How EWURA arrived at the pump price in debate now behind the scene?

Santa

Member
Feb 10, 2009
5
0
Kazi ni kwako....
 

Attachments

  • Ewura Fuel Price Build up.zip
    845.8 KB · Views: 79
  • Ewura Fuel Price Build up.pdf
    1 MB · Views: 119
NGELEJA KAONDOE HARAKA SANA PASENTI YA 'GHARAMA ZA SAIDIA CCM ISHINDE'
KWENYE BEI ZETU ZA MAFUTA NCHINI AU MSUBIRI KUJIKAANGA WENYEWE SIKU SI NYINGI NA HILI KASHFA NZITO LA MAFUTA NCHINI


Kwa hili la mafuta, CCM wanalo safari hii; Wadanganyika tayari wameshtuka - wafanyabiashara kwa watumiaji wa mwisho!!!!!!!

Sana sana labda CCM wajiamulie tu mapema kabla mambo hayajaingia kwenye ngwe ya pili ya wananchi watumia mafuta kujiunga kwenye maandamano kwa pamoja na wafanyabiashara wa mafuta nchiilio kuondoa MIZIGO KERO ya miaka mingi sasa CCM kujipenyezea gharama za ziada kwenye bei ya kila tone la mafuta iingiayo nchini.

Kwa kweli ni masikitiko makubwa sana kuona wananchi tulivyomasikini wa kutupwa nchini nabado chama hiki kiendelee kututwisha mzigo wa kudumu wa kugharamia chaguzi za CCM kila tunaponunua mafuta nchini!!

Busara zinasema kwamba afadhali CCM kiondoe mapema zaidi kabla ya mambo kutifuka na kuchafuka zaidi nchini; hizi 'GHARAMA BLACK MARKET' AU MGAO WA GHARAMA YA 'SAIDI CCM ISHINDE UCHAGUZI' iliopachishwa kwenye bei ya kila tone la mafuta aina zote tunazonunua nchini ili bei iweze shuke; wafanyabiashara nao wapate japo kafaida zaidi na wananchi tukapate ka-ahueni baada ya kulitua chini hili ruba CCM kujibandika.

Katika hili la kupandisha gharama ya mafuta nchini ili mkakidhi mahitaji binafsi ndani ya chama, chaguo ni lenu CCM; kusuka au kunyoa!!!!!!!
 
CCM kikituondolea huu mzigo wa 'GHARAMA YA UCHAGUZI' kwenye Price Structure za bei za mafuta, maji na umeme basi kwa haraka sana maendeleo yatapatikana nchini, wawekezaji kuongezeka, ajiri kurejea, unafuu wa bei za bidhaa na huduma kushuka, gharama ya maisha kuwa nafuu zaidi nchini na uchumi wetu kukua zaidi!!!

Mzee wetu Mkuu wa EWURA, mbona hili unalifahamu sana na jinsi Watanzania tunavyohenyeshwa kila siku na gharama kiinimacho kwa faida binafsi ya CCM.

Kumbuka, baada ya kustaafu lazima Watanzania tutakuhoji juu ya hili sawa na jinsi ambavyo Mzee Makame alivyonatiwa na kashfa ya kudumu la kulichakachulia CCM uchaghuzi wetu.
 
Hayo mafaili hayafunguki (huenda cmptr yangu ina virusi).
Iweke nzimanzima jomba tufaidi wote bana!
 
HIVI NI MTU GANI AU CHAMA GANI NCHINI ILIYOJIFICHA NYUMA YA
SHIRIKA MFUU LA TIPER NA KUTAFUNA PASENTI 18 ZA FEDHA WATANZANIA KILA
TUNAPONUNUA MAFUTA NA KUCHANGIA KUTUPANDISHIA
GHARAMA ZA MAISHA KIASI HIKI????


Wasomi wa hapa JF na Tanzania kwa ujumla; inakua vipi mambo ya msingi ya kuitajika kushikilia bango mpaka kieleweke tena yenye maslahi makubwa kwetu sisi wananchi wote??

Nahoji kwamba inakua vipi kwamba wala hatuonekani kupenda kujadili kwa kina wakati mwenzetu SANTA kafanya kubwa ajabu kutuwekea hadharani hapa DATA za kufa mtu?? Kila mtu akamuelimishe watu kumi mara baada ya kusoma hii songombingo ya CCM na jinsi wanavyoinyonya nchi bila huruma!!!!!!

Watanzania wote tuamke sasa hivi na kila mtu afungue hii PDF na kudadavua zaidi vijipasenti ambavyo ndivyo vinavyotufanya tuwe masikini kiasi hiki bila ajira wakati wengine wamejikalia tu Masaki wakiangalia tu billioni ngapi zimeingia benki kwa saa kwa kila Mtanzania yeyote anaponunua badhaa yoyote ya petroli?????????

Ni nani huyu aliyejipachisha jina la TIPER (shirika lililokufa siku nyingi nchini) na kuendelea kuzoa 18% kwa li lita ya mafuta aina yoyote ile (katika familia ya bidha zitokanazo na petroli) nchini na tena sisi kuendelea kumzawadia senti 20 zaidi juu ya ile pasenti 18???

Haruna Masebu, Jairo, Ngeleja, Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mzee NdiaMukama pamoja na Rais Kikwete tupeni jibu juu ya haya.

Mwisho, kila mmoja wetu akae akijua ya kwamba ni UONGOZI WA PASENTI nchini ndiyo inayofanya maisha yawe ya gharama yasioshikika kiasi hiki.

Ni sharti tupige kelele sote kwa pamoja juu ya hili tatizo sugu la PASENTI YA CHAMA katika mafuta hapo ndipo bei za bidhaa viwandani vitapata kushuka, nauli mijini na mikoani kushuka zaidi.

Ndio, nasema kwamba hata na ujenzi nayo kote nchini utaweza kufanyika zaidi kwa unafuu, uwekezaji kuongezeka, ajira kuongezeka zaidi, kipato kuboreka kwa kila mmoja wetu na MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA kuwezekana zaidi ya vijikauli mbiu tu kwenye jukwaa za siasa kupata nafasi za uongozi.
 
Huu ni wizi wa jumla

Tiper fee... take it out or at least weka 5%, kama WMA wanachukua 1.00 then sijui kwanini tiper wanalamba
\
aisee
 
This is bongo bana the gvt inakunguta 539 shilingi kwa kila lita ya mafuta tunategemea yashuke bei ? ukiweka za EWURA na wenzake ni jumla ya 602.
 
This is bongo bana the gvt inakunguta 539 shilingi kwa kila lita ya mafuta tunategemea yashuke bei ? ukiweka za EWURA na wenzake ni jumla ya 602.

Tafadhali karekebishe kauli hapo penye wino mwekundu.

Ni CCM iliyokaa majuzi Dodoma na kuanza kutoa chozi la mamba kwenye ugumu wa maisha kwetu ndio wanaotafuna hiyo hela kila Mtanzania kila sekunde tukingapo mafuta aina yoyote ile.

Kwa msingi huu, gharama za uchaguzi kwa faida ya CCM tunalazimika kubeba sote hata kama wewe ni mwana-TLP.
 
Mbowe na zito alisema bungeni kuwa tozo ndogondogo hata zikitolewa bei ya mafuta haiwezi shuka na akashauri serikali ipunguze kodi kutoka sh 539 hadi sh 250 then mafuta yatapungua kwa sh300 then hii itafanya petrol iuzwe kati ya sh 1700 hadi 1750,hii ingekuwa nafuu jamani lakini serikali imekataa.
 
Tatizo ni kwamba wazo hata likiwa zuri kama nini lakini likitolewa na mwakilishi wa kambi ya upinzani basi tayari CCM linaona wanategwa mahali wakati Tanzania ni yetu sote tu!

Wazo hilo hapo chini na mchanganuo wake hakika ingalikua tiba tosha kwa mashaibu yanayoikumba uchumi wetu hivi sasa.

Mbowe na zito alisema bungeni kuwa tozo ndogondogo hata zikitolewa bei ya mafuta haiwezi shuka na akashauri serikali ipunguze kodi kutoka sh 539 hadi sh 250 then mafuta yatapungua kwa sh300 then hii itafanya petrol iuzwe kati ya sh 1700 hadi 1750,hii ingekuwa nafuu jamani lakini serikali imekataa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom