Huduma za kisanii za CRDB

canaan

Member
Mar 1, 2008
46
6
Majuzi CRD Bank wameanzisha huduma ya Tembo card master card. Huduma hii
ilizinduliwa kwa mbwembwe na majigambo ya aina yake. Kama kawaida ya
watanzania tunapenda sana sifa ya kwamba sisi ndio kwanza kutoa kitu
fulani, lakini huduma zinazoendana na kuwa wa kwanza is virtually
zero.

Baada ya kusikia majigambo yao, na ukizingatia hii huduma nilikuwa
naitaka sana ili niweze kufanya online transactions; nilichangamkia
kuchukua Mastercard ya Tembo na kuweka vijisenti kadhaa ili niweze
kununua vitu mbalimbali hasa Amazon. Nilishangaa kwamba kadi yangu
ilikuwa haitambuliwi.
Nikachukua jukumu la kwenda kwenye tawi langu ili kujua kulikoni;
nilipofika mapokezi nikamkata dada mmoja na kumwambia tatizo langu na
kumuonyesha kadi yangu. Baadae akaniambia siwezi kufanya transaction
mpaka nijaze fomu ambayo nitailipia shilingi 1000 kwa mwezi; nikasema
sawa na akanipa fomu nikajaza, Baadae akaipeleka kwa boss wake na kuja
na jibu kwamba Tembo Mastercard haifanyi online transaction bali ni
Visa Card.
Nikashangaa sana vitu viwili:

1. Kwa ufahamu wangu, mtu anayekaa/handle Inquiries lazima awe
knowledgeable na huduma zinatolewa na benki, na sio mtu wa ku-
mislead wateja na kuwapotezea muda wao. Hapo sio mahali pa kumuweka
staff aliyepo orientation
2. CRDB msipende sifa za kuwa kwanza kutoa huduma fulani wakati hakuna
kinachoendelea. Benki makini inayoendeshwa na watu makini inajipanga
na kuhakikisha kwamba inapoanzisha huduma fulani panakuwa hakuna
porojo tena - only for the customer to see results and enjoy the
product - vinginevyo utawala wa benki unaonekana kama una walakini.
 
CRDB ni bank ya kisanii, jamaa wana-bank charges ambazo zingine hata hazijuliknani ni za nini hasa, jamaa yangu alinilalamikia kuwa anataka kuhama nimshauri ni bank gani wapo honesty kumuuliza akanipa msululu wa bank charges kwa mwezi jumla ni kama
  1. Monthly salary commission Tzs 3,000
  2. Monthly Maintanance fee Tzs 700
  3. Monthly Internet banking fee Tzs 1,000
  4. Online purchase ability monthly Tzs 1,000
  5. Any ATM withdrawal Tzs 700
  6. Any online purchase charge
Ukiangalia msululu wa hizi gharama yaani kuna fixed amount ya karibia Tzs 6,000 anakatwa kila mwezi zidisha mara 12 unakuta kwa mwaka ni kama Tzs 72,000 fixed anakatwa, plus kwenye drawing ambapo hufanya twice a week ni kama Tzs 1,400 mara wiki 52 kwa mwaka ni kama Tzs 72,800 plus online purchase yaani wanachukula karibia Tzs 160,000 kwa mwezi sasa yeye analalamika kuwa huu ni mshahara wa mtu huu. Halafu ukija kwenye interest analipwa zero kwa mwaka, wakati pesa yake wanaifanyia kazi kukopa watu na aliwahi kuomba mkopo wakampatia masharti magumu kweli akashindwa. Yaani jamaa wa CRDB wanakagua accounts za watu na kuona kuna kiasi gani ili waweke charge gani ili kuhalalisha kuchukua some amount.
 
Front staff kwenye CRDB Azikiwe branch na branches nyingine nyingi tu nilizowahi kufika ni horrible. customer service yaani ni ZERO!! Ni bora yaani hata umkute male staff staff kuliko hao akina dada ndio na attitude zao yaani inatia wazimu. Sasa sijui tatizo ni kutolipwa vizuri ama just a cheap, stinking negative attitude.
Lakini all in all banks nyingi bongo customer service ni ZERO esp. hao front staff
 
hivi hawa tellers wanalipwa sh ngapi? Mbna wanapozi,malingo kujisikia hasa wadada
 
Huwa sibembelezi mhudumu wa aina yoyote kwa sababu yeye ndy anatakiwa anibembeleze, kwenye matawi yangu wananifahamu vyema: akinizingua tu nachoma kwa meneja wao. Sisi watz wakati mwingine tunawapa vichwa hawa wahudumu; tunapenda sana kubembeleza huduma-tunakuwa wadogo na wapole kwa watu wanaotakiwa kutuhudumia kwa moyo mweupe! Hata wahudumu wa baa nao huringa ati! mwe
 
Huwa sibembelezi mhudumu wa aina yoyote kwa sababu yeye ndy anatakiwa anibembeleze, kwenye matawi yangu wananifahamu vyema: akinizingua tu nachoma kwa meneja wao. Sisi watz wakati mwingine tunawapa vichwa hawa wahudumu; tunapenda sana kubembeleza huduma-tunakuwa wadogo na wapole kwa watu wanaotakiwa kutuhudumia kwa moyo mweupe! Hata wahudumu wa baa nao huringa ati! mwe


Unaenda kumstaki mdada kwa bos wakati mdada analiwa na huyo boss,, unategemea nini?
 
Back
Top Bottom