How to get a twenty hectors for 99 years lease for farming from Government?

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Ndugu wanajamiiforums!

Kama mtu anataka serikali impe ardhi kwa kipindi cha miaka 99 afanyeje? Ardhi yenyewe ni kwa ajili ya kilimo na mifugo.

Kuna watanzania wana elimu ya kilimo na mifugo na wamejiunga kikundi na wanataka kupata ardhi kama heka 20 mpaka 60 kwa ajili ya kuanza mradi wa kilimo na ufugaji.

Ardhi yenyewe inatakiwa Arusha au Morogoro.

Hawajui pa kuanzia na wanaogopa serikalini kuna 'bureaucrasy'

Wameitikia wito wa Kilimo kwanza na wanataka kujiajiri na pia kupata mkopo benki.

Wanataka ardhi yenye kufaa kwa kilimo na mahali penye mvua ya uhakika au uwezekano wa umwagiliaji.

Wana Jamii forums wenye habari zozote tafadhali toeni msaada.
Wanajamii wengine wana ruksa kujiunga, karibuni
 
Naomba nianze na marekebisho ya maneno yako,unataka eka 20 au hekta 20? Hekta 1 ni sawa na eka 2.5,pili ardhi iko ya kumwaga sana huko morogoro (mbingu,Ifakara,chita),nikisema Arusha nitakuwa nakudanganya mchana kweupe. Ila maeneo yafuatayo yana ardhi kubwa ila yana ugomvi usioisha hayatawafaa ( kilosa,kilombero,ulanga,mlimba,mtibwa na mang`ula). Wote wanafikiria kwenda huko.

Kwa kuwa umetaja maeneo uyapendayo itakuwa vigumu kukutajia maeneo mengine. Ila yapo yaliyo mazuri zaidi. Pili mnaweza kugawa maeneo yenu ktk makundi mawili,kilimo kivyake na mifugo kivyake.
 
Kwa kawaida wizara ya ardhi hutoa hati ya miaka 99 kwa ardhi ya kilimo na hasa shamba likiwa kubwa. Unachotakiwa kufanya ni kuomba ardhi hiyo kupitia serikali ya kijiji au mamlaka husika (local goverment or ministry of lands) na kisha utatakiwa ku-survey na hatimae kuomba milki ya ardhi husika. Mara nyingi kuna ucheleweshaji hivyo unatakiwa kuwa na uvumilivu
 
Kuna utaratibu ufuatao unatumika sana na ni halali,ili kukwepa usumbufu wa serikali naomba nikwambie. Serikali ya kijiji inaweza kukupa ardhi isiyozidi eka 49 kama mtu binafsi, na inaweza kukupa ardhi isiyozidi eka 100 kama kampuni. Zaidi ya hapo ni suala la serikali kuu.

Ushauri wangu,tafuta ardhi kwanza (nimeuliza kipimo chako hapo mwanzo ili nikusaidie),hapo utakapoipata ichunguze(ukiweza nunua kipande kidogo kiendeleze) kabla hujaenda huko serikalini. Ukienda kuomba serikalini,unaweza ukapelekwa TIC kumbe wewe ni size ya kijiji.

Ukifika pale TIC (wilayani,mkoani) kuwaambia habari hiyo,utapewa msululu wa kufuata mpaka ukome,au ukaishia kuwajulisha jamaa(wanene) kuwa sehemu fulani kuna dili. Ila kama wewe ni mnene pia nenda pale TIC watakwambia wapi kuna ardhi ya kumwaga. Nakupa hayo kwa sababu yamenikuta tayari.
 
Back
Top Bottom