Hujaona Manufaa au Umuhimu wa Sensa? Au Umeamua kutoona?

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Kabla na baada ya zoezi la sensa ya watu na makazi kuanza kumekuwa na mjadala unaoonesha kuwa baadhi ya watu hapa nchini bado hawajaona manufaa au umuhimu wa zoezi hilo.

Hadi sasa kuna makundi mawili ambayo yako kinyume na zoezi hilo. Kundi la kwanza ni la wale wanaotaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa.

Kundi hili lina vinara wake ambao wanaendesha kampeni za wazi kuwashawishi na kuwataka waislam wagomee zoezi hilo. Kundi la pili halina vinara wala halina makundi ya kampeni.

Hili lina mtu mmoja mmoja ambaye hataki kushiriki zoezi la sensa kwa sababu kila mmoja wao anadai haoni manufaa ya zoezi hilo kwa mtu binafsi na kwa taifa tangu zoezi kama hilo lianze kufanyika miaka ya nyuma.

Kwa upande mwingine kuna serikali ambayo ambayo inadai kuwa zoezi la sensa halihusiani na masuala ya imani. Ni zoezi la kuiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo kulingana na takwimu zinazoonesha idadi ya watu, kipato chao, makazi yao ili iweze kutoa huduma kwa uwiano wa idadi ya watu wake. Na kwamba serikali haina dini ingawa watu wake wana dini.

Kwangu mimi kama ninavyoelewa, nami sina elimu ya demografia, zoezi la sensa na makazi linamanufaa kadhaa lakini miongoni mwa hayo ni kama yafuatayo:-
  1. Serikali na taifa linabaini wastani wa kiwango cha ongezeko la watu wake hivyo huweza kuweka maoteo ya vipaumbele kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
  2. Serikali na taasisi mbalimbali zitaweza kujua wapi na kwa kiasi gani huduma fulani zipelekwe. Mfano, kwa kujua idadi ya watu wa eneo fulani unaweza kujua hata athari za magonjwa kwa jamii hizo mfano UKIMWI nk kwa kuwianisha waathirika na idadi ya watu mahali hapo.
  3. Serikali itaweza kuweka uwiano wa huduma za kijamii mfano shule, vyuo, hospitali, nk katika kila eneo kwa kuangalia idadi ya watu katika eneo husika.
  4. Ulinzi na Usalama hupangwa kwa kulenga uwiano wa polisi mmjoa na raia anaopaswa kuwahudumia. Mwanajeshi mmoja na raia anaopaswa kuwalinda wakati wote wa amani na wakati wa vita.
  5. Daktari, mwalimu, muuguzi nk wote wanapangwa na kuelimishwa kwa kuzingatia uwiano wao na idadi ya watu wanaopaswa kuwahudumia sawa sawa na vigezo vya taaluma au kada zao.
  6. Kisiasa na kidini, kila chama au dini inatumia takwimu za idadi ya watu na makazi ili zijipange kupata wafuasi au kuhudumia wafuasi wao katika maeneo husika. Sidhani kwamba chama au msikiti au kanisa litapeleka huduma zake nyikani kusiko watu wala makazi.(Ingawa kwa wakristo yawezekana, kwani, Yohana Mbatizaji alianza huduma yake nyikani-Biblia)
  7. Zoezi la sensa linasaidia kujua idadi ya watu na marika yao. Kwa mfano, leo hii kuna kampeni inayoendelea kwamba wazee wapewe huduma bure za afya pia walipwe mafao ya uzeeni pasipo kubagua kati ya wastaafu na wakulima wazee. Kampeni hizi zitapangika kwa urahisi na kuwa endelevu kwa kujua wastani wa ongezeko la wazee na makazi yao kwa kila kipindi fulani.
  8. Kwa kujua idadi ya watu nirahisi kuoainisha utajili wa raslimali zetu na uondoaji wa umasikini kwa mtu mmoja mmoja na hadi taifa kwa jumla.

Kwa hiyo, kwa hayo machache inaonesha jinsi ambavyo sensa na ya watu na makazi ilivyo na manufaa kwa ustawi wa jamii. Pamoja na umuhimu huo, kwa serikali ya kifisadi, serikali ya kitabaka, serikali ya watawala wachache na familia zao sensa haina maana.

Lakini kwa kuwa dola wakati wowote inaweza ikachukuliwa na chama kingine nje ya hiki cha kifisadi kisichotawala kisayansi na kitakwimu; kinachotoa huduma kifisadi na kisiasa. Zoezi la sensa litatumiwa na chama cha ukombozi wa umma kuleta mabadiliko na mapinduzi halisi ya kuelekea maendeleo ya umma.

Idadi ya watu ikijulikana ipasavyo, masuala ya "kasungura" kadogo linaweza kwisha tukijipanga sawasawa kupitia chama na utawala mbadala.
ALUTA CONTINUA!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom