How Air Tanzania Should be Restructured

Mkuu Mkandara,
nimekuoata maelezo yako, lakini ukweli ni kwamba ATCL kama ilivyo sasa haina mvuto kwa wanunuzi hasa katika mfumo wa hisa. Watu wanaponunua hisa wanatarajia kupata dividends kutoka kwenye faida itakayotengenezwa. Sasa ukiangalia ATCL haitengenezi faida zaidi ya hasara, kwa mantiki hiyo hata ukisema uzipenyeze kinamna-namna pale kwenye soko la hisa hakuna atakayeweza kuzinunua kwani kwa ukizinunua maana yake utapata hasara na kama mtaji kako katakwenda na maji.

Kitu ambacho kinaweza kufanyika ni mwenye mali sasa hivi kwa maana ya serikali kutafuta mbia ambaye watajumuika kuiendesha ATCL endapo serikali itaona haiwezi kubeba mzigo wa risk at 100%.

Baada ya hapo endapo kampuni itaanza kutengeneza faida kutoka katika operations zake (Operating Profit), kuweza kuonesha kuwa kunauwezekano wa faida kuongezeka na kuimarika kifedha nk, then
hapo hisa zake zitaweza kupanda thamani na kuuzika.

Au njia nyiingine ni serikali kubaki peke yake na kufanya mikakati ya kuliimarisha na hatimaye kufikia kiwango cha kuridhisha kuweza kupata faida nk kama nilivyoainisha hapo juu.

Au njia nyingine serikali kuiuza ATCL kwa mmiliki mpya, lakini katika hali ilivyo sasa ATCL atakayenunua ndiye atakaepanga bei.
 
Pundamilia07,

Mkuu nimekusoma.. Hizi ni Option tatu ambazo zinaweza kuchukuliwa... na sisi hapa nadhani tunajadili na kubadilishana mawazo kipi kizuri kinachoweza kufanyika..
Binafsi naamini kabisa kwamba ATCL inatakiwa kuwa overhauled na restructuring iwe ktk mfumo wa shirika binafsi in form of Public company, na huwezi kufanya hivyo bila kuuza share ambazo kwa mtazamo wangu DSE is the right place...
Ni vigumu leo hii watu kununua share ATCL kwa sababu Uongozi uliopo hauwapi wananchi matumaini kuwa shirika hilo linaweza kuibuka upya..then kitu cha kwanza ni kubadilisha kabisa Uongozi na nafasi ya serikali (wanasiasa) ktk kuendesha shirika hilo..
Mkuu kumbuka kwamba tumeuza mashirika yetu zaidi ya 3,000 ambayo yalikuwa hayazlishi na kati yake kuna viwanda..
Lakini yote yaliuzwa tena wanunuzi walipangana ikiwa na maana sio swala la viwanda au mashirika yenyewe kuwa na upungufu isipokuwa tatizo lipo ktk Uongozi.. Muhimu zaidi kwa wawekeshaji ni soko lililopo, na hakuna ushindani zaidi ya shirika moja la mtu binafsi Precision...
Hivyo, nina hakika watakao faidika na uwekeshaji ATCL ni watu wa kwanza kununua share ambao watakuwa na maamuzi ya uongozi wa shirika hilo..Mara nyingi mashirika yanayouza share huwa na vichwa ktk board of Directors na hakuna Mungu mtu...halafu wakati huo huo ushirikiano wa Ubia na shirika kama Emirates au Gulf Air utalipandisha hisa within no time..kwani wafanyabiashara toka mikoani wataweza kukata ticket zao huko huko na kuunganisha na ndege hizi Dar au Kili kwenda Arabuni au Ulaya..Hivyo soko la ndani kwa ATCL litapanda ghafla!..

Kubomoa Utawala wa ATCL kuondoa wanasiasa ni muhimu sana, serikali inatakiwa haraka sana kuweka mkakati wa stimulus wakati kama huu na kukubali shirika hilo lijiendeshe kama shirika la biashara..Na tujenge fikra za kufahamu kwamba Mali ya Tanzania sio lazima iwe inamilikiwa na serikali isipokuwa wananchi wenyewe..serikali ni watu zile fikra za kijamaa pamoja na fikra chafu za Ubepari maskini kuwa ni wageni wanaoweza kuijenga Tanzania hazina nafasi kabisa ktk dunia ya leo..Tazama yaliyotokea shirika la reli!..bado serikali yetu inashindwa kuelewa kwamba wanachotakiwa wao kuweka ni regulations ku secure na ku protect interest maslahi ya Taifa..
Hizo hatua nyingine zote zinaweza kufanyika lakini tukumbuke tu uwezekano mkubwa wa Taifa letu kufanikiwa ni ktk muundo huu zaidi ya ile mingine ambayo inaweza kuzaa tatizo tata la usafiri nchini kiasi kwamba tukakubali kushindwa na nchi ikachukuliwa na Mabapari wa nje..
 
...restructuring, giving more money to ATCL or forcing mattaka out none of that is going to produce anything positive,why? it has been tried & failed...acha wafe tuu na wenye pesa na kujua airline industry watakuja tuu,hawa na TANESCO ni cancer wanatakiwa kufutika kabisa!
 
Koba, Nadhani bado hatujaelewana.. Unapo overhaul kampuni nzima ina maana wote wanaofanmya kazi sasa hivi watapitiwa uwezo wao, umuhimu wa kazi zao na kadhalika ili kubakia ktk shirika.
kama alivyosema Mwanahalisi, haiwezekani shirika kuwa na wafanyakazi 300 wakati shirika lina ndege chache.. Ukitazama sehemu za kukatia ticket, hakuna haja ATCL kuwa wao pia mawakala wa ticket badala yake wananchi watafungua maduka ya kuuza ticket after all siku hizi ni mtandao unamaliza kazi zote..
Kwa njia yoyote ile ni lazima shirika lifanyiwe restructuring iwe tumeuza au vyovyote vile, muhimu tuwe na usafiri kwa sababu navyofahamu akili ya mwafrika sisi akina ndivyo tulivyo.. kama shirika la ndege litauziwa mtu binafsi basi kinachofuata ni viwanja vya ndege kutofanyiwa ukarabati kabisa kwani seriikali itaona hakuna umuhimu..Na matokeo yake ndio kama huko Shinyanga ndege za Barricks zinashuka na kuruka bila kukaguliwa...The next thing tutauza rada na kila kitu kinachohusiana na anga!.. Ndivyo tulivyo akili ya maskini akianza kuuza nguo zake basi hataachia hapo..
Jamani fikirini nayosema msitumie hasira zetu kwa yote yaliyowahi kutokea.. badala yake tujiulize tumejifunza nini na wapi yalikuwa makosa yetu kwani shirika la ndege kama shirika halina makosa wala hitlafu isipokuwa sisi wenyewe...
Koba nitakupa mfano hai wa lawama za kiswahili, unajua siku zote wanaume huwalaumu wanawake kuwa Tasa? yaani hawazai wakati kisayansi inajulikana kwamba Ni wanaume waoatunga mtoto na kuna asilimia kubwa ya wanaume hawana kizazi kuliko wanawake ambao mara zote utasa wao hutokana na maradhi ya wazi kabisa kuliko mwanamme.

Lakini hata siku moja mswahili hawezi kuamini hivyo na kila siku wanawake ndio wanaachwa kwa matusi mazito kuwa hawazai..hivyo mkuu tuwe na uhakiika na maamuzi yetu ktk swala hili badala ya kushusha lawama tu kwa shirika ATCL kumbe wanaume wenyewe ndio matasa!
 
Iuzwe tu! Mbona waSwiss na waZambia wameweza? Pesa zitakazookolewa ziwekweze kwenye usafiri wa reli! Tuongeze tracks na twende kwenye umeme badala ya diesel.

Amandla......

Fundi Mchundo AKA FTC:

Tunarudi pale ya kuruka vipande vya chupa na kukanyaga miiba. Usafiri wa ndege unaitajika Tanzania.

Na usafiri wa reli vilevile unahitajika. Na usafiri wa meli na mabasi unahitaji.

Tusichohitaji ni usafiri wa kutumia ungo tu.

Kuna utafiti nimeufanya kuhusiana na watanzania. Na kama ningepata wadhamini au sehemu ya kupeleka paper ya utafiti wangu, ningeweza kutoa matokeo ya utafiti.
icon10.gif

Katika utafiti wangu nimegundua kuwa mashirika mengi ya kitanzania yana muundo hulehule unaofanana kiutendaji. Kutakuwepo na mkurugenzi, bodi ya wakurugenzi na mambo wengi. Hawa watataka kuwa na ofisi, magari na kuishi Osterbay kwa gharama za mashirika. Na sehemu zenye matawi zitakuwa na mameneja.

Tunachosahau ni kuwa gharama zingine zinazochangia kuua kwa mashirika ni muundo wa mashirika yenyewe. Unapopanga nyumba ya meneja Osterbay na shirika ku-spend dollar 4000 kwa mwezi, ni kuwa mnaliongezea shirika mzigo. Na shirika linavyokuwa na watendaji wa ngazi za juu wengi, ndio matumizi yanapoongezeka na profit margin zinapopungua.

Kwa maoni yangu, shirika la ATC lenye ndege chini ya 5, linatakiwa kuendeshwa very simple. Iga model ya Southwest. Southwest ilipoanza meneja alikuwa anafanya kazi ndani kama kukiwa na upungufu wa Hostess.

Inawezekana kuwa na-sound kama aliyekosa akili, lakini huwezi kuwa na structure ya uongozi wa airline yenye ndege 20 kwa airline yenye ndege mbili tu.
 
Habari zilizoingia hivi punde zinasema wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya precission wanajiaandaa kuipeleka management ya ATCL
mahakamani kutokana na kukaidi kulipa pesa za saccos ambazo wafanyakazi hao wamekuwa wanachama kwa miaka mingi..pamoja na wafanyakazi wa ATCL.

A kiongea bila kutotaka kutajwa jina baadhi ya wafanyakazi walikusanyika jana wakiwepo wafanyakazi wa swissport na BP
na kuamua kwa pamoja kuipeleka menejiment ya atcl mahakamani kuweza kupata haki zao.....

Akizungumza kwa jazba mmoja wa wafanyakazi wa Swissport alisema namnukuu "UNAJUA SISI NI WANACHAMA WA CHAMA KIMOJA CHA KUKOPA NA KULIPA kijulikanacho kama WANAHEWA
sasa kila tukienda viongozi wanatuambia wanaidai atcl million 425
kila tukiombahata pesa kidogo tunakatiliwa kabisa wakati ni haki yetu na kusema pesa zote wameshikilia manegement ya ATCL..."

Chanzo chetu kilijitahidi kumtafuta mkurugenzi wa ATCL bw David Mattaka bila mafanikio na kuambiwa yuko kwenye mkutano...
habari zaidi zinasema baadhi ya wafanyakazi wa Swissport na Precission leo hii waliamua kwenda kumuona mkurugenzi na kukosa ushikirikiano... kibaya zaidi wakati tukiwa tunajitahidi kuendelea kujua ukweli wa swala hilli, baadhi ya wafanyakazi walikataa kabisa kujibu na kusema anayejua hilo ni Mattaka na management yake ...lakini ni kweli wanadaiwa hela nyingi tu na kibaya zaidi kwenye mishahara inaonyesha imekatwa wakati pesa hazipelekwi sehemu husika.....

Nilijaribu kumpa pole dada yule na mwisho kumuuliza kama wafanyakazi mmelijua hili muda wote hamjui ni kosa la jinai kampuni kukata malipo ya mishahara ya mfanyakazi na kutumia bila ridhaa yalke ama mlijulishwa na kukiri hakuna kitu kama hicho kabla ya kuanza kunihuzunsha kwamba hata makato ya PPF hawajapeleka toka mwezi wa tano.....

Swali linakuja hivi PPF mnalijua hili? Na kama kweli kama ilivyosemwa kuna hatua gani zaidi zinafanyika kuhakikisha malipo ya kila mfanyakazi yanawafakia katika muda unaotakiwa...iweje kampuni ya mohamed entrp..ikae mwezi mmoja bila kulipa muwafikishe mahakamani na kuwaachiia viongozi wa atcl wakicheza na maisha ya watu...je hamjui hivi sasa wafanyakazi ikatokea wakaomba kustaafu hamuoni usumbufu mtakaoanza kumfanyia mfanyakazi huyu aliekaa kwenye kampuni zaidi ya miaka 25....

JE na hao wafanyakazi wanampango gani kuhakikisha pesa zao zinazokatwa zinalipwa sehemu husika?

Hakuna sheria yoyote inaowafikisha hawa viongozi mahakamani na kama ipo JF tunaitaji kuwakomboa watu kama hawa, haiwezekani mtu anajua PPF yake haijalipwa toka mwezi wa tano mwaka jana na akakaa kimya lazima kuna kitu hapa katikati...

Serikali kabla ya kuamua kupunguza kazi wafanyakazi wa ATCL mkawasaidia kwanza kuwalipia malimbikizo yao ambayo menejimenti ya atcl iliamua kuzichukua pesa zao bila taarifa na kushindwa kuzifikisha panapoitajika..kuliko kuwapunguza na kuanza kuwapa usumbufu wakati wa kudai haki yao

Kwa hao wafanyakazi mnaojipanga kwenda mahakamani hakikisheni mnampata wakili anaejua sheria za kazi aweze kuwasaidia ...kwa hili halina tofauti na kuwaibia wafanyakazi.....

Mh NYANGANYI....kweli unawezaje kuongoza viongozi wanamna hii wanaoamua kutumia hadi pesa za wafanyakazi pasipokujua...huoni kuna umuhimu wa kuwawajibisha wahusika haraka iwezekanavyo....

Nawatakia mafanikio mema ,na kutoa ushauri muwe makini huko muendako.......turufu mahakamani imeamua kutawala utu wa watu
 
...wakuu socialism does not work and its time for government to deregulate and get out of the market. We all know that state ownership is a way for corrupt and incompetent,why enrich mafisadi and cheat the people of development,why give more money to a dead company...better loan precision or any other company hapo tax yetu itafanya kazi na atleast inaweza kurudi
 
Koba,
wakuu socialism does not work and its time for government to deregulate and get out of the market. We all know that state ownership is a way for corrupt and incompetent,why enrich mafisadi and cheat the people of development,why give more money to a dead company...better loan precision or any other company hapo tax yetu itafanya kazi na atleast inaweza kurudi
hata sisi tunaona hivyo hivyo isipokuwa ATCL kama shirika sasa hivi inahitaji msaada kuwa bailed out..Ondoa kabisa mawazo ya hao viongozi... ktk issue hii..chukulia kama hakuna mtu hivi sasa.
Hivyo badala ya kufanya kama Marekani sisi tunafanya kinyume nikiwa na maana kuwa mashirika yanayoomba fedha Marekani ni mashirika binafsi ambayo yanataka msaada wa serikali.. Sisi tanzania ATCL ni shirika la serikali na linahitaji msaada... kwa hiyo tunachofanana hapa na Marekania ama nchi za Ulaya ni ile kuwa bailed out lakini sasa regulations zetu zitakuwa tofauti na zile za Ulaya..
Wakati wao waki regulate kuweka accountability - sisi tunatakiwa ku deregulate sheria ya Umilikaji huo mkono wa state ownership, lakini bila kufanya makosa ambayo yamewafikia nchi za Ulaya na Marekani mashirka hayo kufa tutaweka regulations za Accountability.. Hivyo tutaweka regulations ambazo zitazingatia kwamba ATCL ni shirika binafsi linalojiendesha hata kama serikali itakuwa na share yake ndogo kutokana na dhamana yake..Kifupi hakuna Responsibility without Accountability.. ndio lugha mpya ya Mtanzania.
Ni kazi ngumu sana lakini ni lazima tuweke mguu ktk kuikoa ATCL kama shirika la Tanzania ambalo wananchi wanaweza kujivunia..Kwa hiyo kuna kuachia kamba serikali na kulegeza masharti ya Kijamaa kisha kuweka masharti ambayo yatawabana viongozi wa shirika hilo kuwa Accountable...
tazama nchi za Nordic, serikali zao ziliwawezesha wananchi wake wenye Idea endelevu ktk innovation...lakini tazama Bongo kwetu bado kabisa siasa zinatumika ni zile za Kifisadi fisadi tu..
Mtu amesoma chuo kikuu na kapanda hadi darini (Phd), kisha kavumbua kitu huyo mtu ataambiwa kwanza ili apate Certifacate of incentive anaambiwa kwanza anatakiwa awe na 1,000,000.. acha mbali gharama za registration...
Sasa huyu mtu katoka shule kasoma miaka zaidi ya 25 tunategemea atazipata wapi dollar 100,000!..Kuna regulations ktk uanzishaji mradi ambazo hazina hata kichwa wala miguu wakati kwa wageni ni poa kabisa.. haya hao Diasporas wanapotaka kurudi nyumbani na kufungua miradi yao utasikia serikali ikidai ni lazima wawe na kitu kama dollar 300,000..
Sasa kama mtu huoni kwamba mfumo kama huu ndio chmbuko la Rushwa, hongo na mafisadi inashangaza sana!.. Hata kama mimi ndio mtoa liseni nikijua una 1,000,000 na kibali changu ndicho pekee kitakuwezesha wewe kufanya hayo unayotaka wakati mimi hali yangu Mungu tu ndiye anajua.. nitaomba unitoe mkuu wangu..Na ukisha nikatia mimi tu wengine watafuata..
kwa hiyo regulations nchini ndilo tatizo kubwa la Rushwa nchini na wale wenye nafasi za wadhifa wanazitumia.. bado kuna Ujamaa na siasa nyingi ktk uchumi wa nchi zetu..
Binafsi nashindwa kabisa kuelewa haya kwani nchi hizi hakuna kitu rahisi kama kuwezeshwa kufungua mradi wako maadam tu idea business plan yako imekamilika. Kuna kijana wa Kibongo kaingia less than five years ago hata hata dollar 100, kapiga box, kajipanga vizuri na kaanzisha mradi wake, leo hii na kachukua risk leo hii anazungumzia gross income ya dollar 1,500,000 kwa mwaka..Kila alipokwenda kawezeshwa kutokana na nuru ya biashara yake kulingana na business plan yake..

Kwa hiyo mkuu mimi ni Conservative na hakuna mwanzo wa mrengo huu kama kumwezesha Mtanzania kuanzisha/kumiliki mali ya nchi yake at low tax rate.., na pili mkono wa serikali ktk maswala ya Uchumi unaishia kwenye sheria ambazo ni rahisi kwa mwananchi wake na ngumu kwa mgeni - status quo....unless kuna makubaliano ya kibiashara kati ya nchi mbili bila ujanja ujanja....Mzawa kwanza!
Na mwisho sikubaliani kabisa na matumizi ya kijinga.. hii mishahara ya mameneja, wabunge na wanasiasa kufikia kununuliwa mashangigi, kupangishiwa majumba ya gharama kubwa, na misafara isokuwa na umuhimu..yote haya dniyo nayopigania kila siku..
Hivyo kuiokoa ATCL ni kuitoa mikononi mwa serikali na kuwauzia wananchi wenyewe kisha ile lugha ya kuwajaza watu mahela itumike kuijaza ATCL kwani kufanikiwa kwake ndio kufanikiwa kwa wananchi na taifa kwa Ujumla..
 
Mkandara,
Mimi nadhani nimekuelewa vizuri nia yako kuwa ATCL itoke kwenye mikono ya serikali na kwenda kwa watu binafsi. Mimi sina tatizo juu ya hilo na hata serikali pia haina tatizo katiika wazo lako.

Lakini kitu kimoja ambacho ni kikwazo kwa ATCL juu ya wazo lako ni kwamba, ATCL haina sifa ya kuwa listed katika soko la hisa kwa sababu kubwa kuwa is not profitable for the time being. Nobody will be ready to invest to the company ambayo inapata hasara. Kwa kuwekeza hapo maana yake ni sawa na kutupa fedha ndani ya bahari au chooni, hapa hakuna tofauti kabisa.

Jambo ambalo linaweza kufanyika kama ambavyo nilishauri hapo mwanzo ni kuwa, mwenye mali agharimie kuliweka shirika hilo katika hali ya kuwa profitable na vilevile lifikie kiwango cha kuridhisha cha kuaminika. Au mwenye mali apatane na mtu ambaye anaona kuwa kwake ATCL ni potential na yuko tayari ku-risk mtaji wake. Hawa wawili au mmoja wao anachokifanya ni kujaribu kuiondoa ATCL hapo ilipo lakini haimuhakikishii kuwa kwa kufanya hivyo atapata faida mara moja , inaweza kuchukua muda kadhaa kutegemea na mikakati yake yake ya kibiashara.

Juu ya mashirika mengine ya ndege ku-merge na ATCL, hilo linategemea ni mkakati gani wa kibiashara mashirika hayo wanayo, pia hakuna kampuni yeyote sasa hivi duniani katika kipindi hiki cha machafuko ya kiuchumi itakayowekeza mahali pasipo kuwa na faida. Kwa mashirika kama Emirates, ATCL kwao si lolote na wala hawahitaji kufanya hivyo kwani mikakati yao kwa sasa hivi juu ya soko la afrika mashariki ni ya muda mrefu kwa maana yeyote yule aidha ni ATCL wenyewe au waungane na shirika jingine, bado Emirates itakuwa iko within. Hawa wakubwa hawaihitaji ATCL kwani haiwasumbui katika shughuli zao. Endapo kwa namna moja au nyingine ATCL ingekuwa inahatarisha market share ya Emirates, basi wangeweza kukaa na kufikiria jambo lolote.

Jambo kubwa ambalo limeikumba ATCL ni kukosa uongozi mzuri na imara ambao ungeweza kuwa na maono mazuri na makubwa katika kuendesha biashara ya usafiri katika zama hizi ambazo zinachangamoto nyingi za kuendesha mambo. Kuna jambo ambalo Zakumi ameligusia kuwa uendeshaji wa makampuni yetu Tanzania upo katika pattern ambayo inafanana kutoka shirika moja hadi jingine, hili ninakubaliana nalo kwani miundo ya leo inahitaji ni ile itakayo endana na shughuli za kampuni. Japokuwa maongelea juu ya marupurupu kama nyumba nk lakini mimi huko sina tatizo. Ninavyoona mimi kuwa jinsi uchumi wa dunia unavyokabiliwa na changamoto mbalimbali na kuongezeka teknolojia kwa kiwango cha juu, miuundo ya mashirika iwe ni kwa ajili ya kukidhi malengo na mikakati ya uwepo wa shirika husika. Na huu muundo na shirika unaweza kubadilika kwa kutokana na mahitaji ya wakati.
 
Last edited:
...wakuu socialism does not work and its time for government to deregulate and get out of the market. We all know that state ownership is a way for corrupt and incompetent,why enrich mafisadi and cheat the people of development,why give more money to a dead company...better loan precision or any other company hapo tax yetu itafanya kazi na atleast inaweza kurudi

Corporate Socialism does work ;)
 
Sasa hapa inabidi tujifunze, je hizo ideologies zina nafasi yeyote kweli kati uchumi wa dunia leo hii?

Tuiangalie Marekani, Russia, China halafu tuoanishe na maneno yetu.

Ninashauri tunapotaka kuangalia mbele haina maana tuangalie na kuhitimisha yale tunayiyaona katika upeo wetu wa macho tu, tujaribu kukaa na kufikiri, tutaoanaje yale yaliyo nje ya upeo wetu wa macho?

Ukiangalia yalipo ndani ya upeo wako wa macho nadhani uutaishia kuongelea juu ya pesa ya walipa kodi,

Lakini ukiweza kuangalia zaidi ya upeo wako wa macho utaona kuwa kuna tatizo la employment kwa vijana, tatizo la nchi kujitosheleza kwa wataalam katika sekta mbalimbali (kumbuka utaalam ni bidhaa inayouzika kama bidhaa nyingine), nk.

Kiuchumi inaaminika kuwa kuimarika katika yale ambayo yanatokana na kuwepo kwa shughuli mama, basi mengine yote yataimarika kwa ujumla wao na yanakuwa na manufaa katika matumizi ya pesa ya walipa kodi kwani faida inawarudia waliolipa kodi hiyo, unemployment itapungua, wataalam wataongezeka nk .

Ni muhimu kwa serikali kuimarisha Air Tanzania lakini kwa kuhakikisha kuwa italeta tija kwa nchi na wananchi wake.
 
Last edited:
Pundamilia,

Mkuu wangu mashirika mengi nchi hizi yameingia Public yakiwa hayana sifa kubwa ya faida isipokuwa future yake ndio inawafanya watu wacheze kamari. Wall street mkuu wangu ni kamari na mara nyingi wenye kuona mbali ndio hufaidika na pato litakalotokana na uwekeshaji..Ktk mfumo huu wa soko kuna Uwazi na Accountability..hivyo agharab kesho kuanza kuulizana ilikuwaje?
Kinachotakiwa kuwavuta wawekeshaji ni mpangilio wa shrika zima kimalengo na matumaini, hali ya Usafiri wa anga sehemu hiyo, connection za kwenda nje na kadhalika..Hata Google na mashirkka mengi humu tumewekesha yakiwa hayana faida kabisa mengine yameingia Public ili kupata mtaji tosha wa kuweza kuendelea iwe kutokana na mtaji mdogo au demand kubwa supply ndogo na kadhalika..
Sisi Wawekeshaji tunatakiwa kusoma alama hizi, tupige ramli za kisomi na sio kusubiri hadi umeskia shirika la Bia na sigara yanaingiza fedha kuliko yote ndio ununue share wakati zimepanda hazishikiki..Au Barriccks ni shirika kubwa la kuchimba dhahabu ndio uingie..ndio mwanzo wa kubambikiwa figures.
Wajanja wote huingia mashrika madogo yenye kuuza share zake chini wakijua kwamba biashara hiyo itakuja panda..
Yes, nikirudi ktk WATU na MAZINGIRA nakuelewa sana kwa sababu hata biashara ndogo Wadanganyika husubiri mtu mmoja aanze, wakiona inaingiza fedha ndipo wote wataivamia.. kama kwenda China...Yet hii isiwe sababu kubwa kama wasomi wapo na watu wanaotakiwa kuwekesha ATCL ni wenye uwezo ambao nina hakika wana wataalam ktk maswala ya Uchumi na mazingira yetu.. Location na soko letu (demand) ambalo halina ushindani zaidi ya Air Precision ni kubwa sana hasa ukizingatia Population yetu. Hata kama asilimi 10 tu ya wananchi wana uwezo wa kupanda ndege ni mauzo ya ticket millioni 3 kwa mwaka..nauli zetu ni kubwa kuliko North America na watu wanadai usafiri wa anga kila siku utaambiwa ndege imejaa..

Pili, kivutio kingine kikubwa kuungana na mashirkka hayo aidha Emirates au Gulf na asikudanganye mtu mashirika yote ya Ulaya yanaanguka kutokana na competition kuwa kubwa.. Hapa nilipo kuna mashirika ya ndege ya ndani yasiyopungua 20 wakati nchi nzima ina population sawa na Tanzania. Now, lets say wao asilimia 80 wanauwezo wa kupanda ndege lakini kuna ndege mara elfu zaidi yetu zikiruka kila dakika..
Emarites wanafahamu soko la Tanzanioa hasa kutokea Dar na wanajua wazi kwamba over 70% ya wasafiri wanatoka bara ambao hulazimika kuja Dar kukata ticket kwa ajili ya Usafiri wa nje. Na wanapofika Dar wanakuta mashirika mengine ya ushindani zaidi ya matano..

Hivyo ukiwapa data za kuonyesha kuwa wasafiri wanaochukuliwa BA, KLM au Swiss air wengi wao wanatoka bara, pia ushirika wao utapunguza karaha za wasafiri kuja Dar kukata Ticket kwa kutumia ATCL, bila shaka Emirates watakuwa interested sana kwani wataua ndege wawili kwa mara moja..
Hayo mashirika yote ya Afrika yaliyoungana na mashrika ya nje sio kwa sababu yalikuwa yakifanya vizuri.. as a fact mashirika mengi yalikuwa yakifanya vibaya isipokuwa yamekuja inuka baada ya kuunganisha na mashirika ya nje...Toka Zambia Airways, hadi Kenya Airways mapato yao yamezidi toka wajiunge na mashirika ya nje, kifo cha mashirika ya ndege duniani alama zake zilianza miaka iliyopita mkuu wangu.. sii Bongo tu..
Hata hao NWA walikuwa miguu juu wakachukuliwa na Delta kwa sababu ya baadhi ya safari zza nmdani NWA ataweza kuwaunguanishia wasafiri wanaokwenda Asia na Europe kwa hivyo NWA end up to be a profitable deal akuinunua.
Just imagine kwa nini msafiri toka Mwanza aje hadi Dar kuchukua BA au KLM wakati anaweza kabisa kukata ticket ATCL toka Mwanza na akapata connection Kili au Dar ambayo Emirates watamfikisha London kesho yake..Zile gharama za kulala Dar, karaha za kutafuta ticket ambazo unaweza ambiwa full booked hadi next week zinaondoka..

Ndio maana nasema inatakiwa watu wakae wakune vichwa kabla ya kufikiria kutupa bahati hii ovyo tukajutia kesho, Hiyo Option ya pili pia nzuri lakini nionavyo mimi kutokana na watu na mazingira yetu swala la Bakhresa pekee kuchukua ATCL litakuwa na utata mkubwa zaidi ya kuwekwa sokoni..Bakhresa atanunua hisa na kuwa ktk board ya wakurugenzi na kutakuwepo vichwa vingine ambavyo wananchi kina yakhe sisi tuliona Bakhresa kaingiza fedha tutafuata...Maadam ni shirika la serikali hadi sasa nadhani kuwapa wananchi nafasi sawa ni it's good Politics kuliko zile za uuzaji nyumba!
 
Pundamilia,

Mkuu wangu mashirika mengi nchi hizi yameingia Public yakiwa hayana sifa kubwa ya faida isipokuwa future yake ndio inawafanya watu wacheze kamari. Wall street mkuu wangu ni kamari na mara nyingi wenye kuona mbali ndio hufaidika na pato litakalotokana na uwekeshaji..Ktk mfumo huu wa soko kuna Uwazi na Accountability..hivyo agharab kesho kuanza kuulizana ilikuwaje?
Kinachotakiwa kuwavuta wawekeshaji ni mpangilio wa shrika zima kimalengo na matumaini, hali ya Usafiri wa anga sehemu hiyo, connection za kwenda nje na kadhalika..Hata Google na mashirkka mengi humu tumewekesha yakiwa hayana faida kabisa mengine yameingia Public ili kupata myaji tosha wa kuweza kuendelea iwe kutokana na mtaji mdogo demand kubwa..
Sisi Wawekeshaji tunatakiwa kusoma alama hizi na sio kusubiri hadi umeskia shirika la Bia linaingiza fedha kuliko yote ndio uingie, Au Barriccks ni shirika kubwa la kuchimba dhahabu ndio uingie.. Wajanja wote huingia mashrika madogo yenye kuuza share zake chini wakijua kwamba biashara hiyo itakuja panda..
Yes, nikirudi ktk WATU na MAZINGIRA nakuelewa sana kwa sababu hata biashara ndogo Wadanganyika husubiri mtu mmoja aanze, wakiona inaingiza fedha ndipo wote wataivamia.. kama kwenda China...Yet hii isiwe sababu kubwa kama wasomi wapo na watu wanaotakiwa kuwekesha ATCL ni wenye uwezo ambao nina hakika wana wataalam ktk maswala ya Uchumi na mazingira yetu.. Location na soko letu (demand) ambalo halina ushindani zaidi ya Air Precision ni kubwa sana hasa ukizingatia Population yetu. Hata kama asilimi 10 tu ya wananchi wana uwezo wa kupanda ndege ni mauzo ya ticket millioni 3 kwa mwaka..nauli zetu ni kubwa kuliko North America na watu wanadai usafiri wa anga kila siku utaambiwa ndege imejaa..

Pili, kivutio kingine kikubwa kuungana na mashirkka hayo aidha Emirates au Gulf na asikudanganye mtu mashirika yote ya Ulaya yanaanguka kutokana na competition kuwa kubwa.. Hapa nilipo kuna mashirika ya ndege ya ndani yasiyopungua 20 wakati nchi nzima ina population sawa na Tanzania. Now, lets say wao asilimia 80 wanauwezo wa kupanda ndege lakini kuna ndege mara elfu zaidi yetu zikiruka kila dakika..
Emarites wanafahamu soko la Tanzanioa hasa kutokea Dar na wanajua wazi kwamba over 7% ya wasafiri wanatoka bara ambao hulazimika kuja Dar kukata ticket kwa ajili ya Usafiri wa nje. Na wanapofika Dar wanakuta mashikrika mengine zaidi ya matano 5..
Hivyo ukiwapa data za kuonyesha kuwa wasafiri wanaochukua BA, KLM au Swiss air wengi wao wanatoka bara,pia ushirika wao utapunguza karaha za wasafiri kuja Dar kukata Ticket kwa kutumia ATCL, bila shaka Emirates wantakuwa interested..
Hayo mashirika yote yaliyoungana na mashrika ya Afrika sio kwa sababu yalikuwa ayakifanya vizuri.. as a fact mashirika mengi yalikuwa yakifanya vibaya isipokuwa yamekuja inuka baada ya kuunganisha na mashirika ya nje...Toka Zambia Airways, hadi Kenya Airways mapato yao yamezidi toka wajiunge na mashirika ya nje..Hata NWA walikuwa miguu juu wakachukuliwa na Delta kwa sababu ya baadhi ya safari zza nmdani NWA ataweza kuwaunguanishia wasafiri wanaokwenda Asia na Europe kwa hivyo NWA end up to be a profitable deal akuinunua.
Just imagine kwa nini msafiri toka Mwanza aje hadi Dar kuchukua BA au KLM wakati anaweza kabisa kukata ticket ATCL toka Mwanza na akapata connection Kili au Dar ambayo Emirates watamfikisha London kesho yake..Zile gharama za kulala Dar, karaha za kutafuta ticket ambazo unaweza ambiwa full booked hadi next week zinaondoka..

Ndio maana nasema inatakiwa watu wakae wakune vichwa kabla ya kufikiria kutupa bahati hii ovyo tukajutia kesho, Hiyo Option ya pili pia nzuri lakini nionavyo mimi kutokana na watu na mazingira yetu swala la Bakhresa pekee kuchukua ATCL litakuwa na utata mkubwa zaidi ya kuwekwa sokoni..Bakhresa atanunua hisa na kuwa ktk board ya wakurugenzi na kutakuwepo vichwa vingine ambavyo wananchi kina yakhe sisi tuliona Bakhresa kaingiza fedha tutafuata...Maadam ni shirika la serikali hadi sasa nadhani kuwapa wananchi nafasi sawa ni it's good Politics kuliko zile za uuzaji nyumba!

Mkandara,
pamoja na analysis yako ndefu lakini je unakubaliana kuwa Emirates wako comfortable na soko la Tanzania? Kwanini wajiingize kwenye ATCL ambayo haina faida kwa sasa? Kama nilivyokueleza hapo awali kuwa ATCL is not profitable kwa hiyo siyo kazi ya Emirates kuifanya ATCL iwe profitable. Kazi ya kuifanya ATCL iwe profitable ni kazi ya mwenye mali kwa sasa. Inshort bidhaa ATCL hainunuliki kwa sasa.

Labda niijaribu kukurudisha nyuma kidogo enzi za PSRC. ATC ilitangazwa mara nyingi na kwa muda mrefu ndani na nje kuwa inauzwa, hakuna shirika lililojitokeza kufanya kununua ATC. Baada ya Sept 11, hali ya bidaa ATC ndiyo ikapoteza matumaini kabisa ya kuuzika. Lakini baadae hali ilipoanza kutulia na kutangazwa tena wakatokea bidders wengine ambapo miongono mwao alikuwa ni South African Airways, Kenya Airways, Precision Air nk. Kati ya hawa SAA ndiye aliyeweka dau kubwa la USD 20m wengine Kenya Airways USD 6m na Precision nadhani USD 3m. Kwangu mimi wote hawa watau hawakuwa serious investors kwani malengo yao wote ni kutawala soko la makampuni yao kwa gharama ya ATC. Nadhani mimi na wewe tumekuwa mashahidi jinsi ambavyo SAA ilivyohakikisha kuwa ATCL inamalizika taratibu na kufutika kabisa. Kenya Airways baada ya kuona hawakuweza kuingia thru bid, wakajiingiza kupitia Precision Air. Si nia yangu kusema kuwa mambo ndani ya Precision Air ni promising, la hasha, Kenya airways bado badoo wako katika mkakati wao wa kuhakikisha kuwa wanatawala biashara hii Afrika mashariki. Kwa kuongezea hapa ni kuwa Precision Air sasa ipo kama tunavyoiona ni kwa sababu ATCL haija-give up, lakini once ATCL ikifutika nadhani black nad white ya existence ya Precision Air ndiyo itajulikana. Sasa basi tusijiachie ili tuje tuandiike tena humu jambo hili hili kila siku, tunahitaji kujituma zidi kuona hali ya baadae itakuwaje. Mfano, Angalia Uganda, in absence ya Shirika la ndege la Uganda, Kenya Air ndiyo inayo-control sehemu kubwa ya usafiri huo kwa sasa hivi na wala hawahitaji kufanaya ubia kama walivyofanya na Precision, je ni kwanini?

Juu ya kununua/ kuuza hisa kwa wananchi, nadhani hapo taratibu za kuandikisha ATCL kwenye soko la hisa haziruhusu kabisa kwani kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na kulinda maslahi ya wananchi. Kama nilivyotangulia kusema kuwa, Mwenyemali anatakiwa kurekebisha shirika kufikia viwango vinavyokubalika ili kuuza hisa katika soko la hisa. Hapa hatuwezi kupindisha utaratibu na kanuni zinazoendesha mamlaka hiyo husika.

Jambo kubw akwa sasa ni kuweka nguvu kwa serikali irekebishe mambo ili wananch waweze kufaidika hapo baadae na umiliki wa shirika lao.

Wakatabahu ndimi Pundamilia
 
Pundamilia,
Mkandara,
pamoja na analysis yako ndefu lakini je unakubaliana kuwa Emirates wako comfortable na soko la Tanzania? Kwanini wajiingize kwenye ATCL ambayo haina faida kwa sasa? Kama nilivyokueleza hapo awali kuwa ATCL is not profitable kwa hiyo siyo kazi ya Emirates kuifanya ATCL iwe profitable. Kazi ya kuifanya ATCL iwe profitable ni kazi ya mwenye mali kwa sasa. Inshort bidhaa ATCL hainunuliki kwa sasa.
Mkuu nitajari bu kukufahamisha mtazamo wangu kwa mifano..
Kwanza nianze na swala la Emirates.. hakuna shirikja ambalo liko confortable ktk biashara za usafiri wangeweza wangeongeza ndege zaidi kuja Tanzania ikiwa kuna wasafiri wengi..Au wangechukua safari za nchi nzima lakini kutonana na sheria na regulations hawana uwezo huo zaidi ya ku run international flights..

Kumbuka mfano niliokupa hapo juu ni kwamba Emirates hawata lazimika kununua ATCL isipokuwa tunashirikiana kibiashara Ubia ambao utamsaidia kila mmoja wetu..
Ubia huu utamwezesha Emirates kuwa na wateja zaidi kwa sababu wasafiri wanaotoka bara wataweza ku book ticket zao toka mikoani na kurahisishwa safari zao kwa connection Dar au Kili..Kwa hiyo Emirates badala ya kuleta ndege moja kwa siku wanaweza kuwa na misafara zaidi ya miwili kwa siku.. Na Upande wetu ATCL itakuwa na wateja zaidi ambao watatoka mikoani wakijua connection ya kwenda Ulaya, Asia au Arabuni unaipata kwa ticket moja tu..hivyo itaongeza soko la ndani kwa ATCL.
Swala la kuuza ATCL mkuu wangu lina utata mkubwa sana zaidi ya kile tunachosoma magazetini. Kumbnuka wakati ATC ilipotakiwa kuuzwa Ufisadi ndio ulikuwa ktk hali ya juu sana, hivyo mimi na wewe hatuwezi kufahamu masharti yaliyofungamana na ununuzi wa ATC kumbuka tu mkono wa serikali ulikuwa bado upo ndani..Kwa mfanyabiashara yeyote ambaye hapendi siasa ndani ya biashara ni vigumu kuwekesha fedha zake pale serikali inapokuwa mdau kwani politics zitaingia. Kwa hyo ATC kama ingekuwa shirika binafsi na likataka kuuzwa ungeona mashirika kama Gulf na Emirates yakijitokeza.. My point being, kama leo tunataka kuuza ATCL ni lazima mkono wa serikali utoke..ATCL iwe shirika huru incoporated la wanahisa ndio member of the board across. Na hata siku moja sifikirii ATCL inaweza kutoka ktk pango hili ikiwa chini ownership ya serikali 100%...Tazama tofauti kati ya ATCL na mashrika yote duniani hata hiyo Air Canada, Ba, SAS au hata Kenya Airways!..wameweza kusimama kwa sababu ya kuuza shares. Hao Uganda Air imekufa kwa sababu kama zetu..

ATC na South Africa ilikuwa deal tu mkuu wangu kwa sababu jinsi ATC ilivyoendeshwa inaonyesha wazi kabisa kwamba ATC ilikuwa another goldmine..
Naweza kusema tatizo kubwa la ATCL kwa South Africa limekuja badilika wakati soko la biashara kwa wananchi wafanyabiashara lilipohamia Ulaya na Asia..wasafiri wengi walikuwa wakienda China, India na Europe badala ya South kama ilivyokuwa awali...Na panga la South lilipokuwa zito kwetu (kulingana na mkataba) tulijikuta hoi bin Taaban na kama ulivyosema Kenya, Suth Africa na Precision wote hawa hawakuwa wanunuzi isipokuwa kutafuta kutawala soko..Kosa kubwa lililofanyika wakati wa kujiengua hatukuwa tayari ku face dunia mpya ya biashara za usafiri wa anga..
Option zipo nyingi mkuu wangu kama ulivyosema lakini bado naamini kabisa hili linawezekana ikiwa kuna Uwazi na ATCL kuingia ktk soko letu, sii ajbau huyo mwenye Emirates mwenyewe anaweza kununua share!
 
Mkandara:

Unajua waholanzi wengi wanakuja Tanzania kwenye utalii kwa kutumia KLM. Ninavyosikia KLM walitaka kuingia ubia na ATCL, lakini inasemekana dili na South Africa ilijaza mifuko ya watu. Hivyo KLM wakabwagwa chini.
 
Zakumi,

Nadhani huna taarifa kamili ya waholanzi(KLM) Serikali ya Tanzania(ATC).

Waholanzi walionesha nia ya kuingia kwenye ubia na Tanzania kwenye ATC katika kipindi cha serikali ya awamu ya kwanza chini uongozi wa Mwalimu. Waliweza kutoa misaada mbalimbali ikiwemo ya kusomesha marubani na mafundi wa ndege za aina ya Fokker 27. Nia na malengo ya waholanzi pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kutuuzia ndege za aina Fokker 27. Na kweli tulinunua ndege hizo na tukaendelea kufanya nao biashara ya vipuli na matengenezo makubwa. serikali pia ikanunua ndege ya aina Fokker 28 na pia baadae Fokker 50. Lakini utengenezaji wa ndege hizo ulikwisha koma kutokana na sababu mbalimbali.

Wakati waholanzi walipokuwa na interest ya kuingia ubia, sera za nchi yetu zilikuwa haziruhusu kwani Azimio la Arusha lilikuwa bado liko hai. (Njia kuu za uchumi lazima zimilikiwe na umma). Kwa maana hiyo basi statement yako ya kusema kuwa KLM walikataliwa kwa vile South African walikuwa wamewajaza watu mifuko inaonesha mapungufu katika kufanya utafiti (RESEARCH) wa hali halisi ya mambo.

Hizi hapa ni facts, sasa unaweza kuzifanyia kazi.

1) Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hatukuwa na uhusiano wowote na serikali ya Afrika Kusini wakati huo kutokana na sera za ubaguzi wa rangi.

2) Wakati serikali ilipouza hisa zake 49% kwenye ATCL, KLM ilikuwa tayari inamiliki 26% ya hisa za Kenya Airways ilizokuwa imezinunua muda mrefu.

3) Kumbuka hata serikali ya awamu ya Tatu haikuweza kuuza hisa zilizokuwepo ndani ya Air Tanzania Corporation (ATC) kwa vile shirika hilo lilianzishwa kwa kutumia sheria maalum ya bunge (Act of Parliament). Serikali ilichokifanya ni kuanzisha Kampuni nyingine Air Tanzania Co. Ltd (ATCL) kwa kutumia ile sheria maarufu iliyopo katika chapter 212 (Cap. 212 of Companies Ordinance Act)

Nadhani nimejaribu kuweka mambo kwenye mstari
 
Pundamilia07,
Mkuu samahani hapa kidogo nitatofautiana na wewe kuhusiana ubia wetu na KLM..
haiwezekani kuwepo fikra za ubia kati yetu na Uholanzi awamu ya kwanza kwa sababu ulizozisema wewe mwenyewe. isipokuwa labda mkataba wa contract za biashara..Kisha wakati wa awamu ya kwanza hakuna shirika lolote duniani lilikuwa na Ubia na mtu. Ni wakati biashara ya ndege ilipokuwa kubwa kiasi kwamba karibu kila nchi duniani ilikuwa na shirika lake hadi mwaka 1982 mafuta yalipopanda na kufuatiwa economic meltdown wakati wa Reagan ndipo ubia ulipoanza ku save mashrika mengi ya ndege au magari.
Kanma unakumbuka awamu ya kwanza ndege za kigeni zilizokuwa zikija Tanzania zilkuwa zaidi ta mashirika 10, KLM, BA,Swiss, SAS, Aeroflot, Sabena, Alitalia, Air France, Air India, PIA, acha mbali za ndani Afrika na nyingine kibao ambazo zote siwezi kuzitaja zote...mashirika yote haya yalikuwa hayana Ubia na mtu mwingine..

Kwa hiyo, hili swala la Ubia limekuja baadaye na kwa sababu kubwa ya kiuchumi (utandawazi na soko huru) ili kuweza kushindana, pia kutokuwa na mipaka ya biashara kama nilivyoelezea huko nyuma jinsi ATCL inavyoweza kufanya kazi na Emirates kuongeza wateja wakati huo huo wakipunguza misafara kwa kugawana kazi za ndani na nje..
Chini ya Ujamaa wa Nyerere ni ndoto kufikiria kwamba Nyerere angeweza kufanya hivyo kwa sababu alikwisha sema hawezi kugeuka jiwe hadi pale tulipopigwa na vumbi la kiuchumi...
 
Mkuu pundamilia,sijui niseme uliona mbali ,nalisikitikia sana ile kampuni,nafikiri we uliona ulivyokuwa jikoni watu walivyokuwa wanachota..ile kampuni naisikitikia sana hata kabla ya kuondoka nilishauri mengi tu na nini cha kufanya wengi wakajua mi natafuta nafasi
MATUMIZI
uongozi umekuwa na matumizi mengi yasiyo na ridhaa na mengine kwa kutumia,nguvu kutumia pesa za kampuni...

MIKOPO:
Kulikuwa na mikopo ya ajabu ajabu ambayo hata kama atakuja CEO gani na kuwekka manegement chafu..kama hiyo iliyo tanzania atcl nina hakika hata wapewe billion kumi hataweza kufika popote kama mwenyekiti wao wa bodi anavypiga kelele...
kumekuwa na mikopo ya viongozi bila kuangalia uwezekano wa kampuni kufa ama walifikiri hata wakiondoka wataachwa...mfano mmojawapo wa kusikitisha ni

CEO:nakumbuka wakati naondoka alipewa mkopo wa miilioni 100...ambayo mpaka leo hii tuna ushahidi ni millioni kumi tu ndio iliolipwa toka aingiziwe kwenye account yake

DIRECTOR'S
HAWA WAMEJIKOPESHA SH MILLION 80 KILA MMOJA PASIPOKUJUA IPO SIKU WATAKOSA PESA YA MAFUTA YA NDEGE.....HAWA WAKO 7 ZIDISHA MARA 80 INATOKA NGAPI=

ACHA MATUMIZI MENGINE MACHAFU...NAFIKIRI KWA USHAURI WA MWISHO WAZIRI AAMUE TU KUMSHAURI RAISI AIFUTILIE MBALI HIYO MANAGEMENT NA KUWEKA WAPYA HARAKA KUIKOA ATCL..HAWA WALIOPO HAWANA MPANGO WA KURUSHA NDEGE SI LEO WALA KESHO......

MI NASHANGAA SANAA IWEJEE MTU KAMA CEO ANADAIWA HELA NYINGI HIVYO NA AENDELEE KUKALIA KITI....CHA KUSIKITISHA ANA MADENI YA TICKETI ZA BURE ZAIDI YA MILLIONI 10 BILA KULIPA ...KWA KUTOA DIRECTION WAPEWE HAWA...SASA NAFIKIRI UMEFIKA WAKATI WA KUAMUA SERIKALI KAMA WANAAIITAJI ATCL AMA LA KULIKO KUWAPOTEZEA WATU MUDA WAO.....KUMEKUWA NA MALALAMIKO HATA MIKOPO WANAYOKATWA HAWAIPELEKI SEHEMU HUSIKA..M NAFIKIRI KIONGOZI ATAKAINGIA AJITAHIDI KUWASAIDIA KUJUA YALE MAKATO YALIENDA WAPI......HAIWEZEKANI MTU ANASTAFU AJUI HATA PPF YAKE IKO AMA LAH.....

WAKUU HUU MUDA TUMSHAURI RAISI NANI AMBE ANAWEZA KUONGOZA ATCL..MEANS AWE NA SIFA GANI...
 
Zakumi,

Nadhani huna taarifa kamili ya waholanzi(KLM) Serikali ya Tanzania(ATC).

Waholanzi walionesha nia ya kuingia kwenye ubia na Tanzania kwenye ATC katika kipindi cha serikali ya awamu ya kwanza chini uongozi wa Mwalimu. Waliweza kutoa misaada mbalimbali ikiwemo ya kusomesha marubani na mafundi wa ndege za aina ya Fokker 27. Nia na malengo ya waholanzi pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kutuuzia ndege za aina Fokker 27. Na kweli tulinunua ndege hizo na tukaendelea kufanya nao biashara ya vipuli na matengenezo makubwa. serikali pia ikanunua ndege ya aina Fokker 28 na pia baadae Fokker 50. Lakini utengenezaji wa ndege hizo ulikwisha koma kutokana na sababu mbalimbali.

Wakati waholanzi walipokuwa na interest ya kuingia ubia, sera za nchi yetu zilikuwa haziruhusu kwani Azimio la Arusha lilikuwa bado liko hai. (Njia kuu za uchumi lazima zimilikiwe na umma). Kwa maana hiyo basi statement yako ya kusema kuwa KLM walikataliwa kwa vile South African walikuwa wamewajaza watu mifuko inaonesha mapungufu katika kufanya utafiti (RESEARCH) wa hali halisi ya mambo.

Hizi hapa ni facts, sasa unaweza kuzifanyia kazi.

1) Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hatukuwa na uhusiano wowote na serikali ya Afrika Kusini wakati huo kutokana na sera za ubaguzi wa rangi.

2) Wakati serikali ilipouza hisa zake 49% kwenye ATCL, KLM ilikuwa tayari inamiliki 26% ya hisa za Kenya Airways ilizokuwa imezinunua muda mrefu.

3) Kumbuka hata serikali ya awamu ya Tatu haikuweza kuuza hisa zilizokuwepo ndani ya Air Tanzania Corporation (ATC) kwa vile shirika hilo lilianzishwa kwa kutumia sheria maalum ya bunge (Act of Parliament). Serikali ilichokifanya ni kuanzisha Kampuni nyingine Air Tanzania Co. Ltd (ATCL) kwa kutumia ile sheria maarufu iliyopo katika chapter 212 (Cap. 212 of Companies Ordinance Act)

Nadhani nimejaribu kuweka mambo kwenye mstari

Pundamilia07:

Nadhani posti yangu nilitumia misamiati inasemekana/nilivyosikia. Hivyo sikuwa na authority au sikuweza authenticate kile nilichosema. Nimesema kama rumor.
 
Back
Top Bottom