Huenda yumo humu JF

Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
323
Wanajamvi, utu uzima unazidi kuyoyoma, miaka 33 inakatika sina wa ubani mie. Huenda yumo humu jamvini aliye mpweke kama mie, binti maridhawa, mpenda maendeleo, asiyezidi miaka 30, elimu angalau asiwe chini ya kidato cha nne, anayejituma katika kufanya kazi mvivu simtaki akha! Kupima Virusi vya UKIMWI muhimu tena asiwe macho juu penzi tamu atapata.

Uliye tayari nitumie PM.
 
kila heri mkuu, hebu weka CV yako sawa sawa mbona kama fupi sana?

Mie ni kijana mcheshi, mwenye kujenga marafiki wema, ninaependa kusoma na kujiendeleza kwa kutaka kujua mambo mapya kuendana na ulimwengu. Mwembamba, elimu yangu kidato cha nne tu, umenisoma? Kingine?
 
kila la kheri wa ndima, mwandani mtie ndani,
ziwe kidogo gharama, za pete pia vidani,
pamoja mali kuchuma, ziwafae maishani,
tena muepuke ngoma, wana mpate sheheni
 
Jamani mnaotafuta wachumba wekeni na picha zenu.
Tunaogopa kuingia choo cha watoto.
 
Naona club yetu wataftaji imeongeza member. Karibu mkuu tutafute wa kutusaidia kutekeleza amri ya Mungu, "zaeni mkaongezeke,muutiishe ulimwengu". All the best.
 
kila la kheri wa ndima, mwandani mtie ndani,
ziwe kidogo gharama, za pete pia vidani,
pamoja mali kuchuma, ziwafae maishani,
tena muepuke ngoma, wana mpate sheheni

Nashukuru Miss Judith, ushauri tazingatia,
nimuepuke Ibilisi, Ukimwi kutojipatia,
Niwe na bora kizazi, ili nisije kujutia

Nimeona umri waenda, sijapata aletulia,
Binti asiye na inda, penzi bora kunipatia
Na yule aliyenitenda, bahati aje ijutia
 
Mhhhh! Judy na Wa ndima mkiamua kuwa pamoja na kufunga pingu za maisha nyumbani kwenu mashairi mtindo mmoja kuanzia mnapoamka mpaka mnapopanda kitandani hahahahahahahah. Ikitokea hivyo basi harusi yenu nitaomba Muumba wetu anipe uzima ili niweze kuhudhuria na kuwapigia vigelegele na kuwaimbia wanameremeta wanameremeta.
 
bubu ataka kusema, heshma umesheheni,
hakima wewe watema, bure hapa jamvini,
yafaa kwake wa ndima, judi daima makini,
mola akupe uzima, heri nyingi maishani
 
Mhhhh! Judy na Wa ndima mkiamua kuwa pamoja na kufunga pingu za maisha nyumbani kwenu mashairi mtindo mmoja kuanzia mnapoamka mpaka mnapopanda kitandani hahahahahahahah. Ikitokea hivyo basi harusi yenu nitaomba Muumba wetu anipe uzima ili niweze kuhudhuria na kuwapigia vigelegele na kuwaimbia wanameremeta wanameremeta.

Huenda tayari anae ndo maana hajajiweka hapo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom