Huku ni kujilinda na nini?

kama ni Moshi sushangai. hawa wamama wanawajibika sana. hapo utakuta alikuwa anatafuta makocha au nginda kwa ajili ya ng'ombe

ni kweli mkuu, kama ni kwa wamangi hapa waaaaaaalah hakuna cha kushangaa. wenzetu hawa wamassaweee, tofauti na makabila mengine mengi, wao huwa "hawaendi" shambani bali "wanaishi" shambani, wakiwa wamezungukwa na shamba-chotara yaani kila kitu ndani yake kuanzia ndizi, kahawa(zimepungua sku hizi baada ya kuchakachuliwa na serikali ya magamba), maduma, ndutu, maharage, mahandi(kwa msimu), mbogamboga, viazi vikuu navitamu, miti, maua masale nk nk (you name it). na hiyo nyumba iliyozungukwa na hayo mazao, ndani yake au pembeni yake kuna ngombe wa kisasa na kienyeji, mbuzi, kondoo(mahususi kwa tambiko mithili ya zile za nchi ya Ahadi au Taifa Teule..teh teh...wachagga bana utawapenda tu nachurale!!) kitimoto, kuku nk nk. This pipo are hardworking jaman acheni. Hilo hapo kiunoni mwa Mama yetu kipenzi ni ama panga, shami au mundo wa kukatia majani ya ngomebe wake wa kisasa, akamue maziwa, si ya kunywa yeye, ila ya kuuza azichange m/wa-toto (na pengine m/wa-jukuu waende shule). halafu sisi wengine huku tunabakia kulalamika oooooh uchagani kumeendelea kuliko kwingine...kalagabaho...teh!!
 
Back
Top Bottom