BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,032
- 3,944
Ninaangalia maadhimisho ya sherehe za Muungano yanayoonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV. Mvua inanyesha. Watoto waliokuwa wakionyesha michezo ya halaiki wamemaliza michezo yao na badala ya kutolewa kiwanjani, wamekalishwa chini kwenye uwanja uliojaa maji huku mvua ikiendelea kunyesha, waheshimiwa wakiwa wamekaa jukwaani wakiangalia ngoma. umri wa wengi wa watoto hawa ni chini ya miaka 16. Hivi hakuna kiongozi yoyote mwenye busara anayeweza kutoa amri watoto wale wanyanyuliwe pale walipo na wakajibanze banze sehemu nyingine badala ya kukaa chini ambapo pameloa chapa chapa?? Huku ndio kuwajali watoto wetu?? Huku ndio kusherehekea Muungano?? Imeniuma sana.