KUTOKA VIKINDU: Polisi wapambana na majambazi, askari mmoja adaiwa kuuawa

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Imetokea usiku huu Mkuranga. Askari wazingira nyumba ambayo walikuwa wanafanya uchunguzi baada ya mauaji ya polisi Mbande.

Radio WAPO.

========

UPDATES;


=> Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.

=> Timu ya Mwananchi iliyo eneo la tukio imeshuhudia magari ya polisi (difenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.

=> Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru njia zimefungwa kutokana na mapambano hayo.

=> Polisi yaweka kizuizi cha barabara eneo la Kongowe, Mkuranga, magari yote yanayotoka na kuingia Dar yanapekuliwa.

=> Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Kuzuia Majambazi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Thomas Njiku amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi ya kichwa katika maeneo ya Vikindu Mkoani Pwani na watu wanaosadikika kuwa ni magaidi.
8f9c9ec9-a62c-4d09-86d7-9716baccdc1b.jpg
53f98493-e81a-4438-9e60-eb95699c72fe.jpg
318c460d-980f-40a3-a914-08ea26822eb0.jpg
acede86b-0d38-49fb-9312-001761e91472.jpg

Nyumba waliokuwa Wanaishi hao Majambazi

=> Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili ambaye anadai alikuwa bega kwa bega na askari hao alisema kwenye nyumba hiyo waliokamatwa ni watu 7, Wanawake, Watoto na Mwaume mmoja. Hakuna Jambazi yeyote aliyeuawa katika tukio hilo zaidi ya afisa huyo wa polisi.

=> Waandishi wa Habari walipata wakati mgumu kwani Walikatazwa kusogelea eneo la tukio wala kupiga picha.

UPDATES; 27 Agosti 2016

=>Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema polisi zaidi ya 80 wanatumwa kwenda kuongeza nguvu katika oparasheni inayoendelea huko Vikindu mkoani Pwani ambapo hadi sasa watu kadhaa wameuawa na wengine kukamatwa.
siro.jpg

Kamishna Simon Sirro

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbade jiji Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini amekataa kutaja idadi yoyote ile ya waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea.

Kuhusu taarifa za uwepo wa askari aliyeuawa, Kamishna Sirro amekataa kuthibitisha au kukanusha na kusema kuwa taarifa kamili kuhusu oparesheni hiyo itatolewa siku ya Jumanne ya wiki ijayo.

Amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu, na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa zitakazoweza kufichua wahalifu hao na kusisitiza kuwa jeshi hilo litawabaini na kuwatia nguvuni wote waliohusika.

Katika hatua nyingine, Sirro ameendelea kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote yale katika mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya zuio la jeshi la polisi la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano nchi nzima.

Usiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo, na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo.

Credit: IPP Media

=======

UPDATES: 05/09/2016

POLISI KANDA MAALUM DAR WAVUNJA MTANDAO WA MAJAMBAZI.

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefakiwa kukamata watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi hatari ambao wamekuwa wakishiriki matukio mbalimbali ya uhalifu kwa kutumia silaha.

Watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walipatikana na bunduki 23 za aina tofauti tofauti, Risasi 835, kifaa cha kuzuia risasi kuingia mwilini tatu (Burret Proof), Sare za Polisi, Pingu 48 pamoja na Radio 12 za mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya kanda maalum, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema kuwa majambazi hao walikuwa na mtandao mkubwa ikiwa ni kununua silaha nje ya nchi kwa ajili ya kufanyia uhalifu katika maeneo mbalimbali.

Kamanda Sirro amesema baada ya tukio hilo timu ya polisi ya upelelezi iliweka mtego na kufanikiwa kukamata majambazi watatu maeneo ya Mbagala, Keko na Kawe.

Kamanda Sirro amesema katika mahojiano walikiri kufanya tukio katika benki ya Habib African maeneo ya Kariakoo 2014 na Stanbic 2014.

Amesema kuwa majambazi walikiri kuwa na wenzao wako katika msitu wa Vikindu.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha kifaa cha kuangalia wakati wakifanya uhalifu majambazi kwa waandishishi wa habari ikiwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha bunduki kwa waandishi wa habari ikiwa ni sehemu yabunduki zilivyokuwa zikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya operesheni walioifanya na kukamata majambazi watatu katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.













 
Na gwanda zake...
Aaaah bado anazipiga pasi
sijui alizitafuta ndani muda gani na kuoga na kuvaa ndani ya na kutafuta dreva maana dreva yuko na muda wa kuingia kazi na kutoka kazi sasa ndani dakika 32 ya tukio na wewe unakuwa wa kwanza kufika katika tukio.basi huyu ndie waziri mchapa kazi ambaye tunamuitaji hakuna haha ya kuwapigia polisi simu 112.


swissme
 
Nilishasema kwenye mojawapo ya comments zangu juzi kuwa hayo mahuaji ya askari yanahusiana na lile tukio la yule jamaa aliyepigwa mawe akauliwa na akakutwa na mabomu ya kurusha maeneo ya Temeke au somewhere.
Shida ya polisi na viongozi wetu wanapenda kudandia treni kwa mbele bila kujiridhisha mapema.
Hawa jamaa wanajitahidi kukusanya silaha za kivita kwa kuiba kutoka vituo vya polisi, pesa wanazo ila hawawezi agiza silaha nje ndio maana wamejikita kwenye kuvamia vituo.
Serikali iamke au kuna siku watajutia na intelijensia zao uchwara. Yaani hii ni kitu rahisi unaunganisha tu dots kuazia yale matukio ya nyuma na zote jamaa wanafanana jinsi wanavyofanya uhalifu.
 
Naomba huyo mtu atafutwe alietoa hizi taarifa hizo ili asaidie kutoa taarifa zaa kina hilo neno ugaidi sio la kulipuuza na inaonekana ana agenda ya siri tafadhali mkuu wa operation na mafunzo kamshina Nsato
 
Jamani angalieni hayo maneno na yawe ya ukweli ndio upost hii inaleta attention isiyo ya kawaida, halafu taarifa kama hizo zina msemaji wake katika jeshi la polisi sio mtu yoyote tu na huyo mtu atajifunza mi maombi yangu tu kwa Msemaji wa jeshi la polisi Afande Advera Bulimba na kamishina wa operation na mafunzo mtutoe wasiwasi wajameni raia wenu kuhusu hiyo taarifa iliotumwa hapo juu
 
Utasikia vikao vya ndani vinasababisha ugaidi......(rejea tamko la nsanto marijani)
Halafu yale mazoezi yalikuwa yakukumbana na raia wasio an silaha....
Waziri wa mambo ya ndani sijui amewahi eneo tukio akiwa na uniform kabisa....(nawaza tu kwa sauti)

Rip askari aliyepoteza maisha
We inabidi uchunguzwe
 
Back
Top Bottom