How independent is NEC?

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
[h=2]Mkuchika aiandikia NEC kuitisha uchaguzi wa Madiwani Arusha[/h]


NA JOHN NGUNGE



5th November 2011


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni








Mkuchika(21).jpg

Hatimaye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi),George Mkuchika


Hatimaye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), ameandika barua rasmi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumuagiza aitishe
uchaguzi kwa viti vitano vya madiwani wa Arusha ambao walifukuzwa na chama chao Agosti 6, mwaka huu.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema jana kuwa amepokea nakala ya barua toka kwa Waziri Mkuchika iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Chadema taifa, Dk. Wilbrod Slaa, ikimtaarifu kuwa ametambua kufukuzwa kwa madiwani hao.
Alisema barua hiyo ya Mkuchika ina mtaarifu Mwenyekiti wa NEC kwamba nafasi za viti vya udiwani katika kata tano za madiwani hao zipo wazi na anatakiwa kuitisha uchaguzi.
“Nimetumiwa nakala ya barua ya Waziri Mkuchika toka kwa Katibu Mkuu Taifa wa Chadema ambayo nimeipata jana, barua hiyo iliandikwa Oktoba 6, mwaka huu, kwenda kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi akitangaza kwamba kata za madiwani hao zipo wazi na atangaze tarehe ya uchaguzi,” alisema. Baada ya kufukuzwa uanachama, madiwani hao walifungua kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha, wakipinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana katika Mkutano wa Dharura, mjini Dodoma, Agosti 6, mwaka huu, ya kuwafukuza uanachama.
Licha ya kufukuzwa kwao, madiwani hao bado walikuwa wakitambuliwa na serikali na kwa wakati mwingine walikuwa wakilipwa posho hadi pale mahakama ilipotupilia mbali kesi yao.
Madiwani waliofukuzwa na kata zao kwenye mabano ni Estominh Mallah,(Kimandolu), Charles Mpanda (Kaloleni), Ruben Ngowi (Themi), John Bayo(Elerai)na Rehema Mohammed (Viti Maalum).



CHANZO: NIPASHE


0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni


Inakuwaje NEC inapokea amri kutoka kwa serikali kwa ajili ya kuitisha uchaguzi ? shouldn't NEC be an independent organ from any govt. interference ? inakuwaje NEC imemtangaze mtu kuwa diwani lakini haina mamlaka ya kutangaza uwazi wa nafasi inapotokea ?? serikali ndio inatangaza kuwepo au kutokuwepo kwa uchaguzi shouldn't be the part of NEC responsibilities??? what will happen if the Govt. refuses to call for election for political reasons ??
ingekuwaje endapo mkuchika mwenyewe angekuwa diwani and for some reason he is supposed to declare his position open against his will?? in my opinion NEC should have total authority to run the election without govt calling the shot. what is yours ??
 
Hapa sasa ndio nakuwa nafunguka macho zaidi na zaidi kwanini hawataki katiba mpya maana ufedhuri wote huo ndio itakuwa kwishneh pia madaraka makubwa ya mjomba si yatapungua! Yaani katiba hii inampa mamlaka ya kuteua kma ifuatavyo:
1. Anamteua waziri mkuu
2. Mawaziri na Manaibu Waziri wote
3. Makatibu wakuu wote wa wizara
4. Wakuu wa mikoa wote
5. Wakuu wa wilaya wote
6. Mabalozi wote
7. Wakuu wa taasisi zote e.g NHC, TACAIDS, TASAF,NSSF,PPF,LAPF,PSPF nk
8. Wakuu wa vyuo vikuu vya umma au serikali wote e.g UDSM, MZUMBE ,SUA, UDOM nk
9. Mkuu wa majeshi
10. Mkuu wa polisi
12. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
14. Gavana wa benki kuu
15. Mwenyekiti shirika la maendeleo la taifa
16. Wakuu wa mkurabita na mkukuta
17.
wengine sikumbuki, kuwang'oa magamba bado kazi ipo!

 
Back
Top Bottom