Hukumu ya kesi ya maandamano ya January 5 ya CHADEMA leo

Rejao,
Sahihisho kidogo shule za kata ada zake kwa mwaka ni 1500 kwa mwaka..

Kwa wanafunzi 417 ni kiasi cha 625.500..

Hii ndio kazi ya kujivunia ya Lema akiwa mbunge!
elimu wanayoipata ni ghali sana kulipa pesa hiyo uliyoitaja hapo!
 
Rejao,
unajua watu wengine pumba...Zimbwbwe Mkate mmoja unauzwa $ 10 Million apo sijuhi atasemaje
Acha uongo wewe, $10million ni kama TZS 16billion, jifunze kutofautisha na kama hujui bora kukaa kimya, Zimbabwe wanatumia ZWD au Zimbabwe Dollar ambayo inabadilishwa kwa ZWD 379 kwa $1 Kumbuka hapa ni TZS 1620 kwa $1, pamoja na misukosuko waliyopitia lakini wamepandisha thamani ya pesa yao sasa imetupita mara 3, yote hiyo kwasababu ya serikali ya ccm (unayoitetea) isiyojua chanzo cha umaskini wa mtanzania, maana kama wangejua wangetatua!
 
Rejao na Rtz, mna bahati sana nimechelewa kuingia kwenye hii thread toka page ya kwanza. Ningewashughulikia mpaka mngekimbia humu JF.
 
Vipi Lema kafikia wapi zile Machinga Complex mbili na barabara za juu?
tuanze na hizi kwanza
Ahadi za Kikwete: 2010 - 2015
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora

  1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  42. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
 
Tumethubutu, tumeweza na tunaendelea kusonga mbele....

dilapidated-school.jpg
800px-we_rule_the_school.jpg
 
Jamaa kasema kweli,hizo kesi niza Lema,ahangaike nazo mwenyewe na famila yake. Zisiwe kero kwa Watanzania wengine.

Nikiisoma thread hii namkumbuka sana mwalimu wangu akiitwa Ganka, alikua hapendi kabisa mtu uandike etc.. Maana ni end of thinking capacity na alitaka watu tutumie akili zaidi kufikiri.

Sitaki kuamini kama hii ndio ETC yako.

ITS TOO LOW FOR GREAT THINKER
 
Acha uongo wewe, $10million ni kama TZS 16billion, jifunze kutofautisha na kama hujui bora kukaa kimya, Zimbabwe wanatumia ZWD au Zimbabwe Dollar ambayo inabadilishwa kwa ZWD 379 kwa $1 Kumbuka hapa ni TZS 1620 kwa $1, pamoja na misukosuko waliyopitia lakini wamepandisha thamani ya pesa yao sasa imetupita mara 3, yote hiyo kwasababu ya serikali ya ccm (unayoitetea) isiyojua chanzo cha umaskini wa mtanzania, maana kama wangejua wangetatua!

Wewe kweli pumba unatakiwa uanze kusoma mwanzo wa thread ndio utajua kwa nini nimeandika hivyo...

Hizo habari za exchange rates za Zimbambwe hazina uhusiano na thread..unajua kama tulikuwa tunaongelea habari za 2005? Saruji ilikuwa inauzwa Sh 800 Namibia kwa mujibu wa Magwanda wenzako!
 
Wewe kweli pumba unatakiwa uanze kusoma mwanzo wa thread ndio utajua kwa nini nimeandika hivyo...

Hizo habari za exchange rates za Zimbambwe hazina uhusiano na thread..unajua kama tulikuwa tunaongelea habari za 2005? Saruji ilikuwa inauzwa Sh 800 Namibia kwa mujibu wa Magwanda wenzako!

Matitizo ya elimu za kukariri ndiyo hayo!! Wenzako wanapongelea Global wewe unaongelea earth!! Nyie watoto wa mafisadi mna matatizo sana!!!


 
Nikiisoma thread hii namkumbuka sana mwalimu wangu akiitwa Ganka, alikua hapendi kabisa mtu uandike etc.. Maana ni end of thinking capacity na alitaka watu tutumie akili zaidi kufikiri.

Sitaki kuamini kama hii ndio ETC yako.

ITS TOO LOW FOR GREAT THINKER
kweli wewe ni katika walio bahatika, ulikwenda shule? hongera
 
Haiwezekani ukawa ni mtanzania. Hii ni chuki ya mtu anaechukia watanzania wote. Kwa kifupi Wewe ni Adui wa nchi...




Rejao,
Sahihisho kidogo shule za kata ada zake kwa mwaka ni 1500 kwa mwaka..

Kwa wanafunzi 417 ni kiasi cha 625.500..

Hii ndio kazi ya kujivunia ya Lema akiwa mbunge!
 
Back
Top Bottom