Huduma mbaya za chuo kikuu huria cha tanzania

UniqueTanganyika

New Member
Mar 21, 2008
4
0
Nina masikitiko makubwa kutokana na huduma ya chuo kikuu huria cha Tanzania kwa wanafunzi tuliopo nje ya nchi.Chuo kimeshindwa kujiwekea mipangilio mizuri hususan katika ufanyaji wa mitihani.
Wanafunzi tuliopo nje tunalipa pesa nyingi kama gharama ya usimamizi na utumaji wa mitihani hiyo ila kwa kweli uongozi wa chuo,pamoja na kuwa mawasiliano ya mtandao,wanashindwa kutoa ushirikiano mzuri kwa wanafunzi wao.Kwa kweli hii inasikitisha sana kwani ni bora wangekuwa wazi kuwa si rahisi kwa mwanafunzi wa chuo chao kufanya mitihani nje ya nchi badala ya kuahidi bila utekelezaji.

Nina mapendekezo kwa mkuu wa chuo kuwa ahakikishe kuwa anaweka watu makini na wenye utaalamu mzuri katika kompyuta kushughulikia utumaji wa mitihani.Sidhani kama vyuo vingine huria duniani wana matatizo kama haya.Hii ni aibu kubwa sana sana kwani imekifanya chuo kuonekana na hadhi ya chini kulinganisha na vyuo vikuu vingine kiasi ambacho hata watu wanahoji kama kweli degree zinazopatikana hapo zina ubora.

Swala lingine ni utaratibu ktk ujajazi wa assignments pamoja na mitihani kwenye ripoti ya maendeleo ya mwanafunzi.Hapa napo wafanyakazi wa chuo hawapo makini katika hili kwani unaweza ukawa na nafasi zilizo wazi na ukiuliza unaambiwa labda ulikosea anwani.Kwa watu wanaotumia kompyuta ktk kuandaa assignments zao,hutengeneza ukurasa wa kwanza ambao huwa na jina la mwanafunzi,jina la kituo,anwani,namba ya usajili,namba ya simu na somo.Unachofanya hapa ni kubadilisha somo tu lakini taarifa nyingine hubaki vilevile.Sasa kama assignments nyingine zimefika kwa anwani hiyo iweje nyingine uambiwe umekosea anwani? Hapa chuo kinatupa wakati mgumu sana.
Naomba hapa uongozi wa chuo ufanye kama ni LAZIMA kila mwanafunzi alete assignments zake zikiwa na nakala na vilevile ni LAZIMA kwa mfanyakazi wa chuo anayepokea assignments hizo aweke sahihi yake pamoja na muhuri wa kukiri upokeaji.IWE NI LAZIMA kwani wengi wao wakiambiwa wasaini kukiri upokeaji wa assignments hukataa, kwanini?

Tafadhali mkuu wa chuo ajiri watu wenye uzoefu ili kukinusuru chuo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom