Hukumu ya KESI inayomkabili John Mnyika (jimbo la Ubungo, submission leo)

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Tiyari tumekwisha kufika mahakani watu ni wengi mno wa vyama vyote viwili yani ccm na chadema. Ulinzi upo kila kona ya mahakama jaji bado hajawasili. Endelea kuwa nimi kila kitu ukipate.

Updates toka chumba cha mahakama hukumu imeahirishwa nafatilia tatizo nini. Stay tunned

John Mnyika


Nasikia adhana, Hayya alas-swalaah; naendelea na mkesha kama wa Loyola kupitia kurasa 111 za mwenendo wa kesi (court proceedings), mpaka sasa nimeandika kurasa 21 za mchango wangu kuhusu majumisho (final submission) kutoka katika rundo la rejea za hukumu mbalimbali zenye misingi muhimu ya kisheria (fundamental legal principles). Nikimaliza kesho namwachia wakili wetu aendelee kwa upande wake, tutakutana mahakamani kesho kutwa tarehe 4 Mei 2012. Tulitafuta kura pamoja, tukapiga kura pamoja, tukazilinda kura pamoja;, kwa pamoja tutaendelea kushinda. AMUA: Maslahi ya Umma Kwanza

Share · Yesterday at 4:18am ·
 
Uvumilivu ni muhimu sana maana kuna watu hujifanya wao ndo majaji wa hz kesi.
 
Tiyari tumekwisha kufika mahakani watu ni wengi mno wa vyama vyote viwili yani ccm na chadema. Ulinzi upo kila kona ya mahakama jaji bado hajawasili. Endelea kuwa nimi kila kitu ukipate.

Ndugu,

Pamoja na kumuombea John John Mnyika, naomba utujue sisi ambao tupo nje ya mahakama
 
Kama hukumu ni ya haki Polisi wa kazi gani? Me nadhani hukumu wanayo polisi! Hili ndo lanalotufanya tusiiamini mahakama yetu maana wanafanya hukumu ionekane kama utabiri wa hali ya hewa ambao unabadilikabadilika kutokana na tabia nchi!
 
Kwa jinsi kesi yenyewe ilivyokwenda,nategemea leo ndio mwisho wa Mnyika.Maana ushahidi wote umeonyesha madudu yaliyofanyika wakati wa kuhesabu kura.CCM tumejiandaa kwa uchaguzi mdogo kwani hatutapoteza tena jimbo la Ubungo.

Mungu wape moyo wa uvumilivu wasiyokubali haki kutendeka wakati wanajua fika makosa yaliyofanyika kupitia Laptops za CDM.Poleni sana.
 
Nilisikia kuwa kesi hii imekaa vibaya kwa Mnyika, sijui kama atapona....
 
Back
Top Bottom