Hoyce Temu na Wabaguzi Mamboleo!

kaka picha tumeziona! moja ni kama hoyce yuko keroro halafu anauliza yani nyie mnasema mimi nimelewa?
yapili sijui ndo kashika bia au pochi haionekani vizuri ni kama imeungwa vile!


ila kaka pamoja na kuosha macho unataka kutueleza nini juu ya picha hizi hasa hapa kwenye jukwaa la siasa?
niwaeleze nini, kwani nini maana ya picha....picha zinajieleza kama huelewi usikonde saa zingie ubongo wa watu tofauti unachukua muda kuelewa mambo tofauti, lkn naamini baada ya kuziangalia sana utazielewa wengine haiwachukui muda sana, lkn ndio hivyo......
 
niwaeleze nini, kwani nini maana ya picha....picha zinajieleza kama huelewi usikonde saa zingie ubongo wa watu tofauti unachukua muda kuelewa mambo tofauti, lkn naamini baada ya kuziangalia sana utazielewa wengine haiwachukui muda sana, lkn ndio hivyo......

kaka nashukuru baada ya kuchukua muda nimeona nipokee tafsiri ya jamaa hapo juu kuwa ni hoyce analia kupinga ushindi halali wa miss tanzania 2007. maoni yangu nishatoa hapo juu. we ya kwako ni yapi?
 
comrade asante kwa hilo.. tena hapo is more interesting. Binti mwenyewe kasema hata huko India hajawahi kufika, nafasi ya kwanza kwenda nje ya nchi ni pale alipoenda kuiwakilisha Tanzania kule Philipines.. sasa sijui afanye nini ili awe Mtanzania maana hata akiolewa na mtu mweusi bado yeye ni Mhindi, hata akila ugali na maharage yeye ni mhindi tu, akivaa kanga na kujipaka wanja, akizungumza kiswahili kama mndengereko (tena binti anazungumza na kisukuma pia)... haitambadili ataendelea kuwa Mhindi tu.. njia pekee ni yeye kuhama Tanzania na kurudi Goa (ambako hana ndugu!) ili akae na watu wanaofanana na yeye!
 
Nasikitika kwamba mijadala ambayo inahitaji uchambuzi wa kina tunaijadili kwa mitizamo ya ki layman mno.Mada hii imeanzia kwenye makala ya mwanakijiji, ukiisoma vizuri mbali ya kuwa alilenga kujadili suala la Ms tz, kajenga hoja kwa mifano mingi ambayo kimsingi ina rise maswali magumu kuliko majibu.Nina hakika hata yeye kuna mambo mle ukimstukiza hawezi kukujibu kwa haraka. We need to think beyond the horizon, suala la uyu dada halina ubishi ni mtanzania na ana haki zote za kutuwakilisha. Tunaweza lakini kwenda mbali ya hapo na kujadili mambo mapana zaidi kuhusu ili suala nje kabisa ya huyu dada. kwa kizungu naweza sema 'we take the topic in broad context and discuss it objectively'' si suala la ubaguzi kabisa hilo ila kujielimisha zaidi, mimi napenda kutumia msemo wa 'think big' Msinifanye niamini JF ni mahala pa 'kupiga soga tu'(quote from http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=66652#post66652) au kutafute easy answers to hard questions,we can do more than that wazee.
 
Bwana Mdogo, unajua kule Bungeni kitu kimoja Spika Sitta alikuwa anakifanya mara nyingi ni kuwalazimisha wabunge wastick kwenye hoja. Walipokuwa wakijaribu kutoka kwenye hoja (hasa wakati bunge limekaa kama kamati ya matumizi) alikuwa akiwaambia subirini "Mshahara wa Waziri".

Hoja tunayoizungumza hapa ni rahisi na iko wazi. Richa Adhia alichaguliwa kuwa Miss Tanzania wiki iliyopita. Richa wazazi wake wana asili ya nje ya Tanzania yaani India. Hivyo Richa hana maumbile ya watu weusi. Alipochaguliwa kuna watu walioneshwa kukasirishwa na kitendo hicho kwa vile aliyechaguliwa siyo "Mtanzania Halisi" na wengine wakidiriki kusema siyo "Mzawa" ingawa binti mwenyewe na wazazi wake wote ni wazaliwa wa Tanzania.

MMoja waliokasirishwa na kitendo hicho ni aliyewahi kuwa Miss Tanzania 99 Hoyce Temu ambaye aliangua kilio na kudai kushangazwa kuwa licha ya kuwepo watu weusi wengi (ambao yeye aliwaita waafrika) kwenye mashindano hayo ikawaje achaguliwe "mhindi". Maneno hayo yakarudiwa na watu kadhaa mitaani na hata humu JF.

Watu wakatoa sababu zao kwanini Richa hastahili kuwa Miss Tanzania, na sababu kubwa na iliyo dhahiri ni kuwa "hawakilishi Watanzania hasa, ukilinganisha kama angechaguliwa Mtanzania Mweusi".

Sasa wewe unaweza kuamua kuzungumzia wahindi na historia yao, familia za kIhindi, unaweza hata kuandika hadithi kuhusu wahindi yote hiyo katika jitihada za kuweka mada katika "broader context". Tatizo ni kuwa, hatuzungumzii wahindi wote, na wahindi wote hawakugombea Miss Tanzania, na si wote walichaguliwa kuwa Miss Tanzania. Kuna binti mmoja ambaye ameshinda tuzo hiyo na ambaye anajisikia kutengwa na nchi ambayo amezaliwa ndani yake, amekulia, amehangaika nk... kisa na mkasa yeye ni "mhindi tu".

Ukitaka kuzungumzia masuala ya wahindi au jamii nyingine anzisha mada, lakini hili la Richa is well defined. Je, unaamini kuwa kitendo cha kumchagua Mtanzania mwenye asili ya Uhindi kuwa Miss Tanzania na kuliwakilisha Taifa letu kwenye mashindano ya dunia ni kosa, ingebidi achaguliwe Mtanzania mweusi?
 
Hivi huyu Binti alianza kuwa Mhindi pale aliposhinda U Miss?

Kama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urembo tayari alikuwa mhindi mbona hayakuwa makubwa?

Unajua nini!
Tukisha maliza kuwabagua wahindi na waarabu tutaanza kubaguana wenyewe kikabila.
Tukimaliza ubaguzi wa kikabila tutaanza wa kiukoo.
Tukimaliza wa kiukoo tutaanza wa kifamilia.
Tukimaliza wa kifamilia tutakuwa tumejimaliza wenyewe maana kila mtu katika familia itabidi Ajiju.

Ubaguzi wa namna yeyote ile ni lazima upigwe vita tena uogopwe kama kufunua vazi la mzazi wako.
 
madilu... hawaelewi ndugu zetu wabaguzi.. ndio maana leo Hoyce anakuja na kubadili vigezo ati sasa siyo rangi ni umbo...!!
 
Duh, haya mambo ya nani mtanzania zaidi kushinda mwingine hayatatufikisha popote. Ni kweli kuna wahindi mafedhuli tena wasio na adabu na kule wale walio-fair na ku-play by the rules ktk shuguli zao za kimaisha. Sasa ku generalize watu hawa as a single collective group sio sahihi...ni makosa na ni UBAGUZI!!!!. Hivi mie na swali hapa, je EL, Karamagi na na timu nzima ya mahayawani wa ccm nao kwani pia ni wahindi??. Kumezuka ubaguzi usio na kichwa wala miguu huko bongo, ebo.......na jamaa yangu mmoja alikuwa analalamika kwamba watu wa kabila lake la kichaga walimbagua kazini kwasababu tu hatoki kijiji au eneo moja na hao jamaa. Mambo ya namna hii, uongozi mbaya na mandembwendembwe mengine ndio yanazamisha MV. Bongo. Kuna wahindi wanatoa mchango mkubwa sana ktk ujenzi wa taifa......tunao madaktari wazuri tu, maprofessor ktk baadhi ya vyuo, enginners na taaluma nyingine nyingi....sasa wakosaji wanakuwa kwenda kundi moja no matter jina lake ni Patel au Karamagi. Say no to RACISM!!.
 
Mi naomba kuuliza hivi ni halali mtu kuhukumiwa kwamba hajui KIINGEREZA? maana english imekuwa kigezo kikubwa sana si katika katika miss TZ pekee yake, bali hata ajira na kazi. Je hi ni halali? inaeleweka kweli kwamba English in Tanzania is a second language, sasa iweje watu wahukumiwe kwamba hawajui kiingereza? Mi naona hiki kigezo ni cha kizandiki, kwanza tuna lugha yetu kwa nini tusijivunie hii lugha ya kiswahili? Mpaka tupime intelectuality ya watu wetu kwa kutumia lugha ya kigeni? Na tulivyo wanafiki Tanzania, tunawalaumu wazazi wanaopeleka watoto wao nje kusoma kiingereza kwenye shule za msingi. Wakati kiswahili hatukithamini. What hypocricy? Mtu akienda kuomba kazi, its normal kuambiwa kwamba kashindwa interview kwa sababu hajui kiingereza, basi kiswahili tukifute tubaki na hiki kiingereza maana naona hakitusaidii.

Na does it mean kwamba wote wanaoenda kwenye haya mashindano kutoka sehemu mbali mbali duniani wanajua kiingereza fasaha? Hapana, mi nasema watanzania tuache unafiki. Siamini kwamba China, India, Brazil, Mexico nk wanatumia kigezo cha lugha hii ya kiingereza. Kwa mwendo huu hatuwatendei haki watu wetu. Jiulize leo ukae Angola na baada ya mda mfupi upewe mtihani kwa kireno na ushindanishwe na mtu aliyesoma kireno maisha yake yote. Naamini hapa jibu mnalo!

Kama huyu dada alishinda kwa kutumia kigezo cha kujieleza kwa lugha ya kiingereza, Naungana na Hoyce Temu kuukata huu uzandiki. Haina maana ya kuwa na lugha ya taifa ambayo hata nyumbani kwetu haikubaliki. Its sheer stupidity kudhani kwamba mtu kuwa exposed ni lazima aongee kiingereza kizuri.

Unategemea mdada wa miaka kumi na nane au ishirini wa Mara, Ruvuma, Mwanza nk aliyekulia upcountry aongee vipi kiingereza fasaha? na ashindane na mtu aliyesoma academies za kiingereza tuu? Mi hapo ndo nachoka na nchi yetu, yaani wote tumekuwa wasanii, kuanzia viongozi mpaka wananchi wa kawaida.

Its distgusting.
 
Masanja, una uhakika huyo dada amesoma academies? Hivi mnataka kuniambia hakuna watanzania wanaoweza kuzungumza Kiingereza kuliko huyo dada? Yeye kujua kiingereza siyo kosa ni mojawapo ya lugha za Taifa!.. Je, huyo dada aliulizwa kwa kiswahili akajibu kwa kiingereza? Je, washindani wengine walijua kuwa mashindano yatahusisha na uzungumzaji kiingereza? Kama walijua na hawakuwa tayari kuzungumza kiingereza hadharani kwanini wasipinge mapema matumizi ya Kiingereza?
 
Hili suala la lugha hebu tuliweke sawa kidogo. Kama angechaguliwa mtu ambaye kiingereza hakipandi, halafu baadaye wanaenda Sanya, China kwenye Miss World, hivi anafikiri ataulizwa maswali kwa Kifipa? As a matter of fact, lugha rasmi za Tanzania ni Kiingereza na Kiswahili na hili liwe changamoto kwa wale wote wanaotaka kugombea Umiss "wherever" bora wapandishe kiingereza chao na hata lugha nyingine za ziada. Hebu fikiria kama angekuwepo binti kati yao ambaye amepandisha Kiingereza na Kifaransa, halafu akijibu anajibu kwa kiingereza halafu anachombezea na kifaransa kidogo, huoni huyo angescore juu kuliko hata Richa!?

Kama tatizo ni kuwa wengine kiingereza kimekuwa "maimuna" sasa kwanini wamlalamike Richa? Sasa walitaka Richa naye azungumze kiingereza cha kuvunja vunja ili alingane nao?

Duh! Mnapoandika muwe na facts za mnachoandika jamani! Mimi nimeshaangalia mara chungu nzima hiyo Miss World/Universe ambapo kuna washiriki toka nchi mbali mbali ambazo hawazungumzi ung'eng'e. Hivyo huwa wanakuja na wakalimani wao ambao watatafsiri swali toka kiingereza kwenda kwenye lugha yao, na majibu kuyatafsiri toka kwenye lugha ya mshiriki kwenda kwenye kiingereza. Nimeshaona washiriki wengi wa Venezuela, Colombia na nchi nyingi za East Europe wakifanya hivyo. Hivyo kwa mshiriki wa Miss World/Universe kutozungumza kiingereza IT IS NO A BIG DEAL AFTER ALL!
 
Nyangumi, yaani wahindi wakioana na watu weusi ndio wanakuwa raia zaidi?

Mkjj Narudia tena swali langu kwako:
Kumbe hilo wewe unaliona ni dogo!? Maana kama hawajioni wao ni bora kuliko wamatumbi kwa nini wasiolewe na kuwaoa!? Kama unazaliwa na kuishi Tanzania miaka nenda rudi kwa nini wengi wao hawawezi kuzungumza lugha yetu ya Taifa!? Kama hawajioni wao bora kuliko sisi kwa nini wanaishi maeneo ya kujitenga 'uhindini' na hatuwaoni wakiishi uraiani? Shilingi ina pande mbili angalia zote na utaweza kuona nani aliyeanza ubaguzi kati ya wahindi na wamatumbi. Ukijibu maswali hayo unaweza ukafikia hitimisho nani mbaguzi kati ya mhindi na mmatumbi.
 
ngojeni afanye vizuri huko miss world, mtaona anavyomwagiwa sifa za "mtanzania mwenzetu",... Hatukawii kusahau, majuzi tu Allan Johnson (wa BBC)watu humu walimwita "mtanzania mwenzetu", kisa; kazaliwa Lindi!!!
 
Mwanakjj, huyu dada sijui alisoma wapi, ila nina uhakika hakusoma shule kama niliyosoma mimi ya huko usukumani. Naomba nikuulize. Hivi kweli inawezekana miss France akaulizwa maswali kwa kiingereza au kispaniola? Jamani hapana tufike sehemu, tujitambue. Mi sina ugomvi na huyo Mtanzania mwenye asili ya kihindi kuwa miss TZ, concern yangu ni kiingereza kutumika kama kigezo. Why?

Watu watasema ni utandawazi, ni utandawazi gani huo uwa-athiri maskini kama TZ na sio China, Japan, France nk? Jamani so far Kiswahili is our remaining idendity, sasa tukikiua, tutabaki na nini? ndo maana mpaka leo hata sisi hatuwezi kuongea au kuandika sentensi mbili bila kuchanga na kiiengereza. As a result vyote kiingereza kwa kiswahili, HATUJUI.
 
Perhaps, What Mkjj is trying to project ni kwamba wahindi wakitubagua its ALRIGHT ila sisi tusiwabague. I agree with that kwamba ubaguzi ni kitu kibaya, ila maoni mengi humu yanaonyesha hisia za wananchi walio wengi. Tatizo ni kwamba ubaguzi upo na wengi wanajua hivyo hata MKJJ anajua, ila sasa inapokuja kuuongelea inakuwa kigugumizi. Tunabaki kukimbilia wosia/hoja za mwalimu Nyerere.

Hakuna watu wabaguzi kama wahindi katika TZ yetu. Ni medeal na kesi nyingi sana za hawa jamaa wanavyowanyanyasa vibarua wa kizalendo bongo. Ofcourse sio wote ila wengi wao wanatuona weusi ni malofa wa kutupwa kuliko hata ngedere. Personally from my experience in public interests work in Tz, I have VERY mixed feelings about this people in my country. Na sitaki kuwa mnafiki katika hili, hawa jamaa wanatudharau sana, ingawa tena dawa ya hili sio kuwabagua, ila inabidi tujaribu kuadress hili tatizo. Hebu Mwanakjj kama unaweza kafanye utafiti huko kwenye viwanda vya wahindi Mbagala, Chang`ombe nk conditions are extremely horrible. I tried, ila nilishindwa kwa sababu nilikuwa nafanya public ionterests work sikuwa na hela ya kuhonga mbele, So IDIDNT SUCCEED. I battled them na mwishoni unagive up. They tend to be so corrupt. Kifupi, I dealt with them and I never liked the experience.

Lastly, maoni mengi humu ni reflection ya hisia za walio wengi katika nchi yetu especially wafanyakazi viwandani na kwingeneko. Ila naomba nieleweke kwamba situmii historia hii kumhukumu Miss TZ wa 2007. My prob. Is kwa nini kiingereza kiwe kigezo? haileti mantiki.
 
ngojeni afanye vizuri huko miss world, mtaona anavyomwagiwa sifa za "mtanzania mwenzetu",... Hatukawii kusahau, majuzi tu Allan Johnson (wa BBC)watu humu walimwita "mtanzania mwenzetu", kisa; kazaliwa Lindi!!!

Mimi msimamo wangu utakuwa ni kama ulivyo. Sigeuki nyuma nikawa jiwe. Hawa watu wanaubaguzi wa hali juu tena kibaya zaidi wanaufanya kwetu dhidi ya wazawa, lakini watu hawataki kuuona huo wala kuuzungumzia wanataka kuzungumzia ubaguzi aliofanyiwa yeye tu!
 
nyinyi wote mnazungumzia "hawa watu" sijui "wahindi vile au hivi" huo ni mjadala mwingine, hamjajieleza vya kutosha kwanini binti huyu specifically, asiwe miss Tanzania? Msianze kusema makosa ya jamii nzima mumwadhibu yeye? Je, binti huyu amewahi kuwabagua watu weusi, je binti huyo alikuwa anajitenga kwenye mashindano n.k mtaendelea kupiga kelele "wahindi hivi au vile" haifanyi kuwa hoja yenu ya kumbagua huyu binti iwe na nguvu!

Mnaweza kusema "wahindi walitunyima mihogo" au "wahindi hawakutupa maji ya kunywa" kuwa ni wabaguzi wakubwa hilo lote sawa na mimi naelewa na ninafahamu kuna wahindi ambao wana tabia hizo za kibaguzi tena si kidogo! Hilo wala siyo mjadala, mjadala ni Richa Adhia amefanya nini cha kibaguzi ambacho kinamfanya asistahili kuwa Miss Tanzania? Hadi hivi sasa hakuna aliyethubutu kutuonesha japo kitu kimoja isipokuwa porojo za "wahindi wako hivi ohh wahindi wako vile"

Give me some undisputable facts kwamba Richa Adhia hastahili kuwa Miss Tanzania kwa vile amefanya hivi au vile au hakufanya hivi au vile!! haya ya 'wahindi wabaguzi' I have had enough.. stick to the topic..

Kwa nini Richa Adhia, aliyekuzaliwa na kukulia Tanzania anayezungumza Kiswahili, Kiingereza, Na Kisukuma (sijui alijifunza shule gani Kisukuma!!) ambaye hakuna hata mahali pamoja ametoa kauli za kibaguzi (at least not in public) au amefanya kitendo chochote cha kuwadhalilisha watu weusi, asiwe Miss Tanzania? Can i make this question more pointed than that?
 
nyinyi wote mnazungumzia "hawa watu" sijui "wahindi vile au hivi" huo ni mjadala mwingine, hamjajieleza vya kutosha kwanini binti huyu specifically, asiwe miss Tanzania? Msianze kusema makosa ya jamii nzima mumwadhibu yeye? Je, binti huyu amewahi kuwabagua watu weusi, je binti huyo alikuwa anajitenga kwenye mashindano n.k mtaendelea kupiga kelele "wahindi hivi au vile" haifanyi kuwa hoja yenu ya kumbagua huyu binti iwe na nguvu!

Mnaweza kusema "wahindi walitunyima mihogo" au "wahindi hawakutupa maji ya kunywa" kuwa ni wabaguzi wakubwa hilo lote sawa na mimi naelewa na ninafahamu kuna wahindi ambao wana tabia hizo za kibaguzi tena si kidogo! Hilo wala siyo mjadala, mjadala ni Richa Adhia amefanya nini cha kibaguzi ambacho kinamfanya asistahili kuwa Miss Tanzania? Hadi hivi sasa hakuna aliyethubutu kutuonesha japo kitu kimoja isipokuwa porojo za "wahindi wako hivi ohh wahindi wako vile"

Tena mnaweza kulalamikia lugha iliyotumika katika mashindano hayo nk lakini hamjaonesha kama hao warembo walijua kiingereza kitatumika au walishtukizwa. Kabla ya mashindano niliona interviews zao wakiwa kambini na walihojiwa na waandishi kwa Kiingereza na Kiswahili HAKUNA hata MMOJA aliyesema kuwa lugha ya kiingereza haimudu na angependa ahojiwe kwa Kiswahili akakataliwa!

Give me some undisputable facts kwamba Richa Adhia hastahili kuwa Miss Tanzania kwa vile amefanya hivi au vile au hakufanya hivi au vile!! haya ya 'wahindi wabaguzi' I have had enough.. stick to the topic..

Kwa nini Richa Adhia, aliyekuzaliwa na kukulia Tanzania anayezungumza Kiswahili, Kiingereza, Na Kisukuma (sijui alijifunza shule gani Kisukuma!!) ambaye hakuna hata mahali pamoja ametoa kauli za kibaguzi (at least not in public) au amefanya kitendo chochote cha kuwadhalilisha watu weusi, asiwe Miss Tanzania? Can i make this question more pointed than that?
 
Mimi msimamo wangu utakuwa ni kama ulivyo. Sigeuki nyuma nikawa jiwe. Hawa watu wanaubaguzi wa hali juu tena kibaya zaidi wanaufanya kwetu dhidi ya wazawa, lakini watu hawataki kuuona huo wala kuuzungumzia wanataka kuzungumzia ubaguzi aliofanyiwa yeye tu!

Richa Adhia alimbagua nani hadi yeye abaguliwe? na hawa wazawa unaowazungumzia wewe ni kina nani hawa?
 
Mwanakijiji,
Kweli si sawa kubagua binadamu kutokana na rangi zao na msimamo wangu pia ni huo. Ila nina haya machache ya kukufafanulia kabla ya kutupa lawama kwa watanzania weusi au na watu weusi kwa ujumla.

MOJA:ANZA KWANZA NA WAHINDI
-Maneno uliyoyasema yapeleke kwanza kwenye jamii ya wahindi hasa pale nyumbani Tanzania, na uwaeleze kwa kinaga ubaga kuwa watu weusi siyo sub-humans au manyani au makuli au wafanyakazi wa nyumbani! bali ni watu kama binadamu wengine ambao wanastahili haki na heshima kama binadamu wengine wenye rangi isiyo nyeusi na kwamba kujichanganya nao si kujishushia hadhi,au kuzungumza lugha yao ya kiswahili kwa ufasaha si kujiaibisha! au hata kusali nao si kupotea!.WAKIKUELEWA,basi ndiyo geukia kwa watanzania weusi ambao kwa karne nyingi sana wamekuwa ni victims wa sera hizo mbovu za kishenzi na kibaguzi!
Hiyo reaction unayoina baadaya ya huyo binti kushinda au kupewa hilo taji ni mwangwi(reflection) wa mambo ambayo watanzani weusi wamekuwa wakifanyiwa na wahindi na waarabu kwa miaka mingi mno.Hebu tu ndugu yangu MwKjj jiulize ni wahindi wangapi ambao wamefungwa jela Tanzania kwa makosa mbalimbali? je ni kweli watanzania weusi tu ndiyo wanastahili kwenda jela? je hii ni haki? je hii haituambii kitu kuhusu rangi zetu nyeusi? sasa mimi si shangai hata kwenye urembo yakawa ni yale yale kuthamini wahindi kuliko dada zetu!

PILI: TOFAUTISHA HALI YA ILIYOKO TANZANIA NA ULAYA AU MAREKANI!
Sikubaliani kabisa na mfano uliutoa kuhusu mtu mweusi kuongoza jeshi la marekani.Yule bwana alikuwa hana sauti yoyote ile kwenye jeshi lile, alikuwa tu kama bendera ikisubiri upepo ndiyo ifuate.Alikuwa anatumiwa tu na kundi la weupe ili kufanikisha sera zao.Hii mbinu mbona si mpya! na wengi wataamini kuwa ni kweli hawa mabwana weupe si wabuguzi kwa kuwa wamemchagua mtu mweusi kuwa mkuu wa majeshi kumbe wao wana monitor the whole situation in the background!
Kwa Tanzania si hivyo,sisi tukimchagua kwa mfano daruwashi au yule mu Iran kwenye serikali yetu tunampa nguvu zote za kisiasa! kwa hiyo mifano yako naona haiangalii hali halisi nchini TZ.Hata UK na nchi nyingine za Ulaya, ujanja ni huohuo kwamba chagua mtu mweusi mmoja au minority mmoja mpe madaraka lakini hatakuwa na sauti ya mwisho bali ni wale wenye rangi nyeupe ndiyo watakuwa na mamlaka juu yake!

TATU: INDIA NA PAKISTANI
Nadhani unaelewa ninini kinawapata wale wahindi wanaojulikana kam DALIT au untouchable ambao wengi wao wana rangi nyeusi! hawa wanabaguliwa na vilevile wanaonekana kama waafrika ambao walikwenda huko karne nyingi zilizopita nani kwamba hawana haki ya kushika nyazifa mbalimbali serikali mwao au kufanya baadhi ya kazi ambazo wahindi wengine wanazishika.Kazi zao ni zile za hali duni na ya chini eti kwa kuwa hawajatakaswa! Sasa huoni kuwa hawa mabwana ni wabaguzi toka huko kwao walikotokea? na kusema ukweli sijamsikia kiongozi yoyote yule Tanzania akikemea ubaguzi ambao wahindi wanaufanya kwa watanzania wenye rangi nyeusi! ila naona inakuwa ni rahisi kwa viongozi tangu enzi za Nyerere kuwalaumu tu watanzania kuwa ni wabaguzi.Wakati wahindi vilevile ni wabaguzi mara dufu.Hivi huoni kuwa hii ni double standard?????

Wembe,
 
Back
Top Bottom