Hukumu ya Mahalu yayeyuka!!!

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,724
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilishindwa kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Euro milioni mbili, inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin, kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kuwa na majukumu mengi.
Hakimu Mkazi Alocye Katemana, alisema kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya kutolewa hukumu na Hakimu Mfawidhi Ilvin Mugeta, lakini hakimu huyo alimweleza kuwa na majukumu mengine ya kimahakama, hivyo asingeweza kuisoma hukumu hiyo jana.
Hakimu Katemana alisema kwa sababu hiyo, Hakimu Mugeta amemweleza kuwa aihairishe kesi hiyo hadi Agosti 9, mwaka huu, itakapokuja kwa ajili ya kusoma hukumu.
Januari 22 mwaka 2007 kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Ben Lincoln, Ponsia Lukosi na Vicent Haule wakidai kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa sita.
Makosa hayo ni kula njama, wizi wa Euro milioni mbili, kughushi vocha za manunuzi ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, kutumia risiti za manunuzi ya jengo hilo kuidanganya serikali na kuisababishia hasara ya Euro milioni mbili.
Ili kuithibisha kesi yao, upande wa Jamhuri ulileta jumla ya mashahidi saba na upande wa utetezi ulileta mashahidi watatu ambao ni Mahalu, Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Grace Martin.

Source: Tanzania Daima
 
kwahiyo kutoa hukumu siyo sehemu ya kazi za mahakama ?? kaendesha kesi kwa miaka 5 sasa ghafla hana muda wa kusoma hukumu?? kwanini mnawadanganya watu kwanini msiwaambie ukweli kuwa jalada la hukumu linapitiwa na ikulu
 
Teh teh teh!, mtoa hukumu ana majukumu mengine!, kwenye kutoa hukumu kwenye kesi za wizi wa mabati, wana majukumu mengine, na hata kwenye kesi kubwa zinazohusisha maslahi ya Taifa, hawa ni waseng***
 
Back
Top Bottom