How Kikwete, new darling of the West, saved Kenya from collapse

Mwafrica hujanielewa na unabidi usome message nzima. Hatuwezi kuishi bila misaada kwa sasa, miaka ijayo itawezekana lakini kwasasa tuna chaguo mbili misaada au madeni, na mimi nafikiri misaada ni mizuri kuliko madeni. Miaka 5 iliyopita nilikuwa natumia $500 kwa mwezi kununua dawa za ndugu yangu za ukimwi na sasa natumia $0 kwasababu dala zipo kwa wagonjwa kwa bure. Hii yote imewezekana kwa sababu ya misaada, kama wewe unataka mikataba ndiyo ilipe dawa ni mawazo yako lakini mimi binafsi na watanzania wengi wamefaidika kwa misaada tutake au tusitake.Nchi yetu itafikia wakati wa kujitegemea lakini kwa sasa kuhudumia watu 40 million na tuna deficit kwenye budget ya 30% na budget yetu yote ya Tanzania ni $3Billion misaada ni muhimu hasa ya afya. Je kuna ubaya gani kusaidia watoto net za mbu hata kama ni $25 million wametoa kwa hilo na watoto wanapona kunaubaya gani? Watanzania kwa upande mmoja tunatabia ya kupinga vitu kwani tunapenda ubishi na ubishi huu wa Mwafrica hauna msingi.


Si kila ufumbuzi unao onekana ni rahisi ni ufumbuzi sahihi.

Misaada ni ugonjwa mbaya kuliko magonjwa yote yaletwayo na umasikini.
Umasikini wetu ni wa mawazo zaidi kuliko kwamba hatuna rasilimali.

Misaada inatunyima nafasi ya kuchukua hatua madhubuti kumaliza matatizo yetu ya kiuchumi.
Misaada inawafanya Watendaji wa serikali,Wabunge na wananchi wengi kugeuza shingo zao na kuangalia nje ya nchi kwa macho ya kuonewa huruma badala ya kutazama ndani ya nchi kwa macho ya upembuzi na kutafakari uwezo wetu tusio utumia.

Deficit unayoiongelea inalelewa na Wabunge wetu na serikali kwa ujumla kwa kuendekeza mambo mengi yasiyo ya lazima. Kwa watendaji wa serikali na baadhi ya wananchi,Misaada kutoka nje ni nafuu yao binafsi ndiyo maana hawaoni aibu kutangaza bajeti tegemezi.
Si lazima viongozi wa serikali watumie VX na GX lakini ni lazima watumie magari imara ambayo yako mengi sana na ya kila aina. Ununuzi wa magari tu nchini Tanzania unaonyesha ni vipi watendaji wetu wa serikali wasivyo ona aibu kuomba misaada kutoka kwa kila wanaye muona anazo.

Si muda mrefu ujao tutaanza kuoamba misaada kutoka nchi masikini kama sisi.
Indonesia, Thailand, Vietnam na hata Kambodia tu kwa sababu sisi Watanzania tunadhani tulizaliwa kuomba na kusaidiwa.

Wabunge na viongozi wa serikali hushhirikiana kupanga bajeti tegemezi kwa sababu tu akili zao na maono yao ni tegemezi.Ndani ya vichwa vyao hawaioni bajeti inayo jitegemea. Ni walemavu.

Mtu akiwa kilema kiungo fulani nje ya mwili wake ni rahisi kwa kila mtu kumwona mlemavu. Lakini mtu akiwa mlemavu katika sehemu ya ubongo inayoshughulikia Vision, nje ataonekana yuko sawa lakini kumbe hayuko sawa hata kidogo, utamwona jinsi anavyohangaika kuiona kesho na keshokutwa katika mipango yake. Viongozi wa serikali yetu tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni walemavu wa ubongo katika sehemu inayoshughulikia Vision, wala siongopi.

Kama una $100.00 ni vipi unaweza gharamia maisha ya $130.00?

Wananchi walio wengi nchini Tanzania wanishi sawa sawa na vipato vyao.
Wale wanaoishi chini ya vipato vyao ndo pekee walioweza kupiga hatua kinyume na matazamiao ya wengi kama siyo wote.

Mafisadi na Serikali yetu ndo wao pekee wanaishi kwa fedha inayozidi kipato. Kwa sababu sehemu ya Bongo zao inayoshugulikia Vision imedata, wanashindwa kelewakwamba nchi ni lazima itumie sehemu tu ya kipato chake na zaidi ni lazima ichukue hatua madhubuti kupigana na jinamizi la kutegemea misaada.

Nchi kutegemea misaada ni ugonjwa mbaya kiuchumi ufananao na ugonjwa wa Ukimwi.

Kwa hiyo nchi inayotegemea misaada ni sawa na mgonjwa wa ukimwi.

Naomba nieleze mfano huu wa ugonjwa wa ukimwi kabla sijaonekana nina matusi na kukosa heshima.

Mgonjwa wa ukimwi hupewa dawa kurefusha maisha yake, kwani mpaka sasa hakuna dawa iwezayo kuponya ukimwi. Nchi inayoishi kwa misaada inaishi kama mgonjwa wa ukimwi kwa sababu misaada ni dawa ya kuairisha matatizo tu.

Hakuna nchi na wananchi wake walioendelea kwa kupewa misaada.
 
Kwa hili la uomba-omba mimi nipo na mwadilu, umatonya hautusaidii kitu bali unatuongezea ufukara. Ufukara wa kiakili, kiuchumi na kinadharia. "mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini".
 
Suala la umatonya, halikuanza na Muungwana, tumezaliwa nalo toka uhuru mwaka 1961, sasa kama kweli mnyonge mnyongeni, basi muungwana apewe haki kwenye kulijadili hili, maana amelikuta na ndio utamaduni wetu as a nation kutoka awamu zote zilizopita,

labda ashauriwe tu tufanye nini tujiuondoe kwenye umatonya?
 
Suala la umatonya, halikuanza na Muungwana, tumezaliwa nalo toka uhuru mwaka 1961, sasa kama kweli mnyonge mnyongeni, basi muungwana apewe haki kwenye kulijadili hili, maana amelikuta na ndio utamaduni wetu as a nation kutoka awamu zote zilizopita,

labda ashauriwe tu tufanye nini tujiuondoe kwenye umatonya?

Kwanza hajaomba ushauri ju ya hili.

Pili kabla hajaamua kuwa rais hakuja kutuuliza iweje sasa wewe unaomba tumpe ushauri wakati anatekeleza kile kilichomfanya agombee?

Tatu sababu kwamba tumepokea misaada siku zote si ya msingi.
Hakuna mabadiriko yanayo kuja kwa kukumbatia kawaida. Msingi wa mabadiriko yeyote ya maana ni kuachna na tabia mfu zinazo kuvuta shati kila siku.

Wananchi wote ni lazima wajifunze kuishi kwa bajeti kwa kuchagua mambo muhimu na ya lazima kuyagharamia.

Nchi nayo ni lazima ijiwekee mikakakti ya kufuta utegemezi toka nje kwanza kwa kutoa tamko na kuweka bayana kwamb ni aibu kuishi kwa misaada. Pia, kuangalia kwa macho yenye maono na kurekebisha kasoro zote zinazo tunyima mapato kitaifa.

Utajiri wa taifa siyo kujaza mapesa kwenye mifuko ya watu, ni kujenga miundo mbinu yote ndani ya nchi ili kuondoa usumbufu mwingi kwa wananchi unao sababishwa na ubovu au kuto kuwepo kabisa kwa miundo mbinu muhimu.
 
Kwanza hajaomba ushauri ju ya hili.

Pili kabla hajaamua kuwa rais hakuja kutuuliza iweje sasa wewe unaomba tumpe ushauri wakati anatekeleza kile kilichomfanya agombee?

Tatu sababu kwamba tumepokea misaada siku zote si ya msingi.
Hakuna mabadiriko yanayo kuja kwa kukumbatia kawaida. Msingi wa mabadiriko yeyote ya maana ni kuachna na tabia mfu zinazo kuvuta shati kila siku.

Wananchi wote ni lazima wajifunze kuishi kwa bajeti kwa kuchagua mambo muhimu na ya lazima kuyagharamia.

Nchi nayo ni lazima ijiwekee mikakakti ya kufuta utegemezi toka nje kwanza kwa kutoa tamko na kuweka bayana kwamb ni aibu kuishi kwa misaada. Pia, kuangalia kwa macho yenye maono na kurekebisha kasoro zote zinazo tunyima mapato kitaifa.

Utajiri wa taifa siyo kujaza mapesa kwenye mifuko ya watu, ni kujenga miundo mbinu yote ndani ya nchi ili kuondoa usumbufu mwingi kwa wananchi unao sababishwa na ubovu au kuto kuwepo kabisa kwa miundo mbinu muhimu.

matatizo ya kumtukuza mtu ndiyo yanayoturudishanyuma. tukiacha tabia hiyo tutafika mbali sana. Kila kitu hata wajibu wa mtu sisi tunaona nia ajabu. mpaka hata kuomba omba sisi tunasifia tu. je tungekuwa tunatumia bongo zetu si ndo ingekuwa bora zaidi kuliko hii?
 
Posted Date::3/8/2008
Subira ya muafaka CUF yafikia kikomo

*Yawaita wajumbe wake wajieleze

*Kutoa tamko baada ya kikao


Na Muhibu Said


KAMATI ya Ulinzi na Usalama ya Chama cha Wananchi (CUF), imewaita wajumbe wa chama hicho wa kamati ya usuluhishi ya mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar, ili kueleza maendeleo na hatma ya mazungumzo hayo.


Wajumbe wa kamati ya usuluhishi ya mazungumzo hayo kutoka CUF, walioitwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya chama hicho, ni Maalim Seif Shariff Hamad (Katibu Mkuu) na Hamad Rashid Mohamed (Mbunge wa Wawi).


Wengine, ni Abubakari Khamisi Bakari (Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni), Joran Bashange (Naibu Mkurugenzi wa Mipango), Juma Duni Haji (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar) na Ismail Jussa (Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa).


Hatua hiyo imefikiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya CUF, ikiwa ni siku moja baada ya kuripotiwa kwamba, ufumbuzi wa mpasuko huo, umekumbwa na kikwazo kinachotishia kuharibu ndoto za Rais Jakaya Kikwete za kuona hali ya utengamano inapatikana visiwani humo.


Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati Ulinzi na Usalama, Saidi Miraji alisema kikao cha kamati hiyo kitafanyika katika ofisi za Vuga, mjini Unguja keshokutwa.


Miraji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Blue Guard na Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa la chama hicho, alisema katika kikao hicho watawaita wajumbe wa kamati ya usuluhishi kutoka CUF na kwamba, ajenda ya kikao itakuwa kupokea taarifa ya maendeleo ya mazungumzo ya muafaka na kuijadili.


"Wazanzibari na Watanzania kwa jumla nao pia wanahitaji kuona muafaka. Mazungumzo yasiyokuwa na mwisho yanawafanya washawishike kupata taarifa," alisema Miraji na kuongeza:


"Ili kuwaridhisha, nimeona niitishe kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama tarehe 10/3/2008. Ajenda itakuwa ni moja tu. Kupokea taarifa ya maendeleo ya mazungumzo na kuijadili. Hivyo, tutawaita wajumbe wa kamati ya mazungumzo".


Alisema wamelazimika kuwaita wajumbe hao kwenda kutoa taarifa hiyo katika kikao hicho kwasababu mbalimbali, ikiwamo kamati kutopata taarifa za maendeleo ya mazungumzo takribani miezi mitatu tangu mazungumzo hayo yaingie awamu nyingine.


Hata hivyo, alisema baada ya wajumbe hao kuwasilisha taarifa hiyo kwa kamati, watawataka watoke kikaoni ili waijadili kabla ya kuuarifu umma.


Alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kamati yake kufanya ziara maalum ya shughuli za chama katika mikoa ya Tanga, Unguja, Pemba na kuhitimishwa na mikutano ya hadhara iliyofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam, Jang'ombe, kisiwani Unguja na kikao cha ndani cha vijana kisiwani humo katika siku tofauti hivi karibuni.


Miraji, alisema katika mikutano hiyo, vijana wa chama hicho waliwabana wakiwataka waeleza kuhusu maendeleo na hatma ya mazungumzo hayo kutokana na kushawishiwa na muafaka uliofikiwa kati ya vyama vya PNU na ODM vya nchini Kenya hivi karibuni.


Alisema hivi karibuni, vijana wa mkoa wa Mjini Magharibi, walifanya mkutano katika eneo la Kilimahewa ambako walimwalika Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahim Sanya na Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano na Umma wa CUF Zanzibar, Salim Bimani.


Aliongeza kuwa, katika mkutano huo, vijana hao waliwataka viongozi hao wafikishe salam hizo kwa chama.


Mazungumzo hayo yanayofanywa na wajumbe wa kamati ya usuluhishi inayojumuisha wajumbe kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CUF, yalianza Zanzibar, Januari 17, mwaka jana.


Mara ya mwisho kamati hiyo ya pamoja, ilikutana Ijumaa wiki iliyopita mjini Bagamoyo, mkoani Pwani na kufikia makubaliano katika masuala ya msingi, kubwa likiwa ni lile linalohusu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa itakayojumuisha vyama hivyo viwili vya siasa.


Hata hivyo, taarifa zinaeleza kwamba Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kwa nyakati tofauti, amekuwa akionyesha kutokuwa tayari kwa sasa, hususan kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayokuwa na Waziri Kiongozi atakayetokana na CUF.
 
Mpasuko wa Zanzibar unamshinda, huko Kenya ni kujitafutia ujiko tu mambo yote wamefanya Wamarekani na waingereza..
 
Madilu,

Naafikiana na wewe 100%! Kutegemea misaada ndo imetufanya tuendelee kuwa maskini pia kimawazo!

Hii 40% ya budget inawezekana kabisa kuweka lengo kuwa na budget isiyotegemea msaada say in 5 or 10 years!

Kama alivyosema Madilu..tupunguze tu matanuzi ya mashangingi, majumba ya ajabu ajabu na posho kama zile za 105,000 ya vikao wafanyakazi BoT ..itapatikana pesa nyngi tu pia kulipia wagonjwa wote wanaotumia ARV na pia pesa ikabaki!

Misaada (unless for humanitarian reasons kama ukame, mafuriko n.k) iogopwe kama ukoma!

Tunahitaji net kuvua samaki na sii samaki aliye tayari tu kula!

Pia serikali ikikosa misaada ndo itaamika..itakusanya kodi na kutowapa matajiri exemtions! Hivi mnajua TRA hukusanya tu 30-40% ya kodi? Watu wengi hawalipi kodi au huhonga maafisa TRA walipe tu kidogo!

Nchi ina mabonde na ardhi safi, dhahabu, mifugo kibao na raslimali watu yet watu wanasema tunahitaji kuwa matonya!

Kama ni Umatonya..for how long?
 
Mpasuko wa Zanzibar unamshinda, huko Kenya ni kujitafutia ujiko tu mambo yote wamefanya Wamarekani na waingereza..

Duh!!! Mzee Masatu maneno haya umeya andika wewe mwenyewe ama kuna kuna mtu anatumia ID yako kumwaga data hizi ?Basi utakuwa umesha amka sasa umeona ukweli kuhusu JK na sirikali yake .Tupo pamoja nimerudi toka Kijijini .
 
i think kikwete knew exactly what he is going to talk with those two goons, but i think the swahili language also lubricated the talks with two..so VIVA Swahili language.
 
Back
Top Bottom