Hukumu Rufaa ya Godbless Lema yaiva

Hapo kwenye red kuna walakini hebu soma hapa chini ushahidi wa Mh. Tundu Lissu (MB) kama ulivyonukuliwa kwenye utetezi wake kwenye kamati haki, maadili na madaraka ya Bunge.

JAJI WA RUFAA MBAROUK SALIM MBAROUK

Mbarouk Salim Mbarouk aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mwaka 2008. Kabla ya uteuzi huo Jaji Mbarouk alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa zimeainishwa katika ibara ya 118(3) ya Katiba:


“Majaji ... wa Rufani watateuliwa na Rais, kwa kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ... zilizoainishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.”


Kwa mujibu wa Ibara ya 94(3) ya Katiba ya Zanzibar, 1984,
“Mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa Jaji wa Mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yoyote ya Jumuiya ya Madola au Mahkama ya Rufaa kutoka Mahkama hizo; au awe Mwanasheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa Jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba.”

Jaji Mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya Katiba ya Zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya Tanzania kama inavyotakiwa na Ibara ya 109(7) ya Katiba.

Jaji huyu ana stashahada ya juu ya sheria (Post Graduate Diploma in Law) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha nchini Uingereza.

Uteuzi wa Jaji Mbarouk kuwa Jaji wa Rufaa ulileta minong’ono mingi katika taaluma ya sheria kiasi kwamba marehemu Wakili Leopold Kalunga anasemekana kufungua shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka uteuzi huo utenguliwe. Hata hivyo, Wakili Kalunga alifariki kabla ya shauri lake kusikilizwa na kwa hiyo liliondolewa mahakamani.

Aidha, monong’ono hiyo ilimfanya Jaji wa Rufaa Mbarouk kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambako bado ni mwanafunzi hadi ninapoandika Addendum hii.
MEMBER
MUMBURYA UMENIFURAHISHA SANA HII NDI JF HAPO NI MEMBER MOD EMBU MPE SN MEMBER TAFADHALI NIRUDISHE MEMBER ...TUNAPENDA WACHAMBUZI KAMA HAWA ....ILA UNAKAA KWA MUDA USIOTE MIZIZ UKAANZA KUTUKANA WALEZI WAKO WAKINA DIDY'S
 
jaji wa rufaa mbarouk salim mbarouk
wakuu huyu bwana lema kama anaweza kuomba hilo jina liisiwepo atakuwa amesaidia..huyo bwana akiongea bwana wake aseme hivi nawaambia ajibu kitu....anyway wanasema kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka sie tulilia naamini wakati huu wa kucheka mungu awatie moyo vijana wetu wa chadema
 
Tunaimani mbunge wetu Lema ataibuka kidedea safari hii pamoja na kuwa baadhi ya majaji hawana sifa!
 
Aiseee baba yangu lema akishinda nyinyiemu itakuwa haina jinsi itabidi 2 wakimbilie mwebwepande
 
Aiseee baba yangu lema akishinda nyinyiemu itakuwa haina jinsi itabidi 2 wakimbilie
webwepande

yeeeeeeewiiiiiii ngoja nipate mbege nikalime
 
Molemo
hapa hamna kitu Lema atulie tu aendeleee na kazi yake ya ujangiri kama zamani na kukwiba magari ya watu Arusha kama alivyotuhumiwa na Zombe kwakuwa wanajuana vizuri..

Ubunge asahau kwa sasa

Mkuu mbona unatoa tuhuma nzito nzito bila ya ushahidi? Jenga hoja mkuu na si ku attack mtu kihivyo, hata kama ni jukwaa huru lakini tunajadili issues!
 
Baada ya kuvuliwa nguo na report ya Tundu Lissu nina wasiwasi Mbarouk Salim Mbarouk anaweza kuleta PERSONAL VENDATTA dhidi ya CDM (read Lema).

GOD BLESS LEMA
 
Duh, ila lile liutetezi wa Lisu ulikuwa wakati muafakaaaaaaa, sasa ndoja tusubiri
 
Jaji wa mahakama ya rufaa kutoka znz anayedaiwa hana degree ya sheria ya chuo kikuu kwa mujibu wa masharti ya kanuni za uteuzi wa majaji nchini amepangwa kuwa kati ya majaji watatu wa mahakama ya rufaa Tanzania kusikiliza rufaa ya Mhe. Godbless Lema anayepinga kutenguliwa ubunge wake na mahakama kuu ya Tanzania.Rufaa hiyo iliyopangwa kusikilizwa na majaji watatu akiwemo MBARUOK Mbarouk itatajwa 20/09/2012.Nafasi ya jaji huyo kihiyo kwa mujibu wa kanuni na sheria za mahakama hataweza kusababisha mtafaruku wa kisheria kama ataendelea kuwa kwenye jopo ilo pindi hukumu itatolewa kwa wakata na wapinga rufani?.
 
Jaji wa mahakama ya rufaa kutoka znz anayedaiwa hana degree ya sheria ya chuo kikuu kwa mujibu wa masharti ya kanuni za uteuzi wa majaji nchini amepangwa kuwa kati ya majaji watatu wa mahakama ya rufaa Tanzania kusikiliza rufaa ya Mhe. Godbless Lema anayepinga kutenguliwa ubunge wake na mahakama kuu ya Tanzania.Rufaa hiyo iliyopangwa kusikilizwa na majaji watatu akiwemo MBARUOK Mbarouk itatajwa 20/09/2012.Nafasi ya jaji huyo kihiyo kwa mujibu wa kanuni na sheria za mahakama hataweza kusababisha mtafaruku wa kisheria kama ataendelea kuwa kwenye jopo ilo pindi hukumu itatolewa kwa wakata na wapinga rufani?.

huyu MBAROUK MBAROUK ndiye yule anayetajwa kwenye ripoti ya utetezi wa Tundu Lissu??????
can somebody do something
 
Haya ndio matatizo ya kuingiza siasa kwenye taaluma za watu!!!
Tatizo DHAIFU mda mwingi yupo nje kuhemea lini atapata mda wa kusoma ripoti?mda mwingi anakuwa kachoka na usanii ndio unaanzia hapo.
 
Back
Top Bottom