Hoyce Temu na Wabaguzi Mamboleo!

Bro, hiyo sasa ni mada nyingine kabisa. Mimi nazungumzia suala la huyu binti, tukubaliane kwanza wale wanaosema kuwa hakustahili kuwa Miss Tanzania wanakosea kwani wanasukumuwa na hisia ya kutukuza nasaba na wana tendencies za kibaguzi. Tukubaliane pia kuwa Richa kama watanzania wengine anazo haki zote ambazo mimi na wewe tunazo (nothing more, nothing less). Tukishakubaliana suala la Richa, then tunaweza kuzungumzia suala la kushiriki kwa baadhi ya Watanzania kwenye mambo mbalimbali ili kuthibitisha utanzania wao. Tunakubaliana?
 
Point yangu haikuwa hiyo ya Utanzania ila issue ya ubaguzi.Hawa wahindi ni watu wanaojibagua wenyewe kabla ya wao kubaguliwa sasa inakuwaje sisi tujipendekeze kwa kama wao wanajiona si moja katika jamii yetu.Angalia kuoana,Misiba nk.Au masuala kama hayo si ubaguzi??
 
Bro, hiyo sasa ni mada nyingine kabisa. Mimi nazungumzia suala la huyu binti, tukubaliane kwanza wale wanaosema kuwa hakustahili kuwa Miss Tanzania wanakosea kwani wanasukumuwa na hisia ya kutukuza nasaba na wana tendencies za kibaguzi. Tukubaliane pia kuwa Richa kama watanzania wengine anazo haki zote ambazo mimi na wewe tunazo (nothing more, nothing less). Tukishakubaliana suala la Richa, then tunaweza kuzungumzia suala la kushiriki kwa baadhi ya Watanzania kwenye mambo mbalimbali ili kuthibitisha utanzania wao. Tunakubaliana?

Mwanakijiji,hapo tupo pamoja.Mie nakubali kama huyo binti ana sifa za kuwa miss,hilo halina mjadala,ni haki yake,kama kuna vigezo vingine ambavyo wanaona hakua navyo,hilo tena ni jingine.Binafsi sina utaalamu na mambo ya u miss,kwa hiyo mie nakubali na namuunga mkono aiwakilishe Tanzania,kwa wale wanaompinga kuhusu rangi yao,si busara kufanya hivyo endapo alikua na vigezo vyote vya kuwa miss.Hili lingine kuhusu ushiriki wa wahindi kwenye shughuli za kijamii limekuja baada ya hili la u miss kuleta mzozo,ndio wengine tumeona tutoe dukuduku letu tulilonalo.
 
Mwanakijiji: Mawazo yako katika hii article murua kabisa. Lakini nahisi hujamtendea haki Hoyce. Katika mahojiano aliyofanya jana ameeleza vizuri sana msimamo wake kuwa yeye hampingi huyu binti kwa sababu ni mhindi, bali kwa sababu taratibu zilikiukwa kuhusu vigezo vya umiss kama vile urefu na unene. Haya ndiyo maelezo yake, na amesisitiza kuwa anaendelea kupinga ushindi wa Richa not on the basis of her colour lakini on the fact kwamba vigezo ambavyo hutumika siku zote safari hii vilipindishwa. Sasa mimi nafikiri kum-condemn huyu dada (Hoyce) kwamba ni mbaguzi wa rangi ni kumuonea. Maybe uliandika hii article kabla hujasoma maelezo ya Hoyce Temu, yasome tena maelezo yake nafikiri yapo kwenye gazeti la Tanzania Daima la leo.

PS: Pokea pongezi kutoka kwa wananchi wa vijijini kuhusu makala yako, wamenitumia message nikupe ujumbe huu, wao wanasema mambo ya internet hawayajui wapo kijijini!
 
Mwanakijiji: Mawazo yako katika hii article murua kabisa. Lakini nahisi hujamtendea haki Hoyce. Katika mahojiano aliyofanya jana ameeleza vizuri sana msimamo wake kuwa yeye hampingi huyu binti kwa sababu ni mhindi, bali kwa sababu taratibu zilikiukwa kuhusu vigezo vya umiss kama vile urefu na unene. Haya ndiyo maelezo yake, na amesisitiza kuwa anaendelea kupinga ushindi wa Richa not on the basis of her colour lakini on the fact kwamba vigezo ambavyo hutumika siku zote safari hii vilipindishwa. Sasa mimi nafikiri kum-condemn huyu dada (Hoyce) kwamba ni mbaguzi wa rangi ni kumuonea. Maybe uliandika hii article kabla hujasoma maelezo ya Hoyce Temu, yasome tena maelezo yake nafikiri yapo kwenye gazeti la Tanzania Daima la leo.

PS: Pokea pongezi kutoka kwa wananchi wa vijijini kuhusu makala yako, wamenitumia message nikupe ujumbe huu, wao wanasema mambo ya internet hawayajui wapo kijijini!

Kitila nakusikia kaka, ila angalia maneno niliyoyasema hapo juu kuwa ubaguzi haukomi, ukikosa rangi unakuja kwenye umbo! Hoyce Temu alipohojiwa wakati anaangusha machozi alinukulikwa akisema hivi "“Hii siyo sawa, kulikuwa na Waafrika wenye sifa na walijibu swali vizuri tena kwa kujiamini, nashaangaa majaji wamemchagua Richa, wakati rangi yake haiwakilishi Utanzania,” Ilivyoripotiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda. Nina uhakika akiendelea kubisha watu watamchezea rekodi ya maneno yake!

Kwa vile tumeonesha ubovu wa fikra hizo ndio maana anageuka na kusema suala ni urefu na unene. Sasa angechaguliwa mnene mnene kweli na bado ni mhindi Hoyce angeangusha machozi kwa vile anatakiwa mwembamba? Halafu hizo taratibu zilizokiukwa ni zipi? NIliandika makala hiyo nikianticipate kuwa Hoyce atajirudi na kujisahihisha siyo kuendeleza maneno ya kubagua. Ndio maana nimesema hapo juu unless Hoyce au Lundenga watuoneshe hivyo vigezo vya urefu (maana sidhani washindani wote walikuwa na urefu sawa) na unene (sidhani pia kama wote walikuwa ni wanene) na vikakiukwa basi Hoyce anaweza kuwa na hoja. Lakini kama ni vigezo vya kufikirika basi tuna tatizo! nani ataweza kuwa miss Tanzania?
 
Nilikuwa sijui Hoyce alisema nini. Kama alisema kama alivyonukuu Mwanakijiji hiyo ni hatari kwa sababu maneno hayo ni ya kibaguzi. Sijui wakati anayatamka kama alitambua kuwa ni ya kibaguzi. Nakubaliana kabisa kuwa ubaguzi ni sumu mbaya sana. Hapa Hoyce ajitokeze na kuomba radhi mapema kwani hakuna "spin" yoyote ile itakayosaidia kwani watu si wajinga. Na kama Watanzania wengi wanaunga mkono hiyo kauli yake hiyo inatisha.
 
Mimi hakukataa, alikubali kabisa sema wazazi wake waliharibu. Ningejibebea kifaa cha kidosi :)
wOrM, wahindi wanajichanganya tu au sio, tatizo wabongo wengi wanaleta mapenzi ya ngwala teh teh. Peleka mtoto wa kihindi bustani cheza kuchi kuchi hoti hee....mamoa safi kabisa, yaani kama unasukuma mlevi. Kama mnataka wajichanganye, na nyie chichanganyeni eboo!!

Tena mmenikumbusha, kulikuwa na mwalimu fulani Mwanza alikuwa anaitwa Mwalimu Mbiti, mweusi, (watu wa Mlimani, Bugando/Pamba primary wanaweza kumjua), yeye mbona alioa mhindi?

Kitila Mkumbo nakubaliana na wewe. Kutokana na maelezo ya Hoyce Temu, watu wamemwelewa vibaya. Ila mwanamke mzuri hivyo anabubujika machozi kwenye kadamnasi kwa kitu hiki duuh...thats some messed up passion. Kwa mtihani uliowekwa hapo mbele yao, Richa ana deserve. Ndio maana sielewi warembo wa kibongo wanang'ang'ania kuongea kiingereza cha tuition na kukariri cha nini. Ongea kiswahili tu, weka mkalimani. Hata huko Miss World pelekeni mkalimani. Hata hivyo, ingekuwa kiingereza ni muhimu sana, basi mbona wangemsogeza Miss TZ UK aingie top 5? Maana binti articulate na angewafunika hadi huyo Richa.

Labda muweke vigezo vyote vya kuchagua Miss hapa, halafu ndo tuchambue Richa kafanikisha vipi. Confidence is one of them am sure. Kwa uzuri walikuwepo wazuri zaidi yake, but she had the 'best' package I guess.
 
Watanzania wenzangu tusiwe wepesi wa kudanganyika na siasa za wote ni Watanzania.

Pamoja na maelezo mazuri ya Mwanakijiji, pia ni kweli kuwa kutakuwa na hoja tofauti jinsi kila mtu anavyoona inafaa.

Kama alivyosema mwana JF mmoja hapo juu, haifai kufananisha Unaigeria na Uhindi.

Ni muhimu tufahamu kuwa hata kama wote waliopata uraia wa kununua watajiita Watanzania lakini bado kuna Mtanzania halisi asiye na kwingineko zaidi ya Bongo...yaani mzalendo, achana kabisa na mipaka iliyowekwa na wazungu ili kurahisisha utawala wao. La sivyo African continent ingegawanyika ktk viinchi vya kabila moja moja kma vitaifa vidogo. Lakini bado kwa context ya rangi African continent refers to black colour people. Waarabu, Wahindi, Wazungu ni wageni tu. Angalia yaliomkuta Camila na Prince Charles na hayati Diana....yote haya ni kupigania asili.

Hawa wahindi wanaotunganya kuwa ni Watanzania, mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wengi walihamishia familia zao kwingineko hasa kwenda India, Canada, USA na UK. Lakini watanzania halisi hata wale wenye pesa zao walibaki hapa hapa.

Mwisho, naamini kama kuna mtanzania atakwenda kwenye mashindo ya aina hii na akajitambilisha kuwa atatumia kiswahili kujieleza ataruhusiwa tu kwani Miss world hawana lugha rasmi na kukataza lugha nyingine. Ni utumwa wetu wa kifikra ndio kinacho tufanya tusiamini kuwa Kiswahili hakitambuliwi.

Last but not least...Nilisikitika sana kuwa TFF wameandaa tiketi za mechi ya kirafiki kati ya Uganda na Tanzania zilizoandiwa kwa kiingireza...ingawa watumiaji wengi Kiswahili ndio lugha yao ya kwanza kabla ya kiingereza.

Tunahitaji kujikomboa kifikra ili hata mataifa ya nje waone kweli kuwa Kiswahili ni moja ya utambulisho wetu.

Ndimi,
Nsololi
 
African beauty ya Tanzania itaonyeshwa wapi,kama hawa watu watatuwakilisha.Kuna sehemu zingine lazima ziwakilishwe na watu asili kama ni ubaguzi wacha waite hivyo.Sehemu kama ya umiss mie sikubaliani kuwakilishwa na watu wasio na asili.Huo ndo mtazamo wangu.
 
Bwana mdogo, hebu kwa dakika chache tuzungumzie hii "asili". Wanaposema asili yake wana maana ya mtu ambaye asili yake si Afrika au inamhusu mwenye asili ya India peke yake? Je, kama Richa angekuwa ana asili ya Ulaya wangekubali? Sasa kama tatizo ni "asili yake" ni wangapi watanzania ambao asili yao ni nje ya bara hilo? Hivi umewahi kukutana na Wairaqw wa mikoa ya mbulu ukiwaona unajua kabisa wana damu ya nje ya Bara la Afrika, je wanastahili kugombea Umiss Tanzania? Vipi kama huyo binti angekuwa ni mtoto wa waarabu Watanzania ambao asili yao ni toka Oman, watu wangepinga pia?
Mwkjj hapo sasa tuko pamoja katika kupanua hoja, ndio ukombozi wa fikra huu ambao kwa hapa JF wewe ni kamanda.asili ya mtu kwa mawazo yangu haiangaliwi tu kwa ngozi, kuna vigezo vingine vinavyoendana na ilo vingi sana hapo,mfano tamaduni za mtu mwenyewe, lugha ya asili,mila na desturi, na vigezo vingine wengine wataongezea.Hivyo ndo vinavyotengeneza asili ya mtu. Kwa mfano wa wairaqw iliowataja tutawangalia si tu kwa maumbili na ngozi zao bali pia na tamaduni zao, kama hazina mwendelezo wa tamaduni za kiafrica, basi inawezekana kukawa na tatizo kidogo. Nitatoa mfano wa wajamaica na nchi za karibean kwa ujumla, wajamaica waliowengi ni weusi, lakini tamaduni,mila na desturi zao sio za kiafrica kwa mtizamo wangu kwa wale wanaompinga Richa wanaweza pia kupinga mtanzania mwenye asili ya kijamaica.nikitoa mfano wa mauaji ya Rwanda( genocide) kitu kilichowapi kazi ngumu ma antholopogist ni kutafiti kama wahutu na watusi wana asili tofauti, ukiangalia findings zao ambazo zinasema hao watu hawana tofauti walitumia vigezo nilivyovitaja hapo juu. sasa jibu la swali lako nitaliacha kwenye swali pia, je watanzania wenye asili ya kihindi wanakizi vigezo hivyo? ni vigumu sana kupata jibu kama tutamuangalia mtu mmoja mmoja nje ya jamii nzima. cha kuongezea tu, suala la uraia ni la kisheria, kuwa mtanzania au la ni sheria tu watu wametunga.suala la asili ni la kijamii zaidi, linapokuja suala la kuwakilisha taifa je tuangalia legal aspect or social aspect? let us think big, maana hii ndo mijadala muhimu, tunaweza kutoka nje ya Richa kutafakali maswali magumu zaidi Richa akiwa tu unifying thread, kuna siku tutapata mgombea urais mchina baada tu ya kupewa uraia wa tanzania miaka 5,what will be the reaction wakati sheria zinasema ni mtanzania na mtanzania yeyote anaweza kugombea urais?
 
African beauty ya Tanzania itaonyeshwa wapi,kama hawa watu watatuwakilisha.Kuna sehemu zingine lazima ziwakilishwe na watu asili kama ni ubaguzi wacha waite hivyo.Sehemu kama ya umiss mie sikubaliani kuwakilishwa na watu wasio na asili.Huo ndo mtazamo wangu.

watu wa asili ya TAnzania ni wapi hao ambao wanastahili kutuwakilisha? Naomba unitajie makabila matano tu yenye asili ya Tanzania..
 
Nyangumi, yaani wahindi wakioana na watu weusi ndio wanakuwa raia zaidi?


Kumbe hilo wewe unaliona ni dogo!? Maana kama hawajioni wao ni bora kuliko wamatumbi kwa nini wasiolewe na kuwaoa!? Kama unazaliwa na kuishi Tanzania miaka nenda rudi kwa nini wengi wao hawawezi kuzungumza lugha yetu ya Taifa!? Kama hawajioni wao bora kuliko sisi kwa nini wanaishi maeneo ya kujitenga 'uhindini' na hatuwaoni wakiishi uraiani? Shilingi ina pande mbili angalia zote na utaweza kuona nani aliyeanza ubaguzi kati ya wahindi na wamatumbi. Ukijibu maswali hayo unaweza ukafikia hitimisho nani mbaguzi kati ya mhindi na mmatumbi.
 
Sina haja ya kutaja makabila Mh.Mwanakjj.Ila haina maana kuwa kabla hili bara halijagawanywa na wakoloni hakukuwa na watu wanaishi.Kulikuwa na watu wanaishi na hawakuwa wazungu,waarabu au wahindi,ila walikuwa watu weusi(wabantu).
Mh.Mwanakjj huo niliotoa ni msimamo wangu na si lazima tukubaliane.Sasa kama ni ubaguzi wacha uwe ubaguzi.
 
Watanzania wenzangu tusiwe wepesi wa kudanganyika na siasa za wote ni Watanzania.


Kama alivyosema mwana JF mmoja hapo juu, haifai kufananisha Unaigeria na Uhindi.

Ni muhimu tufahamu kuwa hata kama wote waliopata uraia wa kununua watajiita Watanzania lakini bado kuna Mtanzania halisi asiye na kwingineko zaidi ya Bongo...yaani mzalendo, achana kabisa na mipaka iliyowekwa na wazungu ili kurahisisha utawala wao



La sivyo African continent ingegawanyika ktk viinchi vya kabila moja moja kma vitaifa vidogo. Lakini bado kwa context ya rangi African continent refers to black colour people. Waarabu, Wahindi, Wazungu ni wageni tu. Angalia yaliomkuta Camila na Prince Charles na hayati Diana....yote haya ni kupigania asili.



Hawa wahindi wanaotunganya kuwa ni Watanzania, mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wengi walihamishia familia zao kwingineko hasa kwenda India, Canada, USA na UK. Lakini watanzania halisi hata wale wenye pesa zao walibaki hapa hapa.


Mwisho, naamini kama kuna mtanzania atakwenda kwenye mashindo ya aina hii na akajitambilisha kuwa atatumia kiswahili kujieleza ataruhusiwa tu kwani Miss world hawana lugha rasmi na kukataza lugha nyingine. Ni utumwa wetu wa kifikra ndio kinacho tufanya tusiamini kuwa Kiswahili hakitambuliwi.


Last but not least...Nilisikitika sana kuwa TFF wameandaa tiketi za mechi ya kirafiki kati ya Uganda na Tanzania zilizoandiwa kwa kiingireza...ingawa watumiaji wengi Kiswahili ndio lugha yao ya kwanza kabla ya kiingereza.

Tunahitaji kujikomboa kifikra ili hata mataifa ya nje waone kweli kuwa Kiswahili ni moja ya utambulisho wetu.

Ndimi,

Nsololi

Bwn Nsololi mimi nafikiri tofauti kati ya mimi na wewe ni kwamba wewe unaongea kidiplosia na unaongea UKWELI mtupu, na NI NAAPA KAMA NINAONGOPA BASI MIZIMU INIADHIBU WEWE NI MOJA KATI YA WTZ WACHACHE SANA HUMU WENYE KUELEWA JINSI DUNIA HII ILIVYO, NA WENYE UWEZO MKUBWA SANA WA KIAKILI NA UNAONA MBALI SANA, UNAELEWA KABISA TATIZO LA NCHI LIPO WAPI, NA UNAELEWA NI KWA NINI HATUPIGI HATUA YA KIMAENDELEO, NA UNAELEWA KABISA KUA CHIMBUKO LA MATATIZO YOTE HAYA TULIONAYO NCHINI MWETU NA AFRIKA KWA UJUMLA NI LA KIFIKRA SISI TUNA ROHO NZURI SANA KAMA ANAVYOSEMA MWNKJI KWA KUMTETEA HUYO DADA WA KIASIA NA KUTULETEA MAMBO YA UMOJA WA MATAIFA YA BINADAMU WOTE NI SAWA NA KUANZA KUMUANDAMA DADA YETU TEMU MWENYE UCHUNGU NA NCHI YAKE NA WATU WAKE AMELIA SANA KWA MAANA NCHI YAKE NA WATU WAKE VINAMUUMA. HAYA MAMBO YA ULIPOZALIWA NDIO KWENU NA UNA HAKI SAWA NA WENYEJI HATA KAMA UNA ASILI YA KIGENI AMBALO NI WAZO ZURI LKN UKWELI NI KWAMBA DUNIA HII HAIPO HIVYO NA WATU KAMA MWKJI WANASHINDWA KUELEWA KWAMBA HAKUNA KITU KAMA HAKI SAWA KWA WOTE HICHO KITU HAKIPO, MWAKA JANA SHULE YETU YA SEKONDARI TULIENDA KUTEMBELEA JAPAN SEHEMU INAITWA MIYAZAKI NA KULE TULIONA BAR NA MADISKO YAMEANDIKWA JAPANESE ONLY NA SIO JAPANESE CITIZEN ONLY NA MTU MWINGINE UNARUHUSIWA TUU KAMA UKIANDAMANA NA MJAPANI, TUKAWAULIZA WATU WAKASEMA NI KAWAIDA HUKO JAPANI, NA JAPNI NI NCHI YA KIDEMOKRASIA INASIFIKA DUNIA NZIMA, NA NINAFIKIRI NCHI NYINGINE NI HIVYO HIVYO, JE KWA NINI SISI TUWE TOFAUTI ETI KWA SABABU MWALIMU NYERERE ALISEMA UKIWAULIZA KILA KITU MWALIMU ALISEMA KANA KWAMBA YEYE ALIKUA MUNGU NA KILA ASEMALO HALIPINGIKI, MWALIMU PIA ALISEMA TUWE NA SIASA ZA UJAMAA NA KUJITEGEMEA KWAMBA TUWEZE KUJITOSHOLEZA NA KILA KITU NA KWAMBA MABEPARI NI WANYONYAJI MBONA KAFIA HOSPITALI ZA ULAYA ZA HAO WANYONYAJI? KAMA YEYE ALIKUA SAWA KWA KILA KITU BASI ANGEFIA LUGALO NA SI KWINGINEKO.
MWISHO MIMI NASEMA HAWA WATU KAMA KINA MWKJI HATUWAHITAJI KTK NCHI YETU NA HUU NDIO MWANZO TUNAITAKA NCHI YETU DADA YETU TEMU AMETUFUNGULIA NJIA NA AMETUONYESHA KWA MACHOZI NA MIMI NASEMA MACHOZI YAKE HAYAENDI BURE NA SIKU ITAKUJA AMBAPO TUTAIMILIKI NCHI YETU NA WATU WOTE WENYE ASILI YA KIGENI NDIO WATAKUA DARAJA LA PILI NA SI KINYUME CHAKE.
Kuhusu suala la tiketi za uwanja nimeuliza swali la kutumia kiswahili humu ktk majadiliano na majibu yake napewa:
"Ndugu yangu kijakazi nionyeshe wapi imeandikwa kwa kisw ni lugha ya taifa"
"unajua ni rahisi kujieleza kiingereza kuliko kiswahili"
"unajua kiswahili ni kigumu sana" n.k
sasa sijui hilo nianze kujibu vipi. Tatizo ni kwamba UKWELI hatutaki kuukubali UKWELI NI KWAMBA NI ASILIMIA SI ZAIDI 5 KATI YA WTZ MIL 37+/- wanaoweza kuzungmza, kusoma na kuelewa kiingere za na mtz yeyote ambaye amezaliwa na kukulia tz anaelewa zaidi kisw/kienyeji zaidi ya lugha nyingine yeyote na huo NDIO UKWELI, na kama unapenda kwenda mbele basi ukubali kwanza...mengi yanakuja...............
 
Wabaguzi huwa hawajifichi.. wananikumbusha George Wallace ambaye aliwakataza watu weusi kusoma kwenye vyuo vikuu vya Alabama vinavyomilikiwa na serikali.. akaapa kuwa "segregation, segregation tomorrow, segregation forever"... Bahati nzuri alipokufa, Alabama ilikuwa inapokewa wanafunzi wa rangi zote kwenye vyuo vyake!! Hivyo viapo vyenu haina maana yoyote maana hata mbinguni wanavipuuza!!! Waliapa kina Botha, waliapa kina Ian Smith, sasa wako wapi?!!
 
Sina haja ya kutaja makabila Mh.Mwanakjj.Ila haina maana kuwa kabla hili bara halijagawanywa na wakoloni hakukuwa na watu wanaishi.Kulikuwa na watu wanaishi na hawakuwa wazungu,waarabu au wahindi,ila walikuwa watu weusi(wabantu).

Hutaji kutaja makabila siyo kwa sababu hauna haja ya kufanya hivyo, ni kwa sababu huwezi. Katika Tanzania kuna makabila matatu tu ambayo yana asili na ardhi hii! Wengine wetu sote ni wahamiaji! Halafu kwa taarifa yako, siyo watu wote weusi ni wabantu!

Mh.Mwanakjj huo niliotoa ni msimamo wangu na si lazima tukubaliane.Sasa kama ni ubaguzi wacha uwe ubaguzi.

Ni kweli si lazima kutokubaliana lakini ni muhimu tuweze kuweka hadharani ni nini tusichokubaliana. Wewe umekubali ni mbaguzi, na mimi nawapinga wabaguzi wa aina yoyote ile! Tunakubaliana kwa hilo?
 
Mwkjj kuna siku tutapata mgombea urais mchina baada tu ya kupewa uraia wa tanzania miaka 5,what will be the reaction wakati sheria zinasema ni mtanzania na mtanzania yeyote anaweza kugombea urais?

Mbona umeenda mbali ndugu? Ebu fikiria RA awe ndo mgombea 2010/2015?, Na kwa mwendo wa takrima na Rushwa za CCM hilo lawezekana kabisaaaaaa! Je, Tanzania haitakuwa koloni la .....

Japo twaitwa wabaguzi, lakini nadhani ni vema kukawa na mipaka ya uraia wa asili na uraia wa sheria!!

Vinginevyo hili laweza kuwa bomu kubwa huko mbeleni.
 
Kitila nakusikia kaka, ila angalia maneno niliyoyasema hapo juu kuwa ubaguzi haukomi, ukikosa rangi unakuja kwenye umbo! Hoyce Temu alipohojiwa wakati anaangusha machozi alinukulikwa akisema hivi ""Hii siyo sawa, kulikuwa na Waafrika wenye sifa na walijibu swali vizuri tena kwa kujiamini, nashaangaa majaji wamemchagua Richa, wakati rangi yake haiwakilishi Utanzania," Ilivyoripotiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda. Nina uhakika akiendelea kubisha watu watamchezea rekodi ya maneno yake!

Eeeheeeee! ebana wee kama haya ndiyo yalikuwa maneno yake basi mimi hapo sipo, ni mbaguzi tena wa kutisha. Kwa kweli mimi haya mambo huwa sifuatilii kabisa, yamenipiga chenga. Nilianza kufuatilia kusoma habari zake baada ya issue ya ubaguzi kujitokeza na nikamsikiliza na kumsoma Hoyce jana na leo. Sasa haya maneno uliyo-quote nilikuwa sijakutana nayo. Alikosea sana na anapaswa kuomba msamaha ajirudi, wala hana sababu ya kujibaragazua maana alichosema mwanzo ndo kinasimama zaidi kuliko alichosema baadaye! She made a big mistake, but it is good that we now know who and how she's! She's absolutely a disgusting racist!
 
Mwanakijiji

Ubaguzi hauwezi kwisha tena kama leo umeona in UK walio wengi ambao DNA zao zimehifadhiwa na police ni minority ambao asili yao siyo England na Scotland hata hapo USA wewe unafahamu North Carolina ni kwa weupe na mswahili hakanyagi na Southern Calorina kwa waswahili huwezi kubadili ndio sababu tuna tofautiana.

Nelson Mandela sanamu yake ilikuwa iwekwe Trafalgar Square lakini kutokana na ubaguzi wazungu walimwekea ngumu Ken Livingstone na ikabidi waipeleke kule Parliament square hivi ni vitu live ambavyo vinatokea hivi sasa. I beg to differ kwa hili na wewe lakini haya mambo hayawezi kwisha asilani na yataendelea hadi tutakapokwisha sisi na kizazi kipya kitayadumisha.

South Afrika wazungu waliachia ngazi kwa mtutu wa bunduki leo hii huwezi kuniambia sisi Tanzania ndio wenye huruma sana wakati hawa wahindi ndio wanatubagua.

Hii niliiweka kule kwenye thread nyingine pia hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=67070#post67070
 
Back
Top Bottom