyote ni haki ya msingi ya kila Mtanzania, hatuwezi kuifuta haki fulani kwa sababu ati hatuna miundo mbinu fulani au hatuipendi.

Hakuna aliyenyimwa kugombea. Utaratibu wetu wa sasa mtu anagombea kupitia vyama. Hivi kweli kama unafaa na watu wanakuona kweli utawafaa, ni lazima uwe mgombea huru? Kwa sasa tuwe wagombea huru kwenye kutafuta wachumba bwana, sio uongozi wa NCHI! Haki tunayoitaka kwa sasa hasa kwenye ngazi ya Urais itatupeleka kubaya.
 
Ipo siku mtamkabidhi kichaa nchi hii!

Katiba (ibara ya 46A) yetu imekaa vizuri sana kwenye hili. Bunge linaweza kumshitaki na kumuondoa madarakani Rais!

Kwa hiyo ukitizama kwa makini utaona kuwa kutokuwepo mgombea huru ndio kunapelekea kuwapa nchi hii 'vichaa' na hata tunashindwa kutumia Katiba kuwaondoa kwa sababu ya 'nidhamu ya chama'.
 
Hakuna aliyenyimwa kugombea. Utaratibu wetu wa sasa mtu anagombea kupitia vyama. Hivi kweli kama unafaa na watu wanakuona kweli utawafaa, ni lazima uwe mgombea huru?


Kama unafaa na watu wanakuona unafaa kwanini watu wasikuchague tu hadi ulazimishwe kujiunga na chama?

Kwa sasa tuwe wagombea huru kwenye kutafuta wachumba bwana, sio uongozi wa NCHI! Haki tunayoitaka kwa sasa hasa kwenye ngazi ya Urais itatupeleka kubaya.

yaani, hawa walio katika Urais sasa hivi wametupeleka/wanatupeleka pazuri? sidhani kama kuna pabaya pa kwenda ambapo hatuwezi kwenda na hawa wanaotokana na chama kimoja cha siasa.
 
Hakuna aliyenyimwa kugombea. Utaratibu wetu wa sasa mtu anagombea kupitia vyama. Hivi kweli kama unafaa na watu wanakuona kweli utawafaa, ni lazima uwe mgombea huru? Kwa sasa tuwe wagombea huru kwenye kutafuta wachumba bwana, sio uongozi wa NCHI! Haki tunayoitaka kwa sasa hasa kwenye ngazi ya Urais itatupeleka kubaya.

Ebu angalia CCJ wanataka kushiriki uchaguzi kupitia vyama, unaweza kujifunza lolote Mkuu kupitia uzoefu wa zengwe wanalopigwa CCJ?
 
Kama unafaa na watu wanakuona unafaa kwanini watu wasikuchague tu hadi ulazimishwe kujiunga na chama?

Kwenye Chama utakutana na watu, utafanyakazi na watu, watu watapata muda kukufahamu kwa karibu zaizaidi ingawa si kwa yote.


yaani, hawa walio katika Urais sasa hivi wametupeleka/wanatupeleka pazuri? sidhani kama kuna pabaya pa kwenda ambapo hatuwezi kwenda na hawa wanaotokana na chama kimoja cha siasa.

Hatuko pazuri sana ingawa kama Watanzania tuko pamoja. Wamefanya yale walioweza kufanya kwa upeo na uwezo wao.
 
I predict mahakama ya Rufaa will blast your government in words that will remain in infamy!

Nadhani umeisikia hukumu iliyotolewa na mahakama kuu juu ya mgombea binafsi. Kwa mara nyingine tena Mahakama imeonyesha jinsi isivyokuwa na uhuru katika maamuzi yake mbali mbali ambayo yanahusu Serikali. CCM wataendelea kupeta kwa miaka mingi ijayo huku nchi ikizidi kudidimia kimaendeleo.
 
Duh Kwa hiyo hata Jaji Mkuu Augustino Ramadhani tegemeo la wengi katutosa kuna mtu ana nakala ya hukumu ili tuone waliegemea wapi ,au wamependekeza nini katika hilo
 
Mchakato wa kuchagua na kuchaguliwa kwa maoni yangu kwa sasa katika NCHI yetu kipaumbele sio mgombea huru. Hatuwezi kurukia huko wakati mambo ya msingi kabisa hayajakaa sawa na wala hatuna utaratibu mzuri wa kuwaweka wazi wagombea. Ipo siku mtamkabidhi kichaa nchi hii!
Tumkabidhi nchi kichaa mara ngapi mkuu, mbona tuna kichaa tayari.
 
  • Watanzania tunataka mgombea binafsi


Thursday, 17 June 2010 08:52

Sadick Mtulya
Mwananchi

MPANGO wa kujipima kwa kutumia vigezo vya utawala bora Tanzania (APRM) unatarajia kuwasilisha rasimu ya ripoti kwa viongozi wakuu wa Bara la Afrika inayoonyesha kuwa Watanzania wengi wanataka mgombea binafsi.


Ripoti hiyo yenye kurasa 600 imesema, kutotekelezwa kwa uamuzi wa kuruhusu mgombea binafsi, kunanyima haki ya msingi ya mtu kuchagua na kuchaguliwa.


Mratibu wa Tathmini ya Utawala bora wa APRM Tanzania, Severinus Hyera alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa rasimu ya ripoti hiyo inatokana na utafiti uliofanyika kwa miaka mitatu, tangu mwaka 2007 hadi 2009.


"Katika utafiti huo uliofanywa na wataalamu kupitia maktaba, mtandao na mahojiano kati ya wananchi wa kawaida katika ngazi ya kaya na wasomi wa kada zote,
watanzania wengi wanataka kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi," alisema mratibu huyo.


Mratibu alizungumza hayo katika semina kati ya APRM na taasisi za kiraia kutoa mapendekezo ya rasimu hiyo kabla ripoti hiyo haijakabidhiwa katika mkutano wa viongozi wa nchi za umoja wa Afrika.


Alisema wataalamu 110 wa masuala ya utawala bora wenye umri kuanzia miaka 26 walihojiwa katika utafiti huo. Kati yao watu watatu walihojiwa kutoka mikoa 25 ya Tanzania Bara na Zanzibar na watu 35 walihojiwa katika semina maalumu jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa mratibu huyo, mbali na watalaamu hao wengine waliohojiwa katika utafiti huo walitoka katika wilaya mbili za kila mkoa pamoja na vijiji, mitaa, shehia mbili zilizowakilishwa kwa uwiano sawa wa jinsia.


Huu ni utafiti wa pili unaounga mkono suala la mgombea binafsi nchini baada ya jana katika utafiti wake kampuni ya Synovate kuonyesha asilimia 48 ya watu 2000 waliohojiwa, wanataka mgombea binafsi.




Kwa mujibu wa utafiti huo wa Synovate, wakati asilimia hiyo 48 ikiunga mkono mgombea binafsi, asilimia 25 ya watu waliohojiwa wamekataa mfumo huo na asilimia 27 walisema hawana jibu ya swali hilo.


Tafiti hizo zimetolewa huku leo Mahakama ya Rufaa ikitarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya mgombea binafsi katika rufaa iliyokatwa na serikali kupinga huku ya mahakama kuu.


Mei 5 mwaka 2006 Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa hukumu kuruhusu mgombea binafsi katika kesi iliyofunguliwa na Mchungaji Christopher Mtikila lakini, serikali ilikata rufaa kupinga hukumu hiyo.


Mtikila alifungua kesi hiyo Februari 17, 2005 akiiomba Mahakama Kuu pamoja na mambo mengine, iamuru kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi za Tanzania.


Hukumu ya Mei 5 mwaka 2006 iliyoruhusu mgombea binafsi ilitolewa na jopo la majaji watatu wa mahakama Kuu Dar es Salaam; Jaji Kiongozi Mstaafu Amir Manento, Salum Massati (aliyekuwa Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa) na Jaji Thomas Mihayo (mstaafu kwa sasa).




Katika kupinga hukumu hiyo serikali ilitoa sababu kadhaa ikiwamo Mahakama Kuu kukosea kisheria kutamka vifungu vya katiba kwa kuwa mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kisheria kusikiliza na kutoa maamuzi katika shauri hilo.


Ilieleza kuwa suala hilo lilikuwa linahusu Katiba na mahakama hiyo haikuwa na uwezo huo na kwamba, hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kutengua Katiba ya Jamhuri au kifungu chochote cha katiba hiyo kwa kuwa ndio msingi na kipimo cha sheria nyingine zote.



 
Wanabodi, hukumu kuhusu kesi ya kikatiba kuruhusu wagombea binafsi uchaguzi mkuu wa mwaka huu, itatolewa na Mahakama Kuu ya Rufani ya Tanzania, siku ya Alhamisi ya kesho kutwa siku.

Swali ni jee hukumu hiyo, italeta kicheko kwa kuruhusu demokrasia ya kweli kwenye chaguzi zetu, au ni kuendeleza kilio cha uminywaji demokrasia kama hali ilivyo sasa?, haswa kwa kuzingatia, maandalizi ya uchaguzi kupitia vyama ndio hayo yamefikia top gear na bunge ambalo ndilo linatarajiwa kufuta vifungu husika na kupitisha sheria mpya ndilio hilo hilo limetengua kanuni zake zenyewe ili kuwa Bunge Haste Haste kuwahi mchakato wa uchaguzi?.

Jee Jaji Mkuu, Agustino Ramadhani, with his Full Bench (Majaji Rufani 7!) kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, atafanya kile akipasacho kufanya na jina lake kuandikwa katika vitabu vya historia ya nchi hii?,

ama naye atajiunga na ule msururu wa wapiga zumari, kutupigia nyimbo zile zile zilizoshachaguliwa na aliyemlipa mpiga zumari huyo kwa mujibu wa ule msemo maarufu wa
"He who pays the piper, may call the tune".

Huku tukiisubiria hiyo alhamisi, hakuna ubaya tuiijadili hukumu hiyo tarajiwa kwa mustakabali wa taifa letu.
Pasco
Leo nilikuwa napitapita tuu humu jf, ndio nikakutana na bandiko hili ambalo nililianzisha mimi, but to my surprise, I didn't know what happened to me, hiyo June 17, sikurudi kumalizia bandiko hili kwa kuleta mrejesho, na wakati nikiandika haya, I was just a lay man, lakini leo ninapoukumbuka uzi huu, mimi sasa ni wakili, ila sio wakili msomi bali ni wakili Mtangazaji, na tangu nimekuwa wakili, bado sija practice, kwasababu nilikuwa sijafikia uamuzi wa my area of specializations, sasa nimepata!. Soon naingia kazini ili tuwatendee haki Watanzania.

Mungu nisaidie!.
P.
 
Kuwepo kwa mgombea binafsi ni faida kubwa kwa siasa za nchi yetu, tatizo watu wengi wanaliangalia kwa nafasi ya urais zaidi. Faida ninayoiona mimi ni kupanua wigowa demokrasia kwa wanasiasa wetu. Tunakumbuka wote yaliyowakuta wabunge 43 wa CCM wakiongozwa na Thomas Nyimbo, walisimama kidete kuihami NBC na TANESCO dhidi ya makaburu,lakini mwanyekiti wao wa chama wakati huo Benjamin Mkapa aliwasambaratisha kwa kuwatishia kuwanyanganya kadi za ccm nao wakanywea, laiti kingekuwepo kipengele cha mgombea binafsi wangeweza kusimama veme katika nafasi zao za kuwakilisha wapiga kura wao badala ya kutumiwa ka muhuri kulita chama cha na serekali yake.Kuwepo mgombea binafsi ni ukombozi kwa watanzania kuweza kupata uwakilishi sahihi na kupata wabunge wanaoweza kulitetea Taifa dhidi ya watawala mafisadi kama waliopo madarakani hivi sasa.
Mkuu SAGAI GALGANO, kumbe na wewe umetoka mbali!. Hata lile jambo langu, naamini hili lingekuwepo, ningesimama mimi kama mimi na kuwaeleza waheshimiwa Wabunge wa Bunge la JMT agenda zangu, amini nakuambia, ningepita!.

Hili la kakikundi fulani ka watu, kuamua haki za Watanzania, must end and must stop kwa kustopishwa!.
P
 
Back
Top Bottom