Hukumu dhidi ya Mbunge Novemba 9

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Hukumu dhidi ya Mbunge Novemba 9
Send to a friend
Wednesday, 26 October 2011 07:30
Brandy Nelson, Mbeya
HUKUMU ya kesi ya kutishia kuua kwa maneno inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Mbarali kupitia CCM, Modestus Kirufi inatarajiwa kutolewa Novemba 9, mwaka huu.

Tarehe ya hukumu hiyo Ilitamkwa jana baada ya mbunge huyo kutoa utetezi wake ulioanza saa 3.00 Asubuhi hadi saa 6.00 mchana mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite.

Akitoa utetezi wake mbele ya mahakama hiyo, mbunge huyo alisema kuwa tuhuma dhidi yake hazina ukweli wowote, bali ni njama za kutaka kumkandamiza kisiasa.

“Tuhuma hizi ni za uongo naomba mahakama iamini hivyo, kwani hili ni jaribio la pili la kutaka kuniondoa madarakani, la kwanza lilikuwa la Kutaka kuninyang`anya kadi ya CCM baada ya kukosa udhibitisho walishindwa na ndiyo maana wameamua kutumia njia hii ili kuniangamiza,” alisema

Alisema kuwa anaamini njama hizo zinafanywa kutokana na kuwa yeye siyo chaguo la baadhi ya viongozi wa CCM wilaya na wao walikuwa na chaguo lao na hivyo ni njama za kisiasa kwani hakuna hoja ya msingi ndiyo maana wanatafuta njia ya kumuondoa madarakani .

Awali katika utetezi huo, Wakili wa mshitakiwa Eckson Mbogolo alitoa nyaraka ya maelezo ya mlalamikaji aliyoyatoa polisi na kumuomba hakimu kupokea kama moja ya vielelezo vya ushahidi wa utetezi wa mshtakiwa nyaraka ambayo ilikataliwa na Wakili wa Serikali upande wa mashtaka Apmak Mabrouk na kusaidiwa na Catherine Gwantu.

Hata hivyo Hakimu Mteite alieleza mahakamani hapo kuwa anaheshimu maelezo ya pande zote mbili kuhusu nyaraka hizo na kwamba nyaraka hizo ni muhimu kutokana na kuwa ndiyo ilitengeneza kesi hiyo na kuileta mahakamani kwani bila maelezo hayo kesi hiyo isingekuwapo.

Baada ya maelezo hayo Hakimu teite alieleza mahakamani hapo kuwa anapokea nyaraka ya maelezo ya mlalamikaji aliyoyatoa katika kituo cha polisi kama moja ya ushahidi wa mtuhumiwa katika utetezi wake.

Mbunge huyo alifikishwa na mahakamani hapo baada ya kukamatwa na polisi akiwa ofisini kwake wilayani Mbarali baada ya kutuhumiwa kwa kosa la kutishia kumuua kwa maneno Ofisa Mtendaji wa Kata ya Luiwa Jordan Masweve.


 
Back
Top Bottom