Huku kuzima moto kutaisha lini?

Foundation

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
1,421
596
Siku chache zilizopita tumeshuhudia Jeshi la Polisi hasa FFU wakishirikiana na mgambo wa Manispaa zote tatu za Jiji la Dar es Salaam wikishirikiana kuondoa Wamachinga katika maeneo mbali mbali hapa Dar es Salaam.

Walianza Ubungo TANESCO wakaenda Stendi ya Mabasi ya Mkoa, hawakuishia hapa tukasikia wamefika mbezi, mara wakaibukia Tegeta na sehemu nyingine. Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni wakasema zoezi litakuwa endelevu.

Najiuliza huo uendelevu wa hili zoezi limeishia wapi? Ukipita Usiku pale Ubungo daraja la Mandela mpaka Riverside, Wamachinga wamerudi kama kawaida. Je huo ndio uendelevu ambao Viongozi wa Mkoa na Wilaya walikuwa wanasema. Pale Ubungo Mataa, upande unaotazmana na shell kama unaenda Daraja la Sam Nujoma napo wamarudi. Bado nauliza huo ndio uendelevu.

Au mimi sikuwaelewa? Ama walisema litakuwa endelevu kwa wale watakaopanga maeneo ya Tanesco tu? Kama hivyo ndivyo,je kuna umbali wowote uliopo kati ya TANESCO na Daraja la Mandela na pale Shell kama itatokea hatari?

Na bado najiuliza kama hatari itatokea ina maana wale wanaopaki teksi na piki piki pale Songas haitwahusu? Wale mbona waliachwa. Au wenyewe wana Danger proof Materials?

Wakubwa kazi kwenu
 
Back
Top Bottom