Hukumu ya Chenge na hukumu ya Mallya yule aliehusika na ajali ya Chacha Wangwe

Katiba haisemi kosa la jinai bali kosa lolote lile,

Nanukuu tena

Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Nisaidieni tafsiri ya kifungu hicho.
 
Weledi wa sheria na katiba endeleeni kutujuza thread ya Mwanaukweli inaweza kutupa ufahamu mpana zaidi!
 
Nimeangalia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimekuta haya:

Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Nisaidieni tafsiri ya kifungu hicho.

Kuamua kulipa faini haifuti kuwa amehukumiwa kufungwa kwa zaidi ya miezi sita.

Hapa kunahitaji wanasheria kuja kutupa tafsiri halali ya kifungu hicho
 
Chenge amehukumiwa kuwa mkosa. Adhabu yake ni jela mwaka. pesa ni badala ya kifungo lakini kifungo si badala ya jela.

Hukumu haikusema anatakiwa kulipa pesa na akikosa aende jela! Ubunge na utumishi wa umma umekoma jana kama Rais, Waziri wa sheria na wabunge waliapa kuiheshimu na kuilinda waliapa kwa kumaanisha.

Kama akiendelea na ubunge, mimi namfungulia kesi Rais kwa kutoiheshimu na kuilinda katiba yetu.





Faini na kifungo viko at per ! lakini wanasheria ndio wanacheza hapo, kwani sheria iko kimya kama mtu amelipa faini!
 
Katiba haisemi kosa la jinai bali kosa lolote lile,

Nanukuu tena

Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Nisaidieni tafsiri ya kifungu hicho.


Duh, ngoja tusubiri Warema atasema nini hapa. I hope hatasema mjadara umefungwa!!
 
Kuamua kulipa faini haifuti kuwa amehukumiwa kufungwa kwa zaidi ya miezi sita.

Hapa kunahitaji wanasheria kuja kutupa tafsiri halali ya kifungu hicho

Wanasheria tupeni michango yenu. Tujiandae kwenda kuchukua Jimbo!!!!!!!!!!!
 
Rejea comment yangu mapema, hati ya mashitaka katengeneza mwenyewe, na hukumu. Kuna issues ambazo kwa mtu wa kawaida ungefungwa, kuidanganya mahakama, kughushi hati za bima, kuendesha wakati akiwa bwii, lakini hayakutamkwa hayo maana ukweli saa tisa alfajiri alikua atoka shamba, kwenye mkutano, semina, warsha, nyumba ndogo, disco, rhumba, taarabu,kurauka au kampeni? napata shida kuelewa mwenzenu
 
serikali ya JK kama ilikuwa serious Cheng engekuwa japo selo kwa issue ya RADA. Kama aliweza kuchomoa hiyo ujue kama alivyosema hosea kwenye wikileaks kuna untouchables.

Mimi nilitegemea untouchable wawe marais wastaafu pekee lakini kansa inazidi kuenea. Two years to come hata madiwani nana wakuuwa wilaya watakuwa hawaguswi.

Nimegundua sababu moja na ya muhimu nn watu kukimbilia kwenye siasa ni kuwa na kinga.
 
Kumbuka kwamba hiyo ni traffic offence ina tofauti na kesi zingine za jinai.

Nisahihisheni kuna aina mbili za kesi (i) Kesi za jinai - criminal
(ii) Kesi za madai - civil case.

Trafic case inaangukia kwenye criminal
 
sasa jamani kama sheria ipo mikononi mwa wachache mbona tutanyanganywa kila kitu? naona uhai wa watu uliochukuliwa kwa uzembe wa chenge sasa jamaa yupo mtaani keshalipa kijisenti 700k
 
Kama sheria ndivyo inavyosema basi Chenge inabidi aachie kiti cha ubunge. Kitu ambacho sijaelewa ni kwa nini kosa la kufoji insurance alikuzungumziwa? Badala yake kosa alilikutwa nalo ni kuendesha gari bila ya insurance tuu, what about forging insurance which is a serious offence. Ikukumbukwe ya kuwa kampuni ya insurance ya taifa iligundua ya kuwa insurance ya Chenge ilikuwa feki.
 
Hivi siku ile ya ajali walimpima kama kapiga ulabu?? Kama hawakumpima then hapo ndio alipopiga bao....
 
jaman hivi uhai wa mtu kweli unadhaman ya laki saba kweli,kama ndo hivi mbona maskin sie wa kwa mfuga mbwa tumekwisha,
lakin wana jf mimi kwa ulewa wangu finyu sijaona kiongozi yoyote yule aliyewah kuhukumiwa jamii ikalizka ya wabongo,toka enzi za mandawa,labda huko mbele huenda yale yakina kaunda yakatokea
 
Mallya alihukumiwa miaka mitatu jela bila faini...usione ajabu kuskia kwamba Chenge alishiriki kupanga hukumu ya kesi yake ndo maana alikwenda na hiyo pesaa mahakamani......hiyo ndo Tanzania sheria ni kwa ajili ya maskin cio wenye pesa...painful,Mungu ibariki Tanzania
 
Malipo ni hapa hapa duniani, Ditopile Majiyatanga Mzuri yupo wapi? kifo cha aibu kilimkumba. Labda Chenge atubu na kumrudia muumba vinginevyo duh.
Usichanganye kati ya Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (RIP) na Chrisant Majiyatanga Mzindakaya. Rudi hapa umuombe radhi Dr. Mzindakaya, alifanya kazi kubwa pale Sumbawanga kuhakikisha msimamizi wa uchaguzi anamtangaza mgombea wa CHADEMA kuwa mshindi kama wapiga kura walivyoamua, lakini akazidiwa nguvu na Pinda aliyetumia uwaziri mkuu wake. Ilikuwa kama sinema ya kuigiza kumuona Mzindakaya anatetea haki ya wana CHADEMA, hali iliyosababisha vigogo hao washikane mashati!
 
Wanajamvi,

Kesi ya Chenge ndio imekwisha. Amekutwa na hatia na amehukumiwa hukumu ambayo sipendi kusema chochote hapa.

Ninavyofahamu mimi, mtu aliyewahi kutiwa hatiani na mahakama kwenye makosa ya jinai, anapoteza sifa ya kuwa kiongozi wa nafasi kama ya Ubunge (kama nimekosea nisahihisheni)


Sasa, hatima ya Chenge ni nini? Au kulindana kutaendelea?.

Kaka Magulumangu ulipata kusema unajipanga kwenda Bariadi 2015, please fuatilia hili pengine hautakuwa na sababu ya kusubiri hadi 2015
 
Moderators, mmeunganisha thread mbili. Moja Inalinganisha kesi ya Chenge na ya Malya; nyingine inajadili hatima ya ubunge wa Chenge.

Lakini mwelekeo wa mijadala hii ilikuwa ni tofauti kabisa.

Please zitenganishe tena ili kila thread ijadili ya kwake.

Naona mjadala wa hatima ya Ubunge umemezwa kutokana na kichwa chake kupotea. Kwa maoni yangu ni muhimu sana kuliweka wazi hilo.

Please naomba mtenganishe.
 
Back
Top Bottom