Hukumu ya kesi ya uchaguzi Igunga

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Wana JF ninapatwa na kigugumizi, hukumu ya kesi ya uchaguzi IGUNGA iliyopangwa tarehe 20 August 2012, mbona tarehe hiyo itakuwa siku ya IDD? au vipi mimi nilinukuu visivyo? Anayeelewa anijuze na mimi, ninachofahamu waziri Magufuri aliingia mitini kutowa ushahidi.
 
Mwezi umeshaanza kuchungulia kwa mbali, kuna uwezekano tukafuturu tarehe 18/19
 
Kisheria,kama siku iliyopangwa inaangukia siku ya mwisho wa juma au sikukuu,shauri litakuwa siku ya kazi inayofuata.Kwahiyo,kama tar 20 itakuwa sikukuu,hukumu itasomwa tar 21.Nadhani umenielewa Mkuu.
 
wanaweza wakaitisha uchaguzi mwengine hawa.

Mkweree amewaambia kuwa hukumu lazima ccm ishinde kwani serikali imefirisika!! Hakuna by- election Igunga; hukumu itakuwa kama ya Segerea, mark my words!!
 
Kisheria,kama siku iliyopangwa inaangukia siku ya mwisho wa juma au sikukuu,shauri litakuwa siku ya kazi inayofuata.Kwahiyo,kama tar 20 itakuwa sikukuu,hukumu itasomwa tar 21.Nadhani umenielewa Mkuu.

sheria namba ngapi ya mwaka gani inayoainisha huu utaratibu mkuu mm ni mdau wa sheria sana
 
wanaweza wakaitisha uchaguzi mwengine hawa.

Hasa ukizingatia kuwa magufuli aliahidi rushwa ya kujenga Daraja la Mbutu na kweli mpaka leo hii kaishia kupeleka Lori mbili za Mawe tu na hataki kugusa mahakamani basi uchaguzi mwingine huoooooo, na safari hii pamba yao wameishusha bei toka Tsh 1000 mpaka Tsh 600/= nafikiri patakuwa patamu zaidi ya uchaguzi uliopita
 

Attachments

  • Photo0030.jpg
    Photo0030.jpg
    210.1 KB · Views: 104
  • Photo0028.jpg
    Photo0028.jpg
    156.9 KB · Views: 88
Hiyo kesi majibu yanajulikana Serikali na mahakama ni maswahiba na mahakama imekuwa ikitii maelekezo yote yawe sahihi au batili kutoka serikalini! rejea kessi ya Arusha mjini, rejea kesi ya Segerea, rejea mgogoro wa madaktari na serikali, rejea recently mgogoro wa walimu na serikali ni wazi mahakama sasa ipo biased haiwezi kutoa haki tena!!bila kuwepo katiba mpya na uhuru wa mahakama hakuna haki!!
 
wadau tunaomba taarifa ya hukumu ya ubunge wa igunga coz tulisikia ni leo tar. 20 mwez wa 8, tunaomba taarifa.
 
Kafumu ameachwa afurahie idd kisha wamtumbulie nyongo!!!!
 
mkuu ngasibaro kwenye hiyo picha kama mawe yaliyopelekwa hapo ni hayo tu hilo daraja litakamilika karne ijayo.
 
Back
Top Bottom