Hotuba zenye maneno kama haya hazitapatikana tena kwenye tanzania hii.....

Hayo maneno tu hayana utendaji wala hayana maana sana wla hayajatuletea jema lolote Tanganyika zaidi ya kututumbukiza kwenye lindi la umaskini.

Nyerere alikuwa ni mpiga porojo mzuri lakini utendaji na uongozi wa kuiendeleza nchi ulikuwa patupu. Ndio maana mpaka leo tunalalamika kuwa eti ni maskini, ukweli ni kwamba Mungu katupa kila utajiri Tanzania lakini katunyima akili, moja wapo ni hili la kushabikia mtu aliyetuweka kizani mpaka leo. Huu ni umaskini wa akili.

Nawaonea huruma sana, mnaomshabikia Nyerere, kwa lipi zaidi? lakini hakuna cha kuwaeleza kwani hamtouona ukweli kwa kuwa akili zenu zimefikia kikomo cha kuona, hizo ndio Fikra Pevu.


Kuna siku ulisema kitu watu wakakushambulia sana kwenye jukwaa la elimu, uliwajibu vizuri, nikashangaa, sikutegemea hekima ile kutoka kwako, unajua ukiona mtu alivovaa tu unaweza kukadiria ni busara kiasi gani yuko nayo kwenye kichwa.

Post hii sasa ndio inaendana kabisa na wewe, Perfect Match!

Kama mtu haamini aangalie picha ya FaizaFoxy katika avatar yake utaona inafanana kabisa ni kiwango cha busara alicho nacho
 
Kichwa cha habari na yaliyoongelewa ndani havijalandana na cjaelewa hapa wamaanisha nini

duh! kama hujaelewa ujue hutakaa uelewe, it must be bigger than what you can chew, achana na haya makitu ya humu nenda facebook, kule utaelewa haraka, vya huku vigumu
 
Wakuu tazameni hotuba za Baba yetu kupitia ITV sasa hivi,hizi hotuba zina mshiko kwelikweli...........
 
Umesema vizuri kiongozi. Kosa kubwa tunalolifanya sisi waTz ni kumchukulia Nyerere kama mtu asiye kuwa na makosa wala mapungufu. Tunge kuwa tunaangalia mapungufu yake pengine tungekuwa tumejifunza mambo mengi sana na tuenge epuka kurudia makosa yale yale. Lazima tukubali kwamba Nyerere kama mwanadamu alikuwa na mambo mengi mazuri lakini alikuwa na mapungufu mengi tu. viongozi wetu wa leo bado wanayatumia mapungufu yake kwa vile hatuja amua kuyaweka wazi kuwa haya yalikuwa ni mapungufu. Moja ni hili la kumuweka mtu kizuiizini bila ya kumfungulia mashitaka ya kutoa rushwa. Ukitumia akili kidogo tu utajiuliza kwa enzi ya zama za Nyerere alishindwa vipi kumtia hatiani kwa tuhuma za rushwa. Tubadilikene jamani vinginevyo nchi hii haitatoka hapa ilipo.

katika moja ya hotuba zake alishawah kukiri kuwa hata serikali yake iliwah kufanya mambo ya kipuuzi(kwann isifanye wakat imekaaa miaka 25??,,,ila akasema serikali za sasa badala ya kuchukua mazuri ya awamu yake zinaendelea na mabaya ya awamu yake
 
duh! kama hujaelewa ujue hutakaa uelewe, it must be bigger than what you can chew, achana na haya makitu ya humu nenda facebook, kule utaelewa haraka, vya huku vigumu

hahahaaaa,,,,,wazo lako mujarabu
 
ALIJENGA VIWANDA WAKAJA HAO MNAOWAITA MARAIS WATENDAJI WAKAVIUA, LEO HII KUNA MAGOFU KIBAO SEHEMU NYINGI SANA AMBAYO YALIKUWA VIWANDA AMBAVYO MWALIMU ALIVIJENGA. wAMEUA RELI, WAMEUA ATC, TANESCO HOI, WAMEUA KIWANDA CHA URAFIKI, WAMEUA VYAMA VYA USHIRIKA.HIVYO VYOTE VILIANZISHWA CHINI YA UONGOZI WA MWALIMU HALAFU KANATOKA KAJITU JKANASEMA ALIKUWA MPIG KELELE TU. RIP MWALIMU, WE REAL MISS U.
 
Namchukulia mwalimu sawa na mzee masikini sana aliyetumia rasilimali yake karibu yote kumpeleka mtoto wake shule, akafaulu na kuwa na maisha mema, lakini kijana baada ya kupata neema, akasahau naye kutimiza wajibu wake kwa wanafamilia wengine.

Sasa hapo ukoo unapotumbukia kwenye lindi la umasikini zaidi, utamlaumu mzazi eti hakutumia muda wake kuuendeleza ukoo? Nyerere did his job, waliofuata wameamua kutumia resources bila akili, asilaumiwe yeye
 
Hotuba hizi kwa Tanzania tutazisikia kama tutabadilisha tume ya Uchaguzi na kupata kiongozi mwenye msimamo kama DR Slaa, kwa Afrika zimebaki kutoka kwa watu waaili tu Julius MALEMA na Bob Mugabe, RIP Mwl. Nyerere
 
Back
Top Bottom