Hukumu dhidi ya Lema ni pigo kwa CCM

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Wengi wanahisi au kusema kwamba kulikuwa na influence juu ya judge kutoa hukumu dhidi ya Lema ili apoteze kiti cha ubunge. Kama kweli hili lilifanyika basi ni kwamba mtu wa CCM yeyotealiyeshiriki kufanya hivyo hana uwezo wa kuona mbali. Hukumu ya Arusha dhidi ya lema ni pigo kwa CCM kwa sababu kadhaa;

i) Uamuzi wa mahakama unazidi kufanya CCM walaumike na kupoteza kuungwa mkono Arusha hata kama hawastahili lawama
ii) CCM Arusha tayari ina nguvu kidogo, uchaguzi mdogo ukiitishwa uwezekano wa wao kuchukua kiti ni mdogo sana
iii) CCM watalazimika kuingia gharama katika na kujishughulisha na kampeni katika eneo ambalo wanajua hawatakiwi
iv) Uchaguzi mdogo Arusha, baada ya ule wa Arumeru, utazidi kuwaweka CCM katika wakati mgumu kuhusiana na kambi ya EL na wale wasio wa EL. Kambi ya EL inayohisi kuhujumiwa juu ya uchaguzi wa Arumeru itataka kulipiza kisasi ikiwa haitakuwa na mgombea wao katika uchaguzi wa Arusha. Na kambi isiyo ya EL haitataka tena mtu wa EL awe mgombea
v) IKiwa CCM itafanya kampeni na matokeo yakawa kwamba Chadema wakashinda uchaguzi mdogo wa Arusha, itakuwa na athari ya kuwafanya wengi waone Chadema inazidi kuwashinda CCM hata pale CCM inapo-influence uamuzi wa mahakama.
vi) Hali itakuwa mbaya zaidi kwa CCM ikiwa Tundu Lissu atashinda kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi na Dr. Makongoro kushindwa
 
ccm hawana ................. za kufikiria hayo wenyewe wanadhani wanaikomoa cdm kumbe imekula kwao
 
Hao uliowaambia ni ccm gani? kwani ccm ya sasa ni vipofu na viziwi. hawaoni wala hawasikii
 
Back
Top Bottom