How To Control Inflation in Tanzania?

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
As per this article:


Tanzania's inflation rate rose in April for the first time since October last year as food and fuel price inflation picked up in east Africa's second largest economy, official data showed on Monday.

The National Bureau of Statistics said the year-on-year inflation rate rose to 9.4 percent from 9.0 percent in March. The inflation rate had been declining steadily after hitting 12.7 percent in October 2009.

The NBS said food inflation rose to 9.8 percent from 9.7 percent a month earlier while fuel, power and water prices were 19.9 percent higher than in April 2009, up from a 16.3 percent annual rise in March.

The government is aiming for an inflation rate of 6 percent by June, although analysts have cautioned this target may be hard to hit due to rising fuel prices and expected increases in government spending ahead of elections in October.

Now my question is: How can we control the inflation in our country? I know I have gurus here and can learn from you guys.
 
BOT wanaweza kudhibiti mfumuko wa bei kwa kuuza BONDS and T-bill katika soko la hisa kwa hiyo watu wataponunua hizi bond na bill watakuwa wanapunguza volume (kiwango) cha pesa kwenye mzunguko ambacho kitasababisha kushuka kwa mfumuko wa bei
 
Now my question is: How can we control the inflation in our country? I know I have gurus here and can learn from you guys.


Njia mbalimbali zinaweza kutumika kupunguza inflation kwa kuzingatia imesababishwa na nini

a) Monetary Policy- njia hii inatumika kudhibiti inflation inayotokana na uwingi wa pesa kwenye mzunguko (money supply and circulation). Kuna tools mbalimbali zinatotumika katika monetary policy ambazo ni;
i. Discount rate –hiki ni kiwango cha riba ambacho kinatozwa kwa mabenki yanapoazima pesa toka central banks. Kunapokuwa na inflation inayotokana na kuwa na pesa nyingi kwenye mzunguko central banks zinaweza kuongeza kiwango hiki cha riba na hivyo kupunguza ukopaji wa pesa.
ii. Open market operations (OMO)-Njia hii inahusisha benki kuu kuuza T-bill and T-bonds kwa umma (watu binafsi na makampuni). Kwa kufanya hivyo pesa zinatoka mikononi kwa umma na hivyo kupunguza uwingi wa pesa kwenye mzunguko. Tanzania hutumia zaidi njiaa hii ukilinganisha na njia nyingine(OMO is the principal instrument for monetary policy in Tanzania) Njia hii huweza kutumiwa pia na serikali to finance temporary shortfall in budeget
iii. Reserve ratio- inahusisha kiwango cha pesa ambacho commercial benki zainatakiwa kuwa nacho against deposits zake kwenye central bank. Wakati wa mfumko wa bei central bank huongeza reserve ratio. Benki kuu ya Tanzania haitumii sana njia hii kutokana na kusababisha uncertainities kwa mabenki zinakazotokana na kubadili kwa reserve ratio mara kwa mara.

b) Fiscal Policy- Hii inahusisha matumizi ya serikali na kodi zinazotozwa na serikali (governmrnt expenditures and taxes). Inflation inaweza kudhibitiwa kwa kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza viwango vya kodi.

Njia nyingine zinazoweza kutumika ni pamoja na ku control population, idadi ya watu ikipungua itapelekea kupungua kwa demand ya bidhaa na hivyo bei kushuka. Njia nyingine ni regulatory kama ambavyo EWURA imekuwa ikifanya kwenye bei ya mafuta.

Ningependa kurejea kuwa ni njia ipi itumike itatokana na kisabishi cha inflation. Kwa inflation iliyopo Tanzania toka mwaka jana about 12% na mpaka sasa about 9% sababu kubwa ni bei kubwa ya chakuala inayotokana na uzalishaji mdogo kutokana na ukame. Sababu nyingine kubwa ni kupanda kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia.

Kwa upande wa bei za chakula moja kati ya mikakati ya serikali ni pamoja na Kilimo Kwanza. Serikali imeamua kwa makusudi kuongeza bajeti ya Kilimo na kutoa ruzuku kwa wakulima wadogo katika mikoa karibu yote wakiwemo wale wanaotumia umwagiliaji katika kilimo chao.

Namalizia kwa kusema kuna njia nyingi za kudhibiti mfumko wa bei kama nilivyojaribu kueleza hapo juu, njia gani itumike hutegemea mlipuko wa bei unasababishwa na kitu gani. Kuna kipindi ambacho njia zaidi ya moja inaweza kutumika kwa wakati mmoja.

Ninatumaini nimeweka mwanga kidogo katika hili!!!
 
darasa la nguvu, thanx luhota

Nadhani tunahitaji kuangalia pia balance of trade kati ya import na export, mauzo ya nje yakiimarika hata fedha yetu itaimarika pia. Kuhusu kilimo unahitajika mkakati wa ziada kwani nguvu kazi ya kulima chakula inakwenda shule za kata na wakihitimu huko breki ya kwanza mijini kusaka ajira.

Kupunguza mfumuko wa bei kwa kupunguza mzunguko wa fedha (monetary control) kutasababisha ugumu wa maisha na watu kuichukia serikali yao hivyo tutakuwa tumezalisha tatizo la kisiasa.
 
Nimefuatilia hotuba aliyoitoa Waziri wa Fedha na Uchumi alipokuwa akiwasilisha Hali ya Uchumi asubuhi ya leo, anasema inflation kwa mwezi April ilikuwa ni 9.4%, mwezi May 7.9%, sijui nini kimesaidia kupunga inflation kwani hali ya chakula bado ni tete na mafuta ndio yanapanda siku hadi siku
 
Nimefuatilia hotuba aliyoitoa Waziri wa Fedha na Uchumi alipokuwa akiwasilisha Hali ya Uchumi asubuhi ya leo, anasema inflation kwa mwezi April ilikuwa ni 9.4%, mwezi May 7.9%, sijui nini kimesaidia kupunga inflation kwani hali ya chakula bado ni tete na mafuta ndio yanapanda siku hadi siku

Kwa hilo jaribu kuwauliza NBS zile weightings zao za bidhaa mbalimbali zinazojaza kapu la bei. Kuna tetesi ya kwamba wameshusha uzito wa chakula katika kapu hilo kutoka 55.9% mpaka kwenye asilimia arobaini n ushee, ni vyema tukapata uhakiki kutoka kwao. Ningependa pia kujua sababu zao kuu za msingi za kufanya hivi ikiwa ni kweli wamefanya hivyo. Kama unakumbuka vizuri uzito wa Mafuta, Nishati na Maji ni asilimia 8.5 na pia zile za usafirishaji ni asilimia 9.7 kwa viwango vya kapu lile la zamani la bidhaa na bei hivyo maongezeko ya gharama ya mafuta hayatosababisha mabadiliko makubwa katika mfumuko mzima wa bei kwani huu ni wastani wa bei za bidhaa mablimbali tu. Fuatilia kwa undani zaidi hapa, National Bureau of Statistics
 
Tusisahau matumizi ya njia bora za uchukuzi katika bidhaa kumfikia mlaji= reli!.......kwa kiasi kikubwa reli ni mhimili mkubwa katika kupunguza overhead costs za bidhaa.
 
Mimi mtazamo wangu ni tofauti kidogo mie naona serikali ikasimamia vizuri suala la ufisadi nchini liishe kabisa ambalo liko kwa kiwango kikubwa sana karibia kila sector itasaidia kupunguza inflation.
 
I seriously doubt if most people know the cause of inflation.Inflation started when Goldsmiths who later became Bankers foutly printed receipts(this later became paper money) with values more than gold they held in their safes.This gold was brought for safe keeping in the middle ages when gold was the medium of exchange.Seeing that people did not come to collect their gold and instead exchanged among themselves the receipts as a medium of exchange,they printed more of the receipts not backed by gold values.This has been the cause of inflation since than.****** huu unafichwa kwa kuwa waliofanya utapeli huu ni mababu wa bankers wakubwa hawa wa leo.:pPaper money not backed by gold of an equal value.So if we want to control inflation,we have to have gold reserves at BOT with a value equal to that of paper money in circulation.I doubt if we have any bullions at BOT.There are so many blaa blaas about the causes of inflation,it's all rubbish.
As per this article:



Now my question is: How can we control the inflation in our country? I know I have gurus here and can learn from you guys.
 
Mie sio mchumi lakini inflation naielewa kuwa ina be caused by "too much money chasing too few goods. The general price level is indeed correlated with the money supply.In a modern economy, prices are seldom driven by the money supply. More commonly,the money supply reacts to changes in the general price level.
 
Back
Top Bottom