Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 883
Hujuma Usalama wa Taifa
na Mwandishi wetu
IDARA ya Usalama wa Taifa imekuwa ikipoteza mamilioni ya fedha kwa ajili ya kulipa ankara za simu za mkononi za watu hewa ambao wamefanikiwa kuzinasa line za simu zinazotumiwa na maofisa wake wa juu. Tanzania Daima Jumatano linakuthibitishia.
Vyanzo vya habari vya uhakika kutoka ndani ya kampuni moja ya simu za mkononi, vimelidokeza gazeti hili kuwa, wamebaini kuwepo kwa mtandao wa watu waliofanikiwa kuzinasa line hizo ambazo hulipiwa na idara hiyo kila mwisho wa mwezi.
Vyanzo hivyo vilieleza kuwa, kampuni hiyo ilishtushwa na matumizi na gharama kubwa ya simu hizo ambazo ziko katika orodha ya maofisa wa juu wa idara hiyo wanaolipiwa ankara za simu zao za mkononi.
Uchunguzi wa muda mrefu wa gazeti hili ulibaini kuwa baadhi ya watu wanaotumia simu hizo si maofisa wa juu wa idara hiyo bali ndugu au jamaa zao ndio waliwahi kufanya kazi katika ofisi hizo nyeti za serikali.
Mmoja wa watu anayetumia simu zenye line hizo alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu madai hayo, awali alilitaka gazeti hili kumpa muda kutoa jibu kwa kile alichokieleza kuwa haruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari bila kupata idhini ya mkuu wake wa kazi na alilitaka gazeti kumpigia simu baada ya dakika tano.
Mtu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Jimmy Mwangonda alipopigiwa tena baada ya muda huo, simu yake iliita bila majibu na baadaye alipoipokea, alieleza kuwa simu hiyo ni mali ya serikali na inatumiwa na watu kadhaa wanaoisaidia serikali katika kazi nyeti, kisha akakata simu.
Alipopigiwa tena ili kutoa ufafanuzi wa maelezo yake, simu yake ilikuwa haipatikani.
Alipoulizwa kuhusu ukweli taarifa hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, alisema kuwa serikali haina watu wanaolipiwa gharama za simu kama maofisa wa juu wa usalama wa taifa kwa ajili ya kuisadia katika kazi nyeti.
Alisema taarifa za kuwepo kwa watu wenye line za simu za maofisa wa juu wa idara ya usalama wa taifa zimemshtua na aliahidi kuwa, serikali itafuatilia suala hilo na itatoa taarifa kwa umma ili watakaobainika kujihusisha na mtandao wafahamike kwa umma, sambamba na kuchukuliwa hatua za kisheria.
-Tanzania Daima 26/11/2008