Huko tuendako shughuli iko ! Jf members tupanuane fikra.

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Wana wa Bodi wenza, habarini za Jumapili .
Napenda sana kuutumia uwepo wa wengi wenu majumbani katika siku kama hii ya leo kupenyeza lile/yale yaliokita/gonga nafsi yangu katika wiki tunayoiacha .
Nyumba ninayoishi kwa sasa ninailipia M 2 , per anual .
Owner wa nyumba hii anakaa mkoa tofauti , na huu nilipo mimi.
Wakati ananipangisha hii nyumba aliniwekea sharti la kutokitumia chumba kimoja, kwamba chumba hicho ni tengefu kwa ajili yake pale anapokuja mjini hapa.
Kufuatia shida ya makazi niliyokua nayo nikalazimika nikubali , aidha sikua nikiyajua yatakayojiri baadae .
Mkuyyatt ninaoupata sasa ndiyo unaonitabainisha kwamba sikua nimefanya maamuzi sahihi .
Owner huyu kwa mwezi anakuja hapa kwa shughuli zake takriban mara 3 - 4 .
Mzee huyu ni cha-pombe kwa kwenda mbele. Akiwa hapa rudi yake home ni kuanzia saa 7 usiku na kuendelea . Na afikapo akigonga mfungua mlango kama si mie basi mmojawapo wa my family member. Majuzijuzi nimempita jirani na hom ambapo kuna grocery, kuniona tu , akanita yuko bwaksi la kisawasawa na akataka nimnunulie pombe " Niitishie bia tatu na usiponinulia tutakutana kwenye kodi "
Sikumnunulia bia hasa kwa kuniudhi juu ya mkwara alionipa .
Kwa mbele nyumba hii ina fremu 4 za maduka , ambapo nimeshawahi kuwasikia waliopanga maduka wakilalamika kua owner huyo akikuomba umnunulie kilaji usipomnunulia lazima akusulubu kwa kukupandishia rent.
Mimi nina kiwanja ambacho nilikinunua pakiwa na kajumba kakushikia kiwanja , kana vyumba viwili na sebule.
Na nilikuta kajumba hako kana mpangaji , ambae akawa mpangaji wangu baada ya ununuzi. Akiwa anamlipa laki 3 per year kwa alieniuzia.
mwaka jana nikaamua nimpandishie kodi hadi laki 4, kwani mie bado sijajipanga kiukamilifu kujenga.
Mpangaji yule akaniambia hana tatizo na hiyo bei ikiwa nitamtengenezea Choo.
Wana Jf , hapa kwenye choo ndipo palipobeba msingi wa mimi kuileta Sredi hii kwenu.
Choo na bafu vya kawaida kabisa kuanzia shimo, kulifunika na kupandisha kuta kimekula M 2 !
Na siku M 2 zinakatika choo/bafu vilikua vinadai vitasa , bawaba, na nyavu za dirisha.
Wanabodi kama choo kinalamba kiasi hiki ? Hizi nyumba tutajenga?
Tatizo liko wapi hadi gharama ya vitu nyeti kwa maisha yetu iwe ghali na juu kihivi ? Tufenyeje kupunguza makali haya ?
Wakati nyumba za kupanga miongoni mwake ni kama hii ya Mz. Cha ulabu kama nnayoishi sasa ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom