Hujaji Mtanzania Atozwa Kaini Kwa Ushirikina Saudia!

KILITIME

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
265
18
MTANZANIA mmoja ambaye ni miongoni mwa mahujaji zaidi ya 1,500 waliokwishawasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hijja, amekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Madina na kutozwa fani ya Riyari 300 baada ya kukutwa na vitabu vinavyodaiwa kuhusika na mambo ya kishirikina.

Taarifa kutoka nchini Saudi Arabia, kama zilivyoripotiwa na Mwandishi Wetu, Bwana Juma Mmanga, zimebainisha kuwa Mtanzania huyo amepigwa faini hiyo ambayo ni sawa na dola 200 za Marekani baada ya kuonekana ni mgeni, lakini kwa nchi ya Saudia Arabia angelazimika kufungwa kifungo cha mwaka mmoja jela au miezi sita.

Imedaiwa kuwa vitabu hivyo vinavyosadikiwa kuwa ni vya kishirikina ni vile vya kuunga na vinavyotumiwa na watu ambao huitumia Kuran vibaya na ambavyo huleta athari kwa jamii ikiwa ni pamoja na kumfanya mtu kupoteza akili.

Wakati huo huo, mahujaji 1,590 kutoka Tanzania tayari wamewashawasili katika uwanja wa ndege wa Madina na Gida ambapo sasa njia za kuelekea katika mji mtakatifu zimefungwa.

Imeelezwa kuwa kutokana na hali hiyo mahujaji wote sasa watakaoshuka Uwanja wa Ndege wa Gida watalazimika kwenda moja kwa moja Makka kusubiri kutekeleza rasmi ibada ya Hija.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Suleiman Lolila alisema Bakwata haina taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo.

“Mbona hizo taarifa sisi hatuna? alihoji Katibu huyo na kuongeza, “Ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako. Sielewi kitu chochote kuhusiana na suala hilo,” alisema.

Katika hatua nyingine, Rehema Mwakasese anaripoti kuwa hofu ya kulipuka kwa ugonjwa wa mafua ya nguruwe kwa mahujaji wanaoshiriki ibada ya hijja nimetoweka na mambo kuendelea kuwa shwari.

Awali, kulikuwa na hofu kuwa huenda mlipuko wa ugonjwa huo ungejitokeza nchini humo kutokana na idadi kubwa ya mahujai kutoka nchi mbalimbali duniani ambao wanashiriki ibada hiyo.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu kutoka Madina Saudi Arabia, Kiongozi wa kundi la Aldir, Sheikh Abdallah Amani, alisema hadi sasa hakuna taarifa zozote za matatizo ya kiafya kwa mahujaji wa Tanzania wala hofu ya kutokea kwa ugonjwa huo.

Sheikh Abdallah, alisema mahujaji wote wa Tanzania wanaendelea vyema na maandalizi ya ibada hiyo ambapo kesho wanatarajia kuondoka kwenye mji wa Madina kwenda Makka ili kuanza rasmi ibada.

Kwa upande wake, Sheikh Muharami Juma Doga, amewaomba Watanzania kuwaombea mahujaji wote waliopo nchini humo ili waweze kumaliza vyema ibada zao na hatimaye warejee nyumbani wakiwa salama.

SOURCE: http://www.majira.co.tz/index.php?o...na-saudia&catid=34:kitaifa-tanzania&Itemid=57
 
Sorry, wakuu, title isomeke neno "Faini" badala ya "Kaini!" Mods naomba mrekebishe title!
 
Mi naomba huyo hujaji anitumie kama experiment ya kunipiga hicho kitonto cha kurani tuone kama kweli kinafanya kazi.

Yaani kuna watu so primitive.
 
Huyu ni wa kumkata shingo tu...sijui wamemwachaje saudi???
Akirudi bongo akatambike..kule hawana ujinga...inawezekana
ushirikina umemsaidia hata kupunguziwa adhabu
 
Mi naomba huyo hujaji anitumie kama experiment ya kunipiga hicho kitonto cha kurani tuone kama kweli kinafanya kazi.

Yaani kuna watu so primitive.
Pale alitaka sijui amloge nani!
 
Huyu ni wa kumkata shingo tu...sijui wamemwachaje saudi???
Akirudi bongo akatambike..kule hawana ujinga...inawezekana
ushirikina umemsaidia hata kupunguziwa adhabu

Mmmmh, naona kama umeenda mbali, kwa habari ya shingo yake!
 
Vipi Kuhusu Kina Sheikh Yahya Hussein?? Si Ule pia ni Ushirikina???
 
Huyu ni wa kumkata shingo tu...sijui wamemwachaje saudi???
Akirudi bongo akatambike..kule hawana ujinga...inawezekana
ushirikina umemsaidia hata kupunguziwa adhabu

My sentiments exactly. Nimeshangaa. Mbona wezi wanawakata mikono iweje mshirikina? Kwa hiyo nia ya kutaka kumdhuru binadamu mwenzako ni kosa dogo kuliko kumwibia?
 
Hivi hizi aya za Quran unaweza kumsomea mtu akachanganyikiwa? Maana nimesikia usemi huo mara kwa mara!
 
Back
Top Bottom