Hujuma: Budget ya Serikali inatumika kuimarisha CCM nchi nzima

Katiba mbovu ilizaa sheria mbovu. Mchakato mbovu utazaa katiba mbovu.

Mimi nilisusia mchakato huu wa kisanii juu ya katiba mpya. Tutaandika nyingine baada ya 2015.

CCM kitarudisha mali zote za umma kilichojimilikisha kiharamu kama majengo, viwanja nk nasi tutaziweka katika kapu/fuko la Taifa. Pia tutapitia na kuchunguza na kuhakiki mahesabu ya hazina, wizara na halmashauri zote ktk kipindi miaka mitano nyuma i.e. 2010 foward;

Kwa wajinga kama Nape ambao wamejaa CCM wanadhani wanachukua chao mapema. Watarudisha na riba. Tunataka haki na uwajibikaji wa hali ya juu, na hizi ghiliba na wizi unaohalalishwa na Pinda utakuja watokea puani.

There's no peace for the wicked!!!
 
...Mkuu na bado wanachota nyingine nyingi toka hazina ili kugharamia ufisadi wao na mambo mengine mbali mbali ndani ya chama chao cha magamba. Ila mie nina wasiwasi na mambo unayoyaandika hapa na utumiaji wa jina lako, nchi yetu imeharibika Mkuu, tafadhali jilinde.
Mkuu mbona una mfundisha uoga...lol
 
Makamu wa rais alipita mkoani kwetu na kuchota hela za serikali eti ni ahadi ya 2,000,000/= kwa tawi la ccm na zililipwa kutoka mfuko wa serikali,.nikajiuliza akifanya hivyo kila wilaya ccm itakuwa imeiba shilingi ngapi za serikali?bado vikao vya ccm vinafanyika kwenye kumbi za serikali bila kutoa hela na wananunuliwa chakula kwa fedha za serikali ...nchi ovyo kabisa hii.
 
Moja ya mambo makubwa ambayo katiba ijayo inatakiwa kuweka bayana ni kufutwa kwa vyeo hivi vya wakuu wa wilaya na mikoa. Katika ngazi ya mkoa:

  1. Kuwe na Gavana wa mkoa ambaye atachaguliwa kwa kura za wananchi wote badala ya kuwa mteule wa rais. Yeye ndiye awe mtendaji mkuu wa mipango ya mkoa.
  2. Kila mkoa uwe na baraza la uongozi (mfano wa bunge) ambalo litakuwa na jukumu la kupanga na kusimamia mipango yote ya maendeleo.
  3. Mkoa uwe na uwezo wa kuajiri wafanyakazi wake wote.
Katika ngazi ya wilaya/manispaa/jiji:
  1. Shughuli zote za maendeleo zisimamiwe na wenyeviti wa wilaya au mameya.
  2. Madiwani kama ilivyo sasa waendelee kupanga na kusimamia mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

Kuhusu shughuli zenye sura ya kitaifa kama maswala ya ulinzi, mahakama, polisi, magereza, uhamiaji nk kuwe na mabaraza ya ulinzi na usalama ambayo mwenyekiti wake awe na wadhifa wa waziri na ateuliwe na rais wa nchi. Kama muundo huu utawekwa basi idadi ya mikoa itabidi ipunguzwe ili mikoa iwe na uwezo mkubwa wa kiuchumi.

Eliah G Kamwela says thanks for this very useful post
 
Acheni matusi jamani, mara muwaite wenzenu Fools mara muwaite watumishi wa umma wana digrii za chupi, hivi nani anawapa jeuri hii??

sio matusi ila jembe liitwe jembe, panga liitwe panga kijiko kiitwe kijiko, mjinga aitwe mjinga and so on!!
 
Vikao vya kamati kuu na NEC ya CCM hufanyika ikulu na sidhani kama CCM wanalipia gharama yeyote ile

8E9U0046.jpg
 
Back
Top Bottom