Hukumu Ya Kifo Kwa Kuwaua Wakristo Misri

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Hukumu Ya Kifo Kwa Kuwaua Wakristo Misri



1.Mohammed Ahmed Hussein, mshtakiwa
2.Maandamano ya wakristo baada ya shambulio la Alexandria


Mahakama ya usalama ya taifa nchini Misri imehukumu kifo muumini mmoja wa Kiislamu kwa kosa la kuua Wakristo sita wa madhehebu ya Copti na polisi mmoja mwaka uliopita.
Mohamed Ahmed Hussein ni mmoja wa watuhumiwa wanaoshtakiwa kuwafyatulia risasi waumini walipokuwa wakiondoka kwenye misa ya mkesha wa Krismasi, katika mji wa Naga Hamady kusini mwa Misri.

Watu wengine wawili wanaohusishwa na mauaji hayo watahukumiwa baadae.

Watu hao walikamatwa mara baada ya shambulio hilo, lakini kesi yao imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara.

Hukumu hiyo imetolewa wiki mbili tu baada ya shambulio la bomu la kujitoa mhanga nje ya kanisa la Copti katika mji wa Alexandria lililouwa watu 23.

Kesi hiyo imeleta chuki miongoni mwa jamii ya Wakristo wa Copti kwa sababu imechukua muda kumshitaki mtuhumiwa huyo ambaye anadhaniwa kuwa na uhusiano na mbunge wa chama tawala.

Hukumu hiyo ya kifo imetolewa wakati kuna wasiwasi mwingi kati ya jamii ya waislamu na wakristo nchini humo.

Mahakama ya usalama ya taifa huko Misri imetoa hukumu ya kifo kwa muumin wa kiislamu kwa kosa la kuua wakristo sita wa madhehebu ya Copti na polisi mmoja mwaka uliopita.
BBC Swahili.
 
Hapo haki imetendeka,lakini kwa nini waislamu wanakua wakorofi sana,sasa watu wapo kwenye mkesha wa x mas unawavamia na kua baadhi yao hivi ni nini kinacho wasumbua hao ndugu zetu?wanakerwa nini kutoka kwa wakristo?
 
Hapo haki imetendeka,lakini kwa nini waislamu wanakua wakorofi sana,sasa watu wapo kwenye mkesha wa x mas unawavamia na kua baadhi yao hivi ni nini kinacho wasumbua hao ndugu zetu?wanakerwa nini kutoka kwa wakristo?

Tafadhali usi-generalize! kuna wanaoua waIslaam zaidi ya wakristo hivi sasa duniani? Tazama Iraq na Afghanistan! au huyaoni? na hii hapa mpya kabisa:

Three killed in voter listing in Nigeria's Jos
(AFP) – 15 hours ago
JOS, Nigeria - A Christian mob razed a mosque and hacked an electoral worker to death Monday as it barred Muslim organisers of April's polls from a registration exercise in Nigeria's Jos region, police said.


soma zaidi: AFP: Three killed in voter listing in Nigeria's Jos
 
Back
Top Bottom