Hujuma Ubalozi wa Tanzania Sweden

Originally Posted by Mafuchila
Acheni unafiki, majina ya waliojiuzia nyumba wametajwa na Ben Moses sio mmojawao, tafuteni jungu lingine.

"Kuhusu familia sita na watumishi wanne waliouziwa nyumba zaidi ya moja, alisema familia tano zimerudisha nyumba tano na kubakiwa na tano wakati watumishi hao wanne wamepewa hadi Septemba 15 kurejesha nyumba ya ziada vinginevyo serikali itafuta mkataba wa nyumba mojawapo.

Kiambatanisho kinaonyesha wahusika walikuwa familia ya Balozi Ben Moses na Dk. Edna Moses (Mambo ya Nje na Afya); Hussein Abdulrahman na Mwanamtama Marandu (Shirika la Reli na Elimu), Emil Kayega na Emerensiana Kayega (Ofisi ya Makamu wa Rais na Ardhi na Makazi), Clement na Esther Mshana (TVT na RTD)."

Duh JF bwana, sometimes inaweza ikawa noma kweli! ukikurupuka,

sasa mkuu Mafuchilla kubali kuwa ulikurupuka bila facts, ili tuendelee na mjadala huu muhimu kwa taifa.
 
Nyinhyi watu wa Denmark mmezidi sana uswahili. ......... huyu mzee ni bingwa wa kutafuta watu wake na kuwasaidia kwa kadiri anavyoweza. Hapa Finland kwa kweli tunajivunia sana kuwa na balozi wa aina yake na tunampa bravoooooooo.

Ndugu Mfuchila,

Huyu ni Balozi wa watanzania wa nchi Gani? Finland tu ama na nchi nyingine????

Je hawa watu wake ni kina nani (nadhani ni few ambao ni pamoja na wewe angalia ulichosema hapo juu)??????

Kama watu wa Denmark wanamsingizia hebu elezea umma hapa nini huyu bwana alipchokifanya walau cha kumkumbuka???????

Bowbow
 
Hakuna unafiki ni kweli Balozi Ben Boses na Dr Edna Moses "walinunua" nyumba 2 wakati utaratibu ni familia moja nyumba moja kama kiambatanisho hapo chini;

Masatu
Sikuwa naifaham hii habari nashukuru kwa kuiweka lakini kuna walakini kidogo

Je imeandikwa Daily News 30, Aug..... lakini ipo kwa kiswahili na mwisho tunaambiwa inatoka Habarileo naomba kufahamishwa hapo kwenye huo utata.

Mzee FMES nashukuru kama hii habari ilikuwa haijafika kwa Membe umfikishie

mimi nipo tayari hata kuwasiliana nae kama atapenda for detail- kwa kweli nimeudhika sana
 
deny_all,

umeuliza swali la msingi sana......Dr Ben Moses ni kati ya ma-PS wachache waliojijengea sifa sana katika uchapaji kazi.............sijui imekuwaje

Unaweza kuwa PS mzuri na usiwe mwakilishi/balozi mzuri!
Hivi kwanini career diplomats wasiachiwe fani yao badala ya kuteua watu kwa considerations ambazo ni irrelevant?.....je ubalozi ni hisani?..kazi gani tena nyingine zinaweza kufanyika mradi umeteuliwa? am I making myself clear?
ENYI CAREER DIPLOMATS HEBU MTUELEZE/MTUELIMISHE KUHUSU HILI...
 
Masatu
Sikuwa naifaham hii habari nashukuru kwa kuiweka lakini kuna walakini kidogo

Je imeandikwa Daily News 30, Aug..... lakini ipo kwa kiswahili na mwisho tunaambiwa inatoka Habarileo naomba kufahamishwa hapo kwenye huo utata.

Mzee FMES nashukuru kama hii habari ilikuwa haijafika kwa Membe umfikishie

mimi nipo tayari hata kuwasiliana nae kama atapenda for detail- kwa kweli nimeudhika sana

Daily News na HabariLeo ni magazeti yanatolewa na kampuni moja Tanzania Standard Newspapers.

HabariLeo linapatikana - HabariLeo: Gwiji La Habari Tanzania | Maskani
Dailynews linapatikana - Daily News: Your Authoritative Newspaper | Home Page
 
japokuwa mimi si career diplomat kwa ufahamu wangu mdogo ni kwamba balozi anaweza kuwa "political appointee" yaani anateuliwa na rais kwa sababu za kisiasa zaidi (wakati mwingine huchanganya na za kibinafsi) au career diplomat anayepanda ngazi hadi kufikia ngazi ya ubalozi.

balozi makini hata akiwa "political appointee", huwatumia wataalamu wanaomzunguka ambao mara nyingi huwa career diplomats. bahati mbaya hao wataalamu wakiwa bomu basi inakuwa taaabu tupu.

sasa kwa balozi ben moses yeye yupo kwenye hilo kundi la kwanza (wapo wanaodai kuteuliwa kwake kunahusika zaidi na uhusiano wake na bwm). binafsi nimewahi kusikia malalamiko kuhusu utendaji wake kwa ujumla wakati yupo canada kwa kiasi kikubwa ninamuamini aliyenipa taarifa hizo japokuwa nakiri sikufanya utafiti zaidi kuhusu hilo suala..
 
Masatu
Sikuwa naifaham hii habari nashukuru kwa kuiweka lakini kuna walakini kidogo

Je imeandikwa Daily News 30, Aug..... lakini ipo kwa kiswahili na mwisho tunaambiwa inatoka Habarileo naomba kufahamishwa hapo kwenye huo utata.

Mzee FMES nashukuru kama hii habari ilikuwa haijafika kwa Membe umfikishie

mimi nipo tayari hata kuwasiliana nae kama atapenda for detail- kwa kweli nimeudhika sana

Mkuu tupo ukurasa mmoja, maana huyo mkulu yupo hapa siku zote hizi zimefika tayari.
 
Balozi Moses hakuwa na uwezo wa kujiuzia nyumba. Uwezo huo ulikuwa Wizara ya Ujenzi. Nijuavyo mimi ni kuwa nyumba zilitakiwa kuuzwa kwa wafanyakazi wa serikali ambao walikuwa wakiishi humo kihalali. Inaelekea Balozi na mke wake wote kila mmoja alipewa nyumba awali kama stahili yake kutokana na wadhfa aliokuwa nao. Hivyo inaeleweka kama kila mmoja akauziwa nyumba hiyo. Tunajuaje kama wakati wanapewa hizo nyumba awali kama hawakuwa na mpango wa kuendelea kuishi pamoja? Je, Dr Edna Moses kama asingekuwa mke wa Balozi asingestahili kupatiwa na kuuziwa nyumba?

Mbona tumesikia kuwa wadogo wa wengine waliuziwa nyumba kimpango? Nyumba ambazo kuna kila uwezekano kuwa kaka mkubwa ndiye aliyelipia! Hawa ndio wa kuwakolomea si huyu.

Kudai kuwa Balozi Moses alijiuzia nyumba ni kumuonea na kutomtendea haki.
 
Aliyetoa mada kuhusu Tanzania kwa kweli alinigusa na alielezea kwa ufasaha vivutio vya Tanzania na hata girl friend wangu amehamasika kwenda Tanzania. Tulipomuomba mtoa mada kuhusu vipeperushi ambavyo mtu akitaka kusoma zaidi ndipo nilipogundua hujuma yenyewe
....
mbona wajichanganya? unalalama na vipeperushu WAKATI huyo girlfriend wako anhamasishwa na wengine. Sasa braza, KIPEPERUSHI kwa huyo MDANE unatakiwa uwe ni wewe. Charity begins at home. Its wahat yopu can do and not what can be done by anyone else. Ikke?
 
..............

Back
Top Bottom