Huduma za wagonjwa matibabu moi zasimama tena

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,193
515
Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dkt. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dkt. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.

Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

Kauli za wagonjwa

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini, "Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao," alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa, "Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?" alilalamika Jenipher.

Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dkt. Ulimboka, "Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dkt. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.

Soma habari nzima kwenye gazeti la Tanzania Daima




Wakati uongozi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), ukitangazia umma kwamba huduma katika taasisi hiyo zimerejea kama kawaida, uchunguzi wa kina wa gazeti la MWANANCHI umebaini kwamba huduma katika taasisi hiyo na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), bado zinasuasua.

Juzi, uongozi wa MOI ulitoa taarifa kwa umma ukisema mgomo wa madaktari bingwa uliokuwa umetangazwa awali ulikwisha, huku uongozi wa MNH nao ukisema huduma zimerejea katika kiwango cha kati na kutaka wagonjwa waendelee na huduma kama kawaida.

Uchunguzi uliofanywa jana katika taasisi hiyo ya MOI na MNH na taarifa kutoka vyanzo mbalimbali, ulionyesha taarifa hizo mbili zinapingana na hali halisi ya utoaji huduma na mahudhurio ya wagonjwa katika hospitali hizo mbili.

Uchunguzi huo ulibaini kwamba, kitendo cha uongozi wa MOI kuwatembeza waandishi wa habari kujionea huduma za upasuaji juzi, kilikuwa ni mchezo wa kupanga ili kuonyesha umma kuwa huduma zimerejea.

Chanzo chetu cha habari kilisema Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Profesa Lawrence Museru alifanya jukumu la kuwapigia simu madaktari ambao anawajua ili kumnusuru na adha hiyo ya mgomo wa madaktari, "Mkurugenzi (Profesa Museru), aliwapigia simu madaktari akiwataka kufika kufanya upasuaji ili nyie waandishi mkipiga picha mwonyeshe kuwa huduma zimerejea," kilisema.

Hata hivyo, alipoulizwa Profesa Maseru alijibu: "Hatuna sababu ya kudanganya mtu. Lakini, kama unataka maelezo zaidi naomba uje ofisini."

Juzi akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi ya MOI, Profesa Charles Mutalemwa alisema toka Jumatatu wiki hii madaktari 79 wamerejea kazini.

Profesa Mutalemwa alisema madaktari bingwa waliorejea ni 18 na 61 ni madaktari wa kawaida na walioko mafunzoni hivyo huduma zinaendelea kuimarika kadri siku zinavyoendelea.

Mwananchi lilifika katika kitengo hicho kujionea hali halisi ya huduma na kukuta wagonjwa wakipangiwa kufika hapo mwanzoni mwa mwezi ujao.

Kauli za wagonjwa

Aidan Kisanga ambaye alifika katika kliniki kutokana na tatizo la kuvunjika mguu, alisema, licha ya kutakiwa kuonana na dakatri jana, imeshindikana, "Nimeambiwa nirejee hapa Juni 30 mwaka huu au kama nitasikia taarifa katika vyombo vya habari kuwa huduma imerejea. Inaniuma kwani mguu wangu unaniuma na sijui nitafanya nini," alisema Kisanga.

Jakobo Chacha mkazi wa Kitunda, alisema alifika hospitalini hapo saa 11.30 asubuhi jana na kupewa namba 26, lakini hakupata matibabu baada ya mhudumu ambaye hakumfahamu, kuwatangazia kuwa hakuna huduma kutokana na ukosefu wa madaktari, "Tulitangaziwa kuwa tuondoke na waliokwishalipia huduma wabaki. Wasiolipia tulikuwa tunapangiwa kila mtu na tarehe yake," alisema Chacha na kuongeza: "Jana (juzi), tumeambiwa madaktari wamerejea na kutakiwa kufika kupata huduma kumbe ilikuwa ni uongo, wanatuambia twende hospitali binafsi sasa kama sisi wa hali ya chini si tutakufa?" alihoji.

Ezekiel Mkandainda ambaye amelazwa katika wodi ya Sewahaji, MNH, alisema mgomo bado unaendelea na jambo hilo limefanya baadhi ya wagonjwa kufariki na wengine kuamua kuondoka kutokana na kukosekana madaktari, "Mwandishi, madaktari bado wanaendelea na mgomo, leo (jana) ilikuwa siku yangu ya kuonana na daktari, lakini hatujamwona daktari yeyote aliyepita wodini kwetu zaidi ya wauguzi," alisema na kuongeza: "Wagonjwa wengi wameondolewa na ndugu zao kwenda kutibiwa kwenye hospitali za watu binafsi. Mimi nimetoka Mkoa wa Kigoma nina matatizo ya kibofu cha mkojo natakiwa nifanyiwe upasuaji, lakini hadi leo sijafanyiwa."

Mgonjwa mwingine aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, MNH, Aisha Abdallah alisema wagonjwa waliopo katika wodi hiyo ni wachache kutokana na wengine kuondolewa na ndugu zao baada ya kukosekana madaktari.

Kauli ya Uongozi MNH

Ofisa Habari wa Hospitali hiyo, Aminieli Aligaesha alisema kusuasua kwa huduma hizo kumetokana na madaktari hao kuanza kazi Julai 2 mwaka huu ambao ni wachache, "Kuhusu huduma kusuasua ndiyo kwanza madaktari wameanza kazi wiki hii siku ya Jumatatu hivyo, tusitegemee huduma kuwa nzuri kama mwanzo. Madaktari watakapokuwa wengi huduma zitatolewa kama kawaida," alisema Aligaesha.


Source: ************************** wavuti - wavuti
 
Wao na media , Drs na solidarity, patamu hapo.Ukisikia kukimbiza mwizi kimya kimya ndio huku.Drs hawasemi kitu ila wananchi watajionea wao kama mgomo umeisha au bado.Liwalo na liwe
 
Mungu mnusuru Dr Ulimboka, nimeomba na kushukuru katika jina lipitalo majina yote, Jina pekee la Yesu.
 
Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Vasco da gama alichimba mkwara nafikiri anajiandaa kwenda misitu ya pande kuchimba mwingine
 
mgomo huu ukiwa kama wa walimu itakuwaje? ambapo ma dr watawatibu wagonjwa, bila kuzingatia maadili nani ataumia?
 
Hotuba ya jk haikuwa na suluisho alisema tu pasipo kuwa na plani B ku kava nafasi ya walotimuliwa na watakaoamua kuacha kama alivopendekeza. Sasa liwalo na linazidi kuwa!
 
Mungu mnusuru Dr Ulimboka, nimeomba na kushukuru katika jina lipitalo majina yote, Jina pekee la Yesu.

Utashukiwa kama mwewe amshukiavyo kifaranga cha kuku. We endelea tu kutaja hilo jina la YESU WA NAZARETI
 
mgomo huu ukiwa kama wa walimu itakuwaje? ambapo ma dr watawatibu wagonjwa, bila kuzingatia maadili nani ataumia?

Ndio maana nawasihi wananchi tiwaunge mkono madaktari kwa sababu siku ya kuugua kwetu tutakabiliana uso kwa uso na daktari bila kusindikizwa na ffu wala diffender. Kumbukeni, kwa msongo wa mawazo ya kipato chini ya kiwango mgonjwa aliwahi kupereshenia kichwa badala ya mguu, na mguu badala ya kichwa, hali itakuaje pale msongo wa mawazo utakapochangiwa na uzembe wetu kutowaunga mkono madaktari? TUTARAJIE KUSIKIA AU KUHISI "SI MLIIUNGA MKONO SERIKALI! NENDENI KWA KOVA MKAANDIKIWE VIPIMO" AU "SUBIRI DOCTA MWIGULU ASAINI FORMS"
 
Mm ninawachukia wanafiki, Madaktari wanaogoma wameshaambiwa waachie ngazi mwajiri wao hayawezi masharti yao kwa nini wanang'ang'ania hapo Hospitalini? Au basi wende kwa mwajiri pale Wizarani kabla ya jmos sasa kutishana na kuumiza wagonjwa MUNGU hapendi tuna kz zingine na kilimo tuacheni
 
eh hii serikali haijawahi tokea tanguu kuumbwa kwa taifa la tanzani!! yaani wanawadanganya wagonjwa hamna mgomo, wagonjwa wanaenda hadi hosp alafu hakuna matibabu!!?? hivi wanajiskiaje?? wana lipi lingine la kusema?? dah kweli udhaifu wa serikali umejidhihirisha wazi wazi sasa
 
Ni kwa faida ya nani kudanganya eti madaktari wamerejea kazini kumbu hakuna hio kitu! Hivi serikali hii ni lini itaacha kuwaona watanzania wajinga?
 
Kwani wizara ya afya mbona kimya?au nao wako kwenye mgomo
 
huu usani wa maisha ya watu sio nzuri serikali ije na jibu la maana na wala sio bala bala
 
jamani ni ukweli muhimbili kuna mgomo baridi mkali sana. nendeni mawodini hasa wodi ya mwaisela iliyokuwa inajaa wagonjwa hadi kwenye korido. ni kweupee hakuna wagonjwa ndugu wamebeba wagonjwa wao wote kwa sababu huduma hamna. mgomo baridi ni mbaya sana kwa madaktari walahi wagonjwa wakiona cha mtemakuni.
 
Back
Top Bottom